Ijumaa, 18 Novemba 2016

MADHARA YAKUKAA MUDA MREFU KWENYE KITI AU CHINI


Pengine tayari unafahamu kuwa kutokujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara ni hatari kwa afya yako. Ndiyo hilo ni jambo ambalo kila mtu analijuwa (common sense). Vipi lakini ikiwa ni kweli unajitahidi kila siku kutimiza jukumu hilo la kufanya mazoezi dakika 30 hadi lisaa limoja na wakati huo huo unatumia masaa mengi ukiwa umekaa kwenye kiti, ukiangalia TV masaa mengi, masaa mengi umekaa na una kazi katika Kompyuta?.

Ndiyo wewe unadhani kwakuwa unaenda kufanya mazoezi kila siku basi hiyo inatosha, si ndiyo?. Ukweli ni kuwa hata kama wewe ni mtu wa kutembeatembea hapa na hapa lakini kama masaa mengine mengi yanatumika ukiwa umekaa kwenye kiti, mwili wako unakuwa karibu na magonjwa mengi bila mwenyewe kutambua.

Haya ndiyo madhara 7 ya kiafya utakayoyapata ukiwa ni mtu wa kupenda kukaa masaa mengi kwenye kiti au chini kila mara

1. Kunakosesha kupata oksijeni ya kutosha

Mara nyingi ukiwa umekaa unapenda kuegemea mgongo na siyo kukaa wima umenyooka, matokeo ya mkao huu ni kuzuia oksijeni kutembea kwa uhuru wote ndani ya mwili na mapafuni kwa ujumla.

Kisayansi tunapumua kwa uhuru wote tukiwa tumesimama na siyo tukiwa tumekaa. Ukiwa umesimamaa ndipo mapafu hupata uwezo wa kujitanua mpaka mwisho na hivyo kuweza kutoa hewa chafu na kuingiza hewa safi ndani kiurahisi zaidi. Hali hii ya kukosa oksijeni ya kutosha mwilini hujulikana kwa kitaalamu kama ‘hypoxia’. Wanasema kukaa kwenye kiti masaa matatu tu ni sawa na mtu aliyevuta sigara 6. Bila kupata oksijeni ya kutosha mwilini mwako kunapelekea magonjwa mengi mwilini bila idadi.

2. Unapata kirahisi kansa ya titi na kansa ya tumbo

Kansa ya titi na kansa ya utumbo mpana mara nyingi imeonekana kujitokeza kwa watu wa kula kulala yaani wale wasiopenda kujishughulisha na mazoezi ya viungo. Kituo cha kudhibiti magonjwa cha Marekani (CDC) kimesema maisha ya kula kulala yanaweza kukuweka kuwa karibu karibu na kansa kwa zaidi ya 40%. Hii ndiyo sababu wanawake wengi wanapatwa na kansa ya matiti miaka hivi karibuni sababu wengi wao ni watu wa kukaa tu nyumbani masaa mengi tofauti na wanaume ambao hutembea huku na huko kutafuta riziki ya kila siku. Kuepuka kansa ya matiti na kansa ya utumbo mpana epuka kukaa kwenye kiti masaa mengi.

3. Una uwezekano zaidi wa kupatwa na maradhi ya moyo

Matatizo katika mfumo wa upumuwaji ndiyo moja ya matokeo makubwa unaweza kuyapata ukiwa ni mtu wa kupenda kukaa kwenye kiti masaa mengi. Ni matokeo ya kutokupata oksijeni ya kutosha kama matokeo ya kukaa kwenye kiti masaa mengi. Kwenye utafiti mmoja uliohusisha watu 800,000, wale waliokuwa wakikaa kwenye kiti masaa 10 kila siku walikuwa na uwezekano mara 147 zaidi wa kupatwa na magonjwa ya moyo kuliko wale waliokaa kwenye kiti masaa machache au mara moja moja.

Kuna tafiti nyingi zinazokubaliana na nadharia hii na inatokana na ukweli kwamba ukiwa umekaa ni rahisi mafuta mengi kujilundika mwilini mwako kuliko ukiwa umesimama. Kadri unavyokaa masaa mengi kwenye kiti ndivyo vimeng’enya vinavyofanya kazi ya kuchoma mafuta mwilini vinavyokuwa na nguvu chache kuchoma hayo mafuta. Na tatizo la unene au uzito kupita kiasi lina uhusiano wa moja kwa moja na matatizo mbalimbali ya moyo.

4. Itakuwa vigumu kitambi na uzito kukuisha

Umewahi kujaribu kufanya mazoezi, kubadili chakula au hata kufunga na bado ukawa unasumbuliwa na kitambi au uzito kuwa mkubwa? Basi jibu la tatizo lako ni kukaa kwenye kiti masaa mengi. Utafiti unaonyesha kukaa tu kwenye kiti hata kama hauli chakula kingi bado utaendelea kuongezeka uzito.

Kwahiyo kama unataka kuondoa kitambi au tumbo au kupungua uzito kwa haraka acha kukaa masaa mengi kwenye kiti, hata kama kazi yako ni ya ofisini jaribu namna unaweza kupata meza ya kusimama huku unaendelea na kazi yako.

5. Ni rahisi kupatwa na ugonjwa wa Kisukari

Unataka kupona au kuepukana na Kisukari aina ya pili? Basi acha kukaa kwenye kiti muda mrefu.  Moja ya hatari zaidi za kukaa kwenye kiti masaa mengi ni kuwa mwili unakuwa hauitiki vema kwa insulin jambo ambalo ni matokeo ya kukaa masaa mengi kwenye kiti na hii ni matokeo ya kuzalishwa kwa wingi kwa kongosho kupita inavyohitajika kama matokeo ya kukaa muda mrefu.

Wakati ukiwa umekaa tu kwenye kiti kongosho linaendelea kutengeneza insulin lakini katika mwili huo uliokaa tu, insulin inakuwa haitumiki vema na mwili jambo linalomaanisha kuwa damu sukari (glucose) haiondolewi kwenye mzunguko wa damu kwa haraka. Hivyo uwezekano wa kupata Kisukari unaongezeka kwa zaidi ya asilimia 14 kwa Yule mwenye tabia ya kukaa masaa mengi kwenye kiti kuliko mtu mwingine yoyote.

6. Utapatwa na maumivu ya nyuma ya mgongo

Ukiwa ni mtu wa kupenda kukaa kwenye kiti masaa mengi kuna uwezekano ukawa haukai hata mkao mzuri kiasi cha kuwa karibu na maumivu ya mgongo kila mara. Watu wa namna hii pia huwa na maumivu ya kwenye uti wa mgongo kila mara. Kwa mjibu wa utafiti wa Taasisi ya 'DNA India' wagonjwa wengi wenye matatizo ya uti wa mgongo ni wale wenye miaka 20 na 30 na wengi wao ni wale hufanya kazi wakiwa wamekaa kwenye kiti masaa mengi.

Miaka ya sasa ni rahisi kukutana na watu wanaolalamika kupatwa na maumivu ya mgongo na wengi wao ukiwachunguza ni wale wanaotumia masaa mengi kukaa kwenye kiti.

7. Utakufa ukiwa bado kijana

Shirika la afya duniani limesema mtindo wa kukaa masaa mengi kwenye kiti ndiyo unaohusika na kuongezeka kwa uzito na unene kupita kiasi katika nchi nyingi zilizoendelea. Na uzito kupita kiasi ni moja ya tatizo kubwa la afya kwa mtu mzima yoyote kuwa nalo ingawa wengi hawaelewi hilo, wengi hasa waAfrika wakiwa wanene au wenye uzito mkubwa ndiyo hudhani hiyo ni afya. Uzito na unene kupita kiasi huja na matatizo mengine makubwa ikiwa ni pamoja na matatizo katika mfumo wa upumuwaji, kisukari, stroke, kukosa usingizi nk na haya yote yanaweza kupelekea wewe kufa ukiwa bado kijana.

Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Harvard mwaka 2014 ulitoa hitimisho kwamba kukaa kwenye kiti masaa mengi ni moja ya sababu ya vifo vya mapema kwa watu wengi. Mtandao wa Huffington ulienda mbali zaidi na kusema kukaa kwenye kiti masaa matatu tu kwa siku ni sawa na mtu aliyevuta sigara 6 na kuwa kukaa kwenye kiti masaa mengi kunaua watu wengi zaidi duniani kote.

Pamoja na kuwa kusimama ni bora zaidi kuliko kukaa, bado unatakiwa utumie muda fulani kukaa pia, usisimame masaa yote kutwa nzima, ukisimama masaa matatu tumia nusu saa nyingine kukaa hivyo hivyo mpaka siku yako inaisha.

Jumapili, 6 Novemba 2016

MAGONJWA YANAYOTIBIKA KWA KUTUMIA MBEGU ZA MABOGA


Mbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya mhimu zaidi mwilini kama madini ya zinki, kopa, maginizia, manganizi na chuma, mbegu za maboga ni tamu na zinaweza kutafunwa nyakati zozote na mahali popote hasa kwa wapenda kutafuna-tafuna kama mimi. Tafiti mbalimbali zimethibitisha pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida nyingi kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10 yafuatayo:

1. UGONJWA WA MOYO:

Kiasi kingi cha madini ya magnesium katika mbegu za maboga yanazifanya mbegu hizi kuwa mhimu sana kwa watu wenye magonjwa mbalimabli ya moyo. Madini ya magnesium ni mhimu kwa ajili ya kuimarisha msukumo wa damu kwenye moyo na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hatimaye kutibu na kuzuia magonjwa ya moyo. Mbegu  hizi pia zina mafuta mengine mhimu zaidi kwa watu wa ugonjwa wa moyo yenye OMEGA 3.

2. HUIMARISHA KINGA YA MWILI:

Mbegu za maboga zimebarikiwa kuwa na kiasi cha kutosha cha madini ya zinki (zinc). Kazi kubwa ya madini ya zink ni kuimarisha kinga ya mwili. Upungufu wa madini ya zink unaweza kupelekea matatizo kadhaa mwilini ikiwemo kuzaa watoto njiti, chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo shuleni kimasomo na matatizo mengine kadhaa ya kimwili na kiakili.

3. HUONGEZA UWEZO WA MACHO KUONA

Mbegu za maboga zina Vitamini E, vitamini A, lutein, beta-carotene na zeaxanthin, vitu hivi vinavyopatikana katika mbegu za maboga ni mhimu kwa ajili ya nuru ya macho. Vitamini A na madini ya zinki ni mhimu kwa ajili ya uzalishaji wa ‘melanin’ kimeng’enya mhimu ambacho hutengenezwa kwa asili na mili yetu kwa ajili ya ulinzi wa afya ya macho.

4. KINGA YA KISUKARI

Kisukari ni moja ya ugonjwa unaoendelea kwa kasi kuwasumbua watu wengi kila pembe ya dunia. Mbegu za maboga zina vitu vitatu mhimu zaidi ambavyo ni ‘Nicotinic acid’, ‘Trigonelline’ na ‘D-chiro-inositol’ ambavyo husaidia kushusha damu sukari mwilini na kudhibiti kazi za insulini hivyo kuwa kinga na kuleta ahueni kubwa kwa watu wenye kisukari.

Kama unasumbuliwa na kisukari fanya mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku na unipe mrejesho hapa.

5. DAWA BORA YA USINGIZI

Mbegu hizi zimegundulika pia kuwa na kirutubisho kinachozalisha homoni za usingizi. Kwenye mbegu za maboga kuna vimeng’enya viwili mhimu zaidi ambavyo huhusika na usingizi na afya ya akili moja kwa moja navyo ni ‘L-tryptophan’ na ‘tryptophan’. Gramu 100 tu za mbegu za maboga zina kiasi cha kutosha cha ‘tryptophan’ mpaka mg 576. Tryptophan ndiyo inahusika kuleta usingizi mlolo na mtulivu pia huondoa msongo wa mawazo au stress mwilini. Kwa kuongezea mbegu za maboga zina kiasi kingi cha vitamin kundi B. Muda mchache kabla ya kwenda kulala tafuna mbegu za maboga na utapata usingizi mtulivu kabisa mpaka asubuhi.

Kwahiyo kama una tatizo la kukosa usingizi jaribu kutumia mbegu za maboga na uniletee majibu hapa. Kumbuka kukosa usingizi mara nyingi huwa ni matokeo ya msongo wa mawazo na kama ulivyoona mbegu hizi zinaondoa pia stress! Kazi ni kwako ndugu.

6. DAWA BORA YA UVIMBE

Mbegu za maboga zinao uwezo mkubwa wa kuondoa sumu mwilini sambamba na uvimbe (inflammation). Kama ujuavyo sehemu kubwa ya vivimbe mwilini ni matokeo ya sumu kadhaa mwilini. Mbegu za maboga zitakuondolea uvimbe mwilini bila kukuachia madhara yoyote mabaya hapo baadaye.  Kama unasumbuliwa na uvimbe popote jaribu kutumia mbegu za maboga na utuletee majibu. Mbegu za maboga pia ni dawa nzuri kwa aina nyingi za kansa mwilini.

7. HUONGEZA MAZIWA KWA MAMA ANAYENYONYESHA

Mbegu za maboga zina protini nyingi bora itokananyo na mimea isiyo na madhara kama ile ya kwenye wanyama. Pia zina OMEGA 3. Mama mjamzito hata unayenyonyesha tumia mbegu za maboga na utakuwa na uhakika wa kutoa maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto.

8. DAWA NZURI KWA MATATIZO YA TEZI DUME

Wataalamu wengi wa lishe wanapendekeza mbegu za maboga zitumike kwa wanaume wa rika zote yaani vijana hadi wazee kwani zimethibitika kuwa msaada mkubwa kwa afya ya tezi dume. Tafiti nyingi zinasema mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya Zinki madini mabayo ni mhimu SANA kwa afya ya tezi dume na husaidia uponyaji wa tatizo la tezi dume moja kuwa kubwa kuliko nyingine tatizo lijukanalo kwa kitaalamu kama ‘benign prostatic hyperplasia’. Wanaume kazi ni kwenu.

9. ZINAONGEZA NGUVU ZA KIUME

Maajabu mengine ya mbegu za maboga ambayo ulikuwa huyajuwi bado. Utaniuliza kivipi zinaondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume? Kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo/stress kitu ambacho ni namba kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, lakini pia zinashusha lehemu (cholesterol), zinatibu kisukari, zinatibu tezi dume (matatizo kama ya ngiri nk), inashusha kisukari, ina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na mbaya kuliko zote ni kuwa zina madini ya ZINKI madini mhimu kuliko kitu kingine chochote kwenye upande wa nguvu za kiume na kinga ya mwili. Bado huelewi? Zina madini ya chuma pia

Uzuri ni kuwa mbegu hizi hazina uchungu wowote,  ni tamu kuzitafuna wakati wowote na mahali popote hata ofisini unaweza kuwa nazo pembeni unatafuna huku unaendelea na kazi zako. Sambamba na hilo kama tulivyoona pale juu kwamba zinaongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha kwa upande wa wanaume zinaongeza pia uwingi wa mbegu za kiume (sperm count) ukitafuna mbegu za maboga siku mbili tu utaona ukipiga bao linatoka la kutosha na zito kweli kweli basi ujuwe ni mbegu za maboga hizo.

10. ZINAONDOA PIA MSONGO WA MAWAZO (STRESS)

Msongo wa mawazo au stress kama mlivyozoea wengi ni tatizo linaloendelea kuwasumbua watu wengi miaka ya sasa. Mbaya zaidi wengi huwa hawaelewi nini madhara ya hizo stress wanazojipa. Yaani stress au msongo wa mawazo unaweza kukuletea magonjwa mengine mwilini zaidi ya 50, hivyo ni jinsi gani unahitaji kuweka chini stress zako na uendelee na maisha kwani kuendelea kuwa ni stress ni hatari zaidi kwa afya yako.

Moja ya sababu kuu ya watu wengi kuwa na stress ni usawa usio sawa wa homoni zao (hormonal imbalance). Hivyo kama una tatizo la homoni kwenye mwili hebu weka mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku na hutakawia kuona tofauti. Mbegu za maboga zina kimeng’enya mhimu sana kwa kutuliza mawazo kiitwacho ‘tryptophan’ na asidi amino zingine mhimu zinazohusika kutengenezwa kwa homoni nyingine ijulikanayo kama ‘serotonin’. Kama ulikuwa hujuwi ni kuwa serotonin ni homoni inayohusika na kazi mhimu sana ya kurekebisha matendo ya kitabia na kutoa matokeo chanya kwa mambo yanayohusu usingizi, hali ya mawazo kwa ujumla na mamabo yanayohusu njaa.

Mbegu za maboga ni msaada mkubwa kwa kina mama waliofikia ukomo wa siku na huondoa matatizo ya kiafya yatokanayo na kukoma kwa hedhi. Ni msaada kwa watu wenye saratani mbalimbali, huimarisha ukuaji na ustawi wa mifupa na meno, huondoa harufu mbaya ya kinywa na husaidia pia wenye tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara.

Namna nzuri ya kula mbegu za maboga:

Unaweza kula zikiwa kavu na ndiyo utapata faida nyingi zaidi ingawa mimi napenda kuzikaanga kidogo kama dakika 15 hivi na huwa nazichanganya na maji ya chumvi ya mawe ya baharini kidogo kwa mbali ili kupata radha.

NB.
Unahitaji ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako cha mbegu za maboga kwa siku ujazo wa kama nusu kikombe cha chai hivi kwa siku