Ijumaa, 18 Novemba 2016

MADHARA YAKUKAA MUDA MREFU KWENYE KITI AU CHINI


Pengine tayari unafahamu kuwa kutokujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara ni hatari kwa afya yako. Ndiyo hilo ni jambo ambalo kila mtu analijuwa (common sense). Vipi lakini ikiwa ni kweli unajitahidi kila siku kutimiza jukumu hilo la kufanya mazoezi dakika 30 hadi lisaa limoja na wakati huo huo unatumia masaa mengi ukiwa umekaa kwenye kiti, ukiangalia TV masaa mengi, masaa mengi umekaa na una kazi katika Kompyuta?.

Ndiyo wewe unadhani kwakuwa unaenda kufanya mazoezi kila siku basi hiyo inatosha, si ndiyo?. Ukweli ni kuwa hata kama wewe ni mtu wa kutembeatembea hapa na hapa lakini kama masaa mengine mengi yanatumika ukiwa umekaa kwenye kiti, mwili wako unakuwa karibu na magonjwa mengi bila mwenyewe kutambua.

Haya ndiyo madhara 7 ya kiafya utakayoyapata ukiwa ni mtu wa kupenda kukaa masaa mengi kwenye kiti au chini kila mara

1. Kunakosesha kupata oksijeni ya kutosha

Mara nyingi ukiwa umekaa unapenda kuegemea mgongo na siyo kukaa wima umenyooka, matokeo ya mkao huu ni kuzuia oksijeni kutembea kwa uhuru wote ndani ya mwili na mapafuni kwa ujumla.

Kisayansi tunapumua kwa uhuru wote tukiwa tumesimama na siyo tukiwa tumekaa. Ukiwa umesimamaa ndipo mapafu hupata uwezo wa kujitanua mpaka mwisho na hivyo kuweza kutoa hewa chafu na kuingiza hewa safi ndani kiurahisi zaidi. Hali hii ya kukosa oksijeni ya kutosha mwilini hujulikana kwa kitaalamu kama ‘hypoxia’. Wanasema kukaa kwenye kiti masaa matatu tu ni sawa na mtu aliyevuta sigara 6. Bila kupata oksijeni ya kutosha mwilini mwako kunapelekea magonjwa mengi mwilini bila idadi.

2. Unapata kirahisi kansa ya titi na kansa ya tumbo

Kansa ya titi na kansa ya utumbo mpana mara nyingi imeonekana kujitokeza kwa watu wa kula kulala yaani wale wasiopenda kujishughulisha na mazoezi ya viungo. Kituo cha kudhibiti magonjwa cha Marekani (CDC) kimesema maisha ya kula kulala yanaweza kukuweka kuwa karibu karibu na kansa kwa zaidi ya 40%. Hii ndiyo sababu wanawake wengi wanapatwa na kansa ya matiti miaka hivi karibuni sababu wengi wao ni watu wa kukaa tu nyumbani masaa mengi tofauti na wanaume ambao hutembea huku na huko kutafuta riziki ya kila siku. Kuepuka kansa ya matiti na kansa ya utumbo mpana epuka kukaa kwenye kiti masaa mengi.

3. Una uwezekano zaidi wa kupatwa na maradhi ya moyo

Matatizo katika mfumo wa upumuwaji ndiyo moja ya matokeo makubwa unaweza kuyapata ukiwa ni mtu wa kupenda kukaa kwenye kiti masaa mengi. Ni matokeo ya kutokupata oksijeni ya kutosha kama matokeo ya kukaa kwenye kiti masaa mengi. Kwenye utafiti mmoja uliohusisha watu 800,000, wale waliokuwa wakikaa kwenye kiti masaa 10 kila siku walikuwa na uwezekano mara 147 zaidi wa kupatwa na magonjwa ya moyo kuliko wale waliokaa kwenye kiti masaa machache au mara moja moja.

Kuna tafiti nyingi zinazokubaliana na nadharia hii na inatokana na ukweli kwamba ukiwa umekaa ni rahisi mafuta mengi kujilundika mwilini mwako kuliko ukiwa umesimama. Kadri unavyokaa masaa mengi kwenye kiti ndivyo vimeng’enya vinavyofanya kazi ya kuchoma mafuta mwilini vinavyokuwa na nguvu chache kuchoma hayo mafuta. Na tatizo la unene au uzito kupita kiasi lina uhusiano wa moja kwa moja na matatizo mbalimbali ya moyo.

4. Itakuwa vigumu kitambi na uzito kukuisha

Umewahi kujaribu kufanya mazoezi, kubadili chakula au hata kufunga na bado ukawa unasumbuliwa na kitambi au uzito kuwa mkubwa? Basi jibu la tatizo lako ni kukaa kwenye kiti masaa mengi. Utafiti unaonyesha kukaa tu kwenye kiti hata kama hauli chakula kingi bado utaendelea kuongezeka uzito.

Kwahiyo kama unataka kuondoa kitambi au tumbo au kupungua uzito kwa haraka acha kukaa masaa mengi kwenye kiti, hata kama kazi yako ni ya ofisini jaribu namna unaweza kupata meza ya kusimama huku unaendelea na kazi yako.

5. Ni rahisi kupatwa na ugonjwa wa Kisukari

Unataka kupona au kuepukana na Kisukari aina ya pili? Basi acha kukaa kwenye kiti muda mrefu.  Moja ya hatari zaidi za kukaa kwenye kiti masaa mengi ni kuwa mwili unakuwa hauitiki vema kwa insulin jambo ambalo ni matokeo ya kukaa masaa mengi kwenye kiti na hii ni matokeo ya kuzalishwa kwa wingi kwa kongosho kupita inavyohitajika kama matokeo ya kukaa muda mrefu.

Wakati ukiwa umekaa tu kwenye kiti kongosho linaendelea kutengeneza insulin lakini katika mwili huo uliokaa tu, insulin inakuwa haitumiki vema na mwili jambo linalomaanisha kuwa damu sukari (glucose) haiondolewi kwenye mzunguko wa damu kwa haraka. Hivyo uwezekano wa kupata Kisukari unaongezeka kwa zaidi ya asilimia 14 kwa Yule mwenye tabia ya kukaa masaa mengi kwenye kiti kuliko mtu mwingine yoyote.

6. Utapatwa na maumivu ya nyuma ya mgongo

Ukiwa ni mtu wa kupenda kukaa kwenye kiti masaa mengi kuna uwezekano ukawa haukai hata mkao mzuri kiasi cha kuwa karibu na maumivu ya mgongo kila mara. Watu wa namna hii pia huwa na maumivu ya kwenye uti wa mgongo kila mara. Kwa mjibu wa utafiti wa Taasisi ya 'DNA India' wagonjwa wengi wenye matatizo ya uti wa mgongo ni wale wenye miaka 20 na 30 na wengi wao ni wale hufanya kazi wakiwa wamekaa kwenye kiti masaa mengi.

Miaka ya sasa ni rahisi kukutana na watu wanaolalamika kupatwa na maumivu ya mgongo na wengi wao ukiwachunguza ni wale wanaotumia masaa mengi kukaa kwenye kiti.

7. Utakufa ukiwa bado kijana

Shirika la afya duniani limesema mtindo wa kukaa masaa mengi kwenye kiti ndiyo unaohusika na kuongezeka kwa uzito na unene kupita kiasi katika nchi nyingi zilizoendelea. Na uzito kupita kiasi ni moja ya tatizo kubwa la afya kwa mtu mzima yoyote kuwa nalo ingawa wengi hawaelewi hilo, wengi hasa waAfrika wakiwa wanene au wenye uzito mkubwa ndiyo hudhani hiyo ni afya. Uzito na unene kupita kiasi huja na matatizo mengine makubwa ikiwa ni pamoja na matatizo katika mfumo wa upumuwaji, kisukari, stroke, kukosa usingizi nk na haya yote yanaweza kupelekea wewe kufa ukiwa bado kijana.

Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Harvard mwaka 2014 ulitoa hitimisho kwamba kukaa kwenye kiti masaa mengi ni moja ya sababu ya vifo vya mapema kwa watu wengi. Mtandao wa Huffington ulienda mbali zaidi na kusema kukaa kwenye kiti masaa matatu tu kwa siku ni sawa na mtu aliyevuta sigara 6 na kuwa kukaa kwenye kiti masaa mengi kunaua watu wengi zaidi duniani kote.

Pamoja na kuwa kusimama ni bora zaidi kuliko kukaa, bado unatakiwa utumie muda fulani kukaa pia, usisimame masaa yote kutwa nzima, ukisimama masaa matatu tumia nusu saa nyingine kukaa hivyo hivyo mpaka siku yako inaisha.

Jumapili, 6 Novemba 2016

MAGONJWA YANAYOTIBIKA KWA KUTUMIA MBEGU ZA MABOGA


Mbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya mhimu zaidi mwilini kama madini ya zinki, kopa, maginizia, manganizi na chuma, mbegu za maboga ni tamu na zinaweza kutafunwa nyakati zozote na mahali popote hasa kwa wapenda kutafuna-tafuna kama mimi. Tafiti mbalimbali zimethibitisha pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida nyingi kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10 yafuatayo:

1. UGONJWA WA MOYO:

Kiasi kingi cha madini ya magnesium katika mbegu za maboga yanazifanya mbegu hizi kuwa mhimu sana kwa watu wenye magonjwa mbalimabli ya moyo. Madini ya magnesium ni mhimu kwa ajili ya kuimarisha msukumo wa damu kwenye moyo na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hatimaye kutibu na kuzuia magonjwa ya moyo. Mbegu  hizi pia zina mafuta mengine mhimu zaidi kwa watu wa ugonjwa wa moyo yenye OMEGA 3.

2. HUIMARISHA KINGA YA MWILI:

Mbegu za maboga zimebarikiwa kuwa na kiasi cha kutosha cha madini ya zinki (zinc). Kazi kubwa ya madini ya zink ni kuimarisha kinga ya mwili. Upungufu wa madini ya zink unaweza kupelekea matatizo kadhaa mwilini ikiwemo kuzaa watoto njiti, chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo shuleni kimasomo na matatizo mengine kadhaa ya kimwili na kiakili.

3. HUONGEZA UWEZO WA MACHO KUONA

Mbegu za maboga zina Vitamini E, vitamini A, lutein, beta-carotene na zeaxanthin, vitu hivi vinavyopatikana katika mbegu za maboga ni mhimu kwa ajili ya nuru ya macho. Vitamini A na madini ya zinki ni mhimu kwa ajili ya uzalishaji wa ‘melanin’ kimeng’enya mhimu ambacho hutengenezwa kwa asili na mili yetu kwa ajili ya ulinzi wa afya ya macho.

4. KINGA YA KISUKARI

Kisukari ni moja ya ugonjwa unaoendelea kwa kasi kuwasumbua watu wengi kila pembe ya dunia. Mbegu za maboga zina vitu vitatu mhimu zaidi ambavyo ni ‘Nicotinic acid’, ‘Trigonelline’ na ‘D-chiro-inositol’ ambavyo husaidia kushusha damu sukari mwilini na kudhibiti kazi za insulini hivyo kuwa kinga na kuleta ahueni kubwa kwa watu wenye kisukari.

Kama unasumbuliwa na kisukari fanya mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku na unipe mrejesho hapa.

5. DAWA BORA YA USINGIZI

Mbegu hizi zimegundulika pia kuwa na kirutubisho kinachozalisha homoni za usingizi. Kwenye mbegu za maboga kuna vimeng’enya viwili mhimu zaidi ambavyo huhusika na usingizi na afya ya akili moja kwa moja navyo ni ‘L-tryptophan’ na ‘tryptophan’. Gramu 100 tu za mbegu za maboga zina kiasi cha kutosha cha ‘tryptophan’ mpaka mg 576. Tryptophan ndiyo inahusika kuleta usingizi mlolo na mtulivu pia huondoa msongo wa mawazo au stress mwilini. Kwa kuongezea mbegu za maboga zina kiasi kingi cha vitamin kundi B. Muda mchache kabla ya kwenda kulala tafuna mbegu za maboga na utapata usingizi mtulivu kabisa mpaka asubuhi.

Kwahiyo kama una tatizo la kukosa usingizi jaribu kutumia mbegu za maboga na uniletee majibu hapa. Kumbuka kukosa usingizi mara nyingi huwa ni matokeo ya msongo wa mawazo na kama ulivyoona mbegu hizi zinaondoa pia stress! Kazi ni kwako ndugu.

6. DAWA BORA YA UVIMBE

Mbegu za maboga zinao uwezo mkubwa wa kuondoa sumu mwilini sambamba na uvimbe (inflammation). Kama ujuavyo sehemu kubwa ya vivimbe mwilini ni matokeo ya sumu kadhaa mwilini. Mbegu za maboga zitakuondolea uvimbe mwilini bila kukuachia madhara yoyote mabaya hapo baadaye.  Kama unasumbuliwa na uvimbe popote jaribu kutumia mbegu za maboga na utuletee majibu. Mbegu za maboga pia ni dawa nzuri kwa aina nyingi za kansa mwilini.

7. HUONGEZA MAZIWA KWA MAMA ANAYENYONYESHA

Mbegu za maboga zina protini nyingi bora itokananyo na mimea isiyo na madhara kama ile ya kwenye wanyama. Pia zina OMEGA 3. Mama mjamzito hata unayenyonyesha tumia mbegu za maboga na utakuwa na uhakika wa kutoa maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto.

8. DAWA NZURI KWA MATATIZO YA TEZI DUME

Wataalamu wengi wa lishe wanapendekeza mbegu za maboga zitumike kwa wanaume wa rika zote yaani vijana hadi wazee kwani zimethibitika kuwa msaada mkubwa kwa afya ya tezi dume. Tafiti nyingi zinasema mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya Zinki madini mabayo ni mhimu SANA kwa afya ya tezi dume na husaidia uponyaji wa tatizo la tezi dume moja kuwa kubwa kuliko nyingine tatizo lijukanalo kwa kitaalamu kama ‘benign prostatic hyperplasia’. Wanaume kazi ni kwenu.

9. ZINAONGEZA NGUVU ZA KIUME

Maajabu mengine ya mbegu za maboga ambayo ulikuwa huyajuwi bado. Utaniuliza kivipi zinaondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume? Kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo/stress kitu ambacho ni namba kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, lakini pia zinashusha lehemu (cholesterol), zinatibu kisukari, zinatibu tezi dume (matatizo kama ya ngiri nk), inashusha kisukari, ina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na mbaya kuliko zote ni kuwa zina madini ya ZINKI madini mhimu kuliko kitu kingine chochote kwenye upande wa nguvu za kiume na kinga ya mwili. Bado huelewi? Zina madini ya chuma pia

Uzuri ni kuwa mbegu hizi hazina uchungu wowote,  ni tamu kuzitafuna wakati wowote na mahali popote hata ofisini unaweza kuwa nazo pembeni unatafuna huku unaendelea na kazi zako. Sambamba na hilo kama tulivyoona pale juu kwamba zinaongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha kwa upande wa wanaume zinaongeza pia uwingi wa mbegu za kiume (sperm count) ukitafuna mbegu za maboga siku mbili tu utaona ukipiga bao linatoka la kutosha na zito kweli kweli basi ujuwe ni mbegu za maboga hizo.

10. ZINAONDOA PIA MSONGO WA MAWAZO (STRESS)

Msongo wa mawazo au stress kama mlivyozoea wengi ni tatizo linaloendelea kuwasumbua watu wengi miaka ya sasa. Mbaya zaidi wengi huwa hawaelewi nini madhara ya hizo stress wanazojipa. Yaani stress au msongo wa mawazo unaweza kukuletea magonjwa mengine mwilini zaidi ya 50, hivyo ni jinsi gani unahitaji kuweka chini stress zako na uendelee na maisha kwani kuendelea kuwa ni stress ni hatari zaidi kwa afya yako.

Moja ya sababu kuu ya watu wengi kuwa na stress ni usawa usio sawa wa homoni zao (hormonal imbalance). Hivyo kama una tatizo la homoni kwenye mwili hebu weka mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku na hutakawia kuona tofauti. Mbegu za maboga zina kimeng’enya mhimu sana kwa kutuliza mawazo kiitwacho ‘tryptophan’ na asidi amino zingine mhimu zinazohusika kutengenezwa kwa homoni nyingine ijulikanayo kama ‘serotonin’. Kama ulikuwa hujuwi ni kuwa serotonin ni homoni inayohusika na kazi mhimu sana ya kurekebisha matendo ya kitabia na kutoa matokeo chanya kwa mambo yanayohusu usingizi, hali ya mawazo kwa ujumla na mamabo yanayohusu njaa.

Mbegu za maboga ni msaada mkubwa kwa kina mama waliofikia ukomo wa siku na huondoa matatizo ya kiafya yatokanayo na kukoma kwa hedhi. Ni msaada kwa watu wenye saratani mbalimbali, huimarisha ukuaji na ustawi wa mifupa na meno, huondoa harufu mbaya ya kinywa na husaidia pia wenye tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara.

Namna nzuri ya kula mbegu za maboga:

Unaweza kula zikiwa kavu na ndiyo utapata faida nyingi zaidi ingawa mimi napenda kuzikaanga kidogo kama dakika 15 hivi na huwa nazichanganya na maji ya chumvi ya mawe ya baharini kidogo kwa mbali ili kupata radha.

NB.
Unahitaji ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako cha mbegu za maboga kwa siku ujazo wa kama nusu kikombe cha chai hivi kwa siku

Jumatatu, 31 Oktoba 2016

UFUGAJI BORA SAMAKI


1.0 UFUGAJI WA SAMAKI

Ø  Ni kitendo cha kuzalisha samaki katika mabwawa, matenki au  Mifereji kwa lengo la chakula au kujipatia kipato

1.1 UMUHIMU WA UFUGAJI WA SAMAKI

Ufugaji wa samaki unazo faida mbalimbali ambazo ni:-

Ø  Kujipatia chakula bora na cha kutosha kwa ajiri ya familia na jamii.

Ø  Njia bora ya kujiajiri na kujiongezea kipato kutokana na mauzo ya samaki.

Ø  Hutoa fursa ya matumizi ya ardhi isiyofaa kwa ajili ya kilimo.

Ø  Ufugaji wa samaki hutoa nafasi ya kilimo mseto cha samaki na mazao/mifugo kwa wakati mmoja katika eneo moja, hivyo kutoa mavuno mengi.

1.2.0  MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA UFUGAJI WA SAMAKI;

1.2.1Mtaji

Ø  Mkulima anashauriwa kuhakikisha kuwa ana mtaji kabla hajaamua kufanya ufugaji wa samaki, kiwango cha mtaji kitategemea ukubwa wa mradi husika.

1.2.2        Soko

Ø  Ni vyema kujua upatikanaji wa soko pamoja na washindani wako kabla ya kuanzisha shughuli hii, japo kwa nchi yetu soko la samaki ni kubwa sana, hii inatokana na uhitaji mkubwa wa samaki katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

1.2.3        Elimu

Ø  Mkulima anapaswa kuwa na elimu ya kutosha  kuhusu samaki na jinsi ya kufuga ili aweze kuendesha mradi kwa urahisi, hivyo mkulima anaweza kutafuta mtaalam kutoka vyuo vya serikali au binafsi.

1.2.4        Upatikanaji wa mbegu(vifaranga) pamoja na chakula.

Ø  Mkulima anashauriwa kuwa na uhakika wa upatikanaji wa mbegu bora na chakula cha kutosha kwa ajili ya kulisha samaki.

1.2.5        Eneo la kufugia samaki

Ø  Ni vyema pia kutafuta eneo zuri kwa ajili ya kuchimba bwawa la kufugia samaki kwa kuzingatia upatikanaji wa maji kwa wakati wote wa msimu wa ufugaji, aina ya udongo, usalama na upatikanaji wa miundombinu husika (barabara, nishati ya umeme).

2.0       AINA YA SAMAKI;

2.1       Utafiti umefanyika katika nchi nyingina kuonelea kuwa samaki aina ya perege/ngege/sato [tilapia] anafaa kufugwa katika mabwawa kulinganisha na aina nyingine.       

2.2       Samaki wa aina hii wana sifa nzuri sana kwani; huishi kwenye maji yenye joto la kadri katika nchi nyingi, wanaweza kuzaana kwa wingi katika mabwawa, hula majani na chakula kingine chochote kinachopatikana kwa urahisi shambani au nyumbani, hukua kwa haraka, uvumilia sana changamoto za bwawa hii ikiwa ni  mabadiliko ya joto, hewa ya oksijeni, na pH, pia nyama ya samaki hawa ni tamu  na yenye ladha nzuri.

2.3       Kuna aina nyingi za sato(tilapia) kama vile Sato mwekundu, Sato wa Msumbiji, Sato mweupe na Sato wa Mwanza.                                                                                      

            Sato hawa hula mimea na majani, huhitaji chakula kingi na huzaana sana, wana doa moja kubwa kwenye pezi la   mgongoni. Sato hawa hula vijimea vya plankiton, hukua kwa haraka na wana mistari kwenye mikia. Aina nyingine za samaki zimechanganyikana na kuwa machotara hivyo siyo rahisi kuwatambua.

2.4       Sato wa  Mwanza ni moja kati ya aina ya tilapia inayoshairiwa kufugwa na wataalamu wengi kwa kuzingatia sifa mbalimbali tofauti na aina nyingine.

3.0    ENEO LINALOFAA KWA UFUGAJI WA SAMAKI AINA YA SATO:

3.1.1 Upatikanaji wa maji

3.1.1 Maji ni moja ya hitaji muhimu katika ufugaji wa samaki. Eneo litafaa kwa ufugaji wa samaki ni lenye maji ya kutosha kuendesha shughuli zote za ufugaji kwa kipindi husika.

3.1.2 Chanzo cha maji kwenye bwawa kinaweza kuwa; mto, mfereji wa kumwagilia, au chemi chemi. Bwawa linahitaji maji mengi na sio rahisi kujazwa na ndoo. Ili kuhakikisha kuwa bwawa linakuwa na maji ya kutosha muda wote, chanzo cha maji cha faa kuwa cha kuaminika.

3.1.3 Kama mkulima ana maji ya kujaza kwenye bwawa kwa msimu, inawezekana pia kufuga samaki. Lakini mkulima ahakikishe anapanda vifaranga vya samaki mwanzo wa msimu wa maji. Hii itatoa fursa kwa samaki kukua hadi kufikia kiwango cha kuvunwa kabla ya maji kukauka.

3.1.4 Kama wakulima wanatumia chanzo kimoja cha maji ni muhimu kuanzisha utaratibu ambao utawezesha wakulima wote kutumia maji hayo bila matatizo. Wafugaji wa samaki wanaweza kujaza mabwawa wakati wowote kutegemea ni kipindi gani maji hayatumiki sana kwa matumizi mengine.

3.1.5 Ili kuhakikisha kwamba bwawa halitumii maji mengi, ni muhimu kuimarisha kingo za bwawa kwa kushindilia vizuri udongo wakati wa ujenzi wa msingi wa bwawa. Hii ina maana kwamba udongo lazima uwe na kiwango kikubwa cha mfinyanzi. Udongo ambao unatumika kutengenezea vyungu au kufyatulia matofali ni mzuri sana kwa shughuli hii. Kama udongo hauna ufinyanzi wa kutosha bwawa litapoteza maji kwa urahisi na italazimu kuongezwa kwa maji mara kwa mara.

3.2 Aina ya udongo

3.2.1 Inashauriwa kuwa udongo wa tifutifu au mchanganyiko wa tifutifu na mfinyanzi ambao una uwezo wa kuhifadhi maji kwa muda mrefu unafaa zaidi kwa ufugaji wa samaki.

3.2.2 Udongo wa kichanga sio mzuri katika kushikilia maji lakini eneo lenye udongo wa aina hii linaweza kutumika kufuga samaki ikiwa mbinu mbalimbali zitatumika.

Zingatia

·         Kwa eneo lenye kichanga lakini lina upatikanaji wa maji ya kutosha mkulima anaweza kutumia mbinu ya kujaza mchanga kwenye mifuko ya saruji iliyokwisha kutumika na kuipanga kwenye kingo za bwawa ili kuimalisha kuta za bwawa. Kwakuwa mifuko inaweza kuoza kutokana na maji, inashauriwa ibadilishwe endapo kingo za bwawa zitaanza kumomonyoka na kuongeza tope ndani ya bwawa.

·         Karatasi ngumu ya nailoni yaweza pia kutumika kuzuia kupotea kwa maji na kulinda kingo za bwawa kumomonyoka.

·         Ujenzi wa kuta za bwawa kwa mawe au bwawa zima ni njia bora zaidi japo ni gharama ukilinganisha na mbinu nyingine.

Mifuko





















picha ya bwawa liliotengeneza kwa karatasi ya nailoni

nylon

kuta

3.3  Mambo mengine ya kuzingatia katika uchaguzi wa eneo la kufugia samaki

3.3.1        Eneo liwe na mteremko kiasi ili kusaidia shughuli nzima ya uingizaji na utoaji wa maji kwenye bwawa. Nguvu nyingi zitatumika kuchimba bwawa eneo lenye mwinuko mkali na ni vigumu kujaza au kutoa maji kwenye bwawa lililochimbwa eneo la tambarare

3.3.2        Eneo linatakiwa kuwa na miundombinu bora na lenye kufikika kwa urahisi ili kusaidia usafirishishaji wa mazao, vifaranga na mahitaji husika.

3.3.3        Eneo lisiwe na historia ya mafuriko, hii ni hatari kwa kuwa mafuliko yanaweza kuvunja kingo za bwawa hivyo kuhatarisha shughuli ya ufugaji.

3.3.4        Eneo lisiwe karibu na maeneo hatarishi kama vile viwanda, shughuli za kilimo zenye kutumia kemikali ili kuzuia madhara ya kikemikali.

3.3.5        Eneo liwe karibu na mmiliki ili kuimalisha ulinzi na urahisishaji wa uendeshaji wa shughuli za uzalishaji. 

7.0       VYANZO VYA MAJI KWA UFUGAJI WA SAMAKI;

7.1       Ni vyema mkulima kuchagua chanzo cha maji kinachofaa kulingana na mazingira yake pamoja na manufaa kwa mkulima.                                                                         

7.2       Unaweza kutumia maji ya kisima, chemichemi, ziwa, mto na bomba kwa kuzingatia sheria na taratibu husika.                                                                 

7.3       Matumizi ya maji ya bomba katika ufugaji samaki ni lazima uzingatie ushauri wa kitaalamu. Lakini mambo yafuatayo yanaweza kumsaidia mkulima kutumia maji ya bomba kama chanzo cha maji; kabla ya kuweka samaki maji yawekwe kwenye bwawa kwa takribani siku kumi, hii itasaidia kuondoa chlorini kwenye maji, mbolea na tembe za vitamin c zaweza pia kutumika kuharakisha uondoaji wa chrolini katika maji.

7.4       Yote hapo juu yaweza kufanyika katika kuondoa chlorine kwenye maji lakini njia sahihi ni matumizi ya dawa maalumu aina ya ………………inayopatikana madukani, japo ndani ya nchi yetu ni ngumu kuipata hivyo yaweza kuagiwa kutoka nje ya nchi.

8.0    GHARAMA ZA UCHIMBAJI WA BWAWA:

8.3    Gharama za uchimbaji zaweza kuainishwa katika makundi matatu; ushauri kutoka kwa wataalamu, gharama za uchimbaji na gharama za kuandaa bwawa kabla ya kuweka maji na wakati wa kuweka maji.

8.4    Gharama za uchimbaji wa bwawa zinatofautiana eneo kwa eneo na namna bwawa linavyochimbwa, hii ikihusisha nguvu na vifaa vitakavyotumika.

8.2    Ni vyema kuajiri watu kuchimba bwawa kuliko kutumia vifaa kama excavator, kama bwawa ni kubwa sana waweza kutumia vyote kwa pamoja. Bwawa linahitaji malekebisho mengi sana madogo madogo, hivyo matumizi ya watu kama nguvu kazi katika kuyafanya hayo ni muhimu.

4.0    KUSAFISHA ENEO, UCHIMBAJI WA BWAWA

4.1    Mara eneo linapochaguliwa, ni muhimu kuondoa majani, vichaka na miti yote. Mizizi ing’olewe kabisa kwa kuwa itaoza na kuacha mashimo ambayo yatasababisha maji kuvuja.

5.5    Mara eneo likisafishwa, bwawa lichimbwe kwa vipimo sahihi ili kujua ukubwa wa bwawa. Hii itasaidia katika uchimbaji, kujua ukubwa wa bwawa na idadi ya vifaranga watakao pandikizwa. Ni vyema kutumia kamba ili kunyoosha ukuta wa bwawa wakati wa uchimbaji.

4.3    Matuta yajengwe kwenye eneo lililosafishwa vizuri na ambalo halina mimea wala mawe kwa ajili ya kuzuia kupotea kwa maji. Pia udongo wa juu ambao una majani na mizizi usitumike kwa kutengenezea matuta ya bwawa.

4.4    Matuta yasijegwe katika eneo la kichuguu kuzuia kupotea kwa maji, japo ni vigumu na mara nyingine haiwezekani kabisa kuzuia uvujaji wa maji kwa aina hii.

8.2    Ni muhimu kuhakikisha kwamba matuta yanajishikilia vizuri kwenye ardhi. Hii inaweza kufanyika kwa kuchimba mfereji kuzunguka bwawa katikati ya eneo ambalo matuta yatajengwa.

4.2    Matuta lazima yashindiliwe vizuri kuzuia maji yasivuje. Njia rahisi ni kushindilia matuta kila baada ya kuweka sentimeta 30 za udongo. Hakikisha udongo unaloweshwa na kushindiliwa kwa kutumia kifaa chenye ubapa chini au kipande cha mti. Ushindiliaji wa aina hii ni sawa sawa na ushindiliaji wa sakafu ya nyumba. Ushindiliaji unafanya matuta kuwa imara na kutuamisha maji

4.0    Upana wa tuta la bwawa inategemeana na ukubwa wa bwawa,ni vyema uwe na mita 3 chini na mita 2 juu, mteremko(slope) katika ukuta wa bwawa ni kitu cha muhimu, hii ni kupunguza mmomonyoko,na inamrahisishia mhusika kuingia ndani ya bwawa kwa urahisi.

6.0    Kina cha bwawa ni vyema kitofautiane, hii ikiwa ni futi 3-4 sehemu ya kina kirefu na futi 1-1.5 sehemu ya kina kifupi. Eneo la kati lichimbwe katika namna itakayowezesha kupata slope ya bwawa katika utofauti wa kina cha juu na chini.

10.1  Bwawa likiwa na kina kifupi, itakuwa rahisi kwa maadui a samaki kukamata samaki. Pia bwawa likiwa na kina kifupi litapata joto haraka wakati wa mchana na kupoa haraka wakati wa usiku. Kwa hali hiyo joto la maji litabadilika sana kitu ambacho ni hatari kwa samaki katika bwawa

10.2  Sababu nyingine  ya kuwa na kina kinachostahili ni kwamba kwenye mabwawa yenye kina kifupi majani huota kwa kasi. Mimea kwenye bwawa la samaki ina athari sawa sawa na mimea shambani.

10.3  Wataalamu hawashauri kuchimba bwawa la kina kirefu kwa kuwa ni gharama, ngumu kulihudumia na kuvuna samaki…………

5.5    Urefu wa matuta utategemea wingi wa udongo, ukubwa wa bwawa na mfumo wa uvunaji wa samaki.

8.3    Ni muhimu pia bwawa lijengwe katika namna itakayoruhsu kujazwa na kukaushwa kwa maji kila inapohitajika. Hii ina maana kuwa maji yaingie bwawani sehemu iliyoinuka na yaweze kutolewa wakati wa kukausha kupitia sehemu ya chini ya bwawa.

5.4    Ili maji yafike sehemu ya bwawa iliyoinuka, mfereji wa kuchepushia maji kutoka kwenye

kijito utengenezwe.

5,3    Sehemu ya kuingiza maji iwekwe kwenye kina kifupi na ile ya kutolea maji iwekwe kwenye kina kirefu kwa kuzingatia picha hapo

FAIDA 27 ZA KIAFYA ZIPATIKANAZO KWA KUTUMIA ASALI NA MDALASINI

MDALASINI NA ASALI

Asali inafahamika vema Duniani kote kama mojawapo ya silaha ya kiajabu katika kupigana na magonjwa na matatizo yatokanayo na uzee. Sasa hivi, utafiti mpya umeonyesha kwamba uwezo wa asali unaweza kuongezwa maradufu kama itachanganywa na mdalasini wa kawaida.

Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea pamoja na kijarida cha afya na lishe, imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na mdalasini pamoja na michanganyiko {dawa} ya kusisimua iletayo afya bora.

Kama ifuatayo:

1. Ugonjwa wa Viungo/Maumivu na Uvimbe {ARTHRITIS}.

Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu moja ya asali pamoja na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko kimoja {cha chai} chenye mdalasini - na kuchua sehemu zilizoathirika. Nafuu hupatikana katika muda wa dakika moja.

Vinginevyo tengeneza chai-kikombe kimoja chenye maji moto, weka vijiko vya chakula -viwili vya asali kwa kijiko cha chai cha mdalasini. Kunywa asubuhi na jioni ili kuondoa maumivu.

Katika tafiti iliyofanyika hivi karibuni na chuo kikuu kimoja huko Copenhagen, madaktari waliwapa wagonjwa 200, {syrup} mchanganyiko wa kijiko kimoja *cha chai* cha asali na kimoja cha mdalasini kila asubuhi kabla ya kifungua kinywa. Asilimia 73% yao waliripoti nafuu kubwa ya maumivu yao na ongezeko katika kufanya shughuli kama kujongea na kutembea vyema.

2. kukatika kwa nywele {HAIR LOSS}

Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta vuguvugu ya olive, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork. Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15.

3. Ukungu wa miguuni {FUNGUS}

Changanya kijiko kikubwa cha mezani cha asali, vijiko viwili vya mdalasini {vya chai}. Pakaa sehemu zilizoathirika usiku kwa muda wa nusu saa, kisha safisha kwa sabuni na maji. Shida yako itakwisha kwenye kipindi cha wiki moja.

4. Maambukizo kwenye kihofu cha mkojo {BLADDER INFECTION}

Bilauri ya maji vuguvugu yaliyochanganywa na vijiko viwili {vya chai} vya mdalasini na kijiko kimoja {cha chai} cha asali huondoa bacteria kwenye kibofu. Unaweza ukatumia juisi ya cranberry badala ya maji ikiwa ambukizo la kibofu linakuwa sugu.

5. Maumivu ya jino {TOOTHACHE}.

Changanya sehemu tano za asali, na sehemu moja ya mdalasini na tumia kwa maumivu ya jino.

Dondoshea kwenye jino au meno yaliyoathirika hadi maumivu yatakapotoweka.

6. Vidonda vitokanavyo kwa mgonjwa kulala kwa muda mrefu {CANKER

SORES}.

Saladi ya kupaka vidonda iliyochanganywa na asali pamoja na mdalasini kwenye chai ya raspberry

nyekundu ni dawa nzuri ya kuondoa maumivu makali ya canker sores.

7. Helemu {CHOLESTERAL}

Kipimo cha helemu cha watu waliokuwa na afya nzuri {katika jaribio} kilishuka kwa wastani wa asilimia 10 katika muda pungufu ya masaa mawili baada ya kunywa bilauri moja {ounce 16} yenye vijiko viwili vikubwa vya mdalasini iliyochanganywa na chai ya moto. Kinywaji hiki kutwa mara tatu kilifanya kazi nzuri ya kushusha kiwango cha helemu mwilini.

Madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta yanaweza kudhbitiwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai hii pamoja na chakula chako. Hii imeripotiwa na mtafiti maarufu Dr Alexander Andreyed na Eric Vogelmann.

Ugunduzi wao uliyakinishwa kwenye jarida mashuhuri la kitiba la Denmark July 1994. vilevile/ aidha uchunguzi mwingine ulibayanishwa kutoa matumizi ya kila siku ya asali safi hupunguza viwango vya helemu.

8. Mafua {COLDS}

Mafua yameshaeleweka ya kwamba hupotea/huondoka baada ya masaa machache baada ya waathirika kutumia kijiko kimoja {cha mezani} cha asali vuguvugu iliyochanganywa na robo kijiko{cha chai} cha mdalasini, mchanganyiko huu ni mahususi katika kusaidia kuondoa chafya na kuvimba koo. 

9. Ugumba {INFERTILITY}

Asali inaaminika kuamsha nyege na wapenzi wa jinsia zote mbili wanashauriwa kunywa anglao vijiko viwili {vya mezani} kila siku kabla ya muda wa kulala {usiku}. 

Mdalasini umetumika kwa muda mrefu kwenye dawa za kihindi na kichina ili kuongeza uwezo wa uzazi kwa kina mama wenye kuhitaji kuzaa.

Kiungo hiki {mdalasini} huchanganywa na kiasi cha asali na kufanya mgando {paste} ambao hupakwa kwenye fizi za meno na kunyonywa na kuingia mwilini taratibu.

Familia moja iliyokuwa haina watoto iltumia mgando huu kwa mafanikio na kupata mapacha wa kike baada ya kushindwa kwa muda wa miaka 14 kupata mtoto. Walikuwa wameshakata tamaa ya kupata mtoto hadi waliposikia kuhusu mchanganyiko huu wa asali na mdalasini.

10.Mchafuko wa tumbo {UPSET STOMACH}

Asali imetambuliwa kwa kipindi kirefu kama dawa ifaayo kuondoa mchafuko wa tumbo pamoja na kichefuchefu. Ongeza kiasi kidogo cha mdalasini na hii tiba ya kimaajabu vilevile itapunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.ll.Esidi/Gesi-Co2. Hco3. Hcl.

Kula asali pamoja na mdalasini huweza kuondoa mchafuko wa tumbo na utumbo uletwao na gesi kwa mujibu wa uchunguzi mahsusi iliofanywa huko India na Japan.

12.Ugonjwa wa Moyo {HEART DISEASE}

Unaweza kukinga kupata ugonjwa wa moyo na kuzuia mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye mishipa ya damu kwa kula asali na mdalasini mara kwa mara-kwa kupakaa wakati wa kifiingua kinywa.

Kula asali ya mkate wa ngano yenye nyuzinyuzi nyingi iliyopakwa kijiko kimoja {cha mezani} cha

mchanganyiko huo hapo juu kila siku. Tiba hii ya maajabu iliweza kupunguza kuganda kwa mishipa ya damu kwa 74% ya wagonjwa waliokuwa katika nyumba za kutunzia wagonjwa - utafiti mmoja ulionyesha.

13. Shinikizo la damu {HIGH BLOOD PRESSURE}

Shinikizo la damu pamoja na matatizo yaambatanayo ya maumivu ya kifua na kizunguzungu yalitoweka kutoka kwa wagonjwa wengi wiki chache tu baada ya watafiti wa kitaliano kuwapa dozi za mara kwa mara za asali ilyochanganywa na mdalasini. Vipimo vya shinikizo la damu vilionyesha

ukawaida na wote 137 waliofanyiwa jaribio hilo waliripoti kujisikia vyema/vizuri baada ya wiki chache za tiba hii ya ajabu.

14.Kinga ya mwili {IMMUNE SYSTEM}

Kinga yako ya mwili itaongezeka mara tatu zaidi ikiwa utatumia mara kwa mara asali na mdalasini kwa pamoja - wataalamu wanasema.

Utafiti wa kitiba unaonyesha kwamba hazina kubwa ya vitamini{vivurutubisho} na madini pamoja na michanganyiko mingine iondoayo magonjwa pamoja na kinga itolewayo na chembechembe nyeupe za damu, husaidia kuzuia magonjwa pamoja na kuharibu vimelea {virus} na {bacteria}.

15.Ukosefu wa nguvu za kiume [Uhanithi]{IMPOTENCE}

Asali ina historia ndefu ya kuamsha uume pamoja na kuwa dawa madhubuti ya kuponyesha uhanithi.

Kutokana na uwezo wake kama kiamshaji/chaji, asali ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya dini za kimashariki mwa Dunia. Mwaka jana, watafiti wa kiaustralia waligundua kwamba asali ina uwezo wa kupeleka mwili kutoa homoni mbalimbali kama ilivyo kwa mdalasini, katika Africa na dunia ya kusini, mabaharia wamekuwa wakipaka asali katika sehemu zao za nje ya uume ili kuongeza stamina zao za kufanya mapenzi.

16.Kutokuchaguliwa kwa chakula {INDIGESTION}

Vijiko viwili vya asali iliyonyunyiziwa mdalasini kabla ya mlo{kula chakula} huondoa kiungulia na wataalamu wanasema kwamba asali husaidia kutolewa kwa juisi zinazotumika kuchaguliwa kwa vyakula tumboni na mdalasini unaongeza spidi ya kuchaguliwa kwa vyakula.

17.Flu {INFLTJENZA}

Tafiti moja ya kihispania imethibitisha kwamba aina ya dawa moja asilia ya ajabu ambayo huharibu vairasi {vimelea} waletayo Flu.

18.Umri wa kuishi {LONGERVITY}

Unaweza kuishi kufikia hadi miaka 100 na kufurahia maisha ya afya na madhubuti kwa kunywa kila siku kikombe baridi cha chai ya mdalasini na asali. Kutengeneza kinywaji hiki kitamu, weka vijiko vine{vikubwa} vya mdalasini katika vikombe vitatu vya maji na koroga kwa dakika 10. kunywa robo kikombe kutwa mara tatu au nne na hivyo utakuwa na kinywaji kingi.

19.Chunusi {PIMPLES}

Changanya vijiko vitatu vya asali pamoja na kijiko kimoja cha mdalasini na pakaa kwenye chunusi.

Uwezo wa asali wa kuua bacteria utaufanya uso wako kuwa kawaida katika muda wa wiki mbili.

20.Kuumwa na wadudu {kwa washawasha} 

wenye sumu Pakaa asali na mdalasini moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia wakati mwasho unapokuathiri. Rudia tena hadi viuvimbe vinatoweka.

21.Madhara ya ngozi {INFECTIONS}

Fanya kama ilivyoelekezwa hapo juu. Rudia kufanya hivyo hadi hali itakapokwisha.

22.Kupungua kwa uzito

Wawezakufurahia vyakula vyote unavyopenda, kuwa na afya nzuri na kupunguza uzito wa mwili ambao hauhitajiki kwa kula chakula chenye nguvu na ladha nzuri, kilichojaa vitu viwili muhimu vya asili ambavyo ni asali na mdalasini.unachohitajika kufanya ni kuhakikisha unavitumia vyote kwa kiasi katika mapishi yako. Vilevile, wataalamu wanasema unaweza kuondoa mabonge ya uvimbe wa nyamanyama nje ya mwili kwa kuanza siku yako kwa kutumia vijiko viwili vya asali iliyochanganywa na kijiko kimoja cha mdalasini ndani ya bilauri ya maji vuguvugu. Rudia mchanganyiko huu kabla ya kulala.

Wakati wa kipindi cha baridi kinapokaribia, ambacho kinaambatana na mazoezi machache, kuongeza hivi vitu viwili vya asili katika chakula ni muafaka. Pia kinywaji hiki vuguvugu kimeshahakikishwa na wataalamu wa lishe kwamba hupunguza hamu ya kula pamoja na kuleta joto mwilini.

23.Saratani {CANCER}

Utafiti uliomalizika karibuni huko Australia na Japan, umeonyesha kuwa asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya mgonjwa anayetumia madawa ya kutibu saratani.

Katika tafiti iliyofanywa kwa wagonjwa waliokuwa wanaugua kwa kiwango kikubwa saratani ya mifupa na tumbo, wale waliokuwa wakitumia kila siku dozi za asali na mdalasini, walionyesha maradufu kupata nafuu kuliko wale waliokuwa wakitumia wakitumia madawa ya sarakani pekee. "Tuliwapa kijiko cha mdalasini na asali kutwa mara tatu kwa mwezi".anasema Dr Hiroki Owatta. "Wengine waliendelea na milo ya kawaida".

24.Uchovu {FATIGUE}

Upo ushahidi mpya kwamba sukari asilia zilizopo kwenye asali zina uwezo wa kuongeza nishati mwilini. Zikitumika ipasavyo, sukari hizi zinaweza kuwasaidia wazee na wengine wanaosumbuliwa na uchovu, wataalamu wanapendekeza kuchauganya nusu kijiko cha asali katika nusu bilauri ya maji, nyunyizia mdalasini na kunywa masaa mawili baada ya kuamka asubuhi. "Kunywa tena saa 9 alasiri wakati nishati {nguvu}inapoanza kushuka" anashauri Dr Milton Abbozza ambaye kazi zake kuhusu asali na mdalasini kama kichocheo cha nishati mwilini zinatambulika kimataifa. "katika wiki moja hii itajionyesha".

25.Kuvimba Nyayo {SORE FEET}

Chua asali na mdalasini vuguvugu katika {miguu} nyayo zilizoathirika baada ya siku ndefu na kazi au baada ya mazoezi marefu. Rudia kila asubuhi halafu nawisha nyayo kwenye maji baridi na vaa viatu.

26.Harufu mbaya kutoka mdomoni

Waamerica wa kusini wanasukutua kwa kutumia asali na mdalasini pamoja na vuguvugu kila asubuhi ili kufanya harufu toka mdomoni kuwa nzuri na safi kiasilia. Katika Asia ya kusini mashariki, watu hula kijiko cha mdalasini na asali ili kuondoa harufu mbaya mdomoni {halitosis}. Wataalamu wanaamini kwamba uwezo wa kuua bacteria uliopo kwenye asali ndiyo unaopigana na harufu mbaya itokayo mdomoni

MARADHI YANAYOTIBU HABBATI SODA 

)Kunyonyoka Nywele

Ataukanda unga wa Habbat-Sawdaa katika juisi ya chirichiri pamoja na kijiko cha siki nyepesi na kikombe cha mafuta ya zeituni, halafu asugue kichwani kwa mafuta hayo kila siku jioni pamoja na kukiosha kichwa kwa maji na sabuni kabla ya kupaka.

Maumivu ya Kichwa

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa , karafuu iliosagwa nusu ya kiwango cha Habbat-Sawdaa  na anisuni (anise), halafu achanganye pamoja. Achukue kiasi cha kijiko kimoja (cha chai), wakati wa kuumwa na kichwa, na ale na maziwa lala (mala), pamoja na kupasugua mahala paumapo kwa mafuta ya Habbat-Sawdaa .

Ukosefu Wa Usingizi

Atachukua kijiko cha Habbat-Sawdaa , achanganye na gilasi ya maziwa moto  yaliochanganywa na asali, baada ya kupoa kiasi atakunywa.

Chawa Na Mayai Yake

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa uliosagwa vizuri aukande kwenye siki mpaka uwe kama marhamu, halafu ajipake kichwani – baada ya kunyoa nywele au kuisugua marhamu kwenye mashina ya nywele, halafu aketi katika mwanga wa jua kitambo cha robo-saa. Na hataosha kichwa ela baada ya masaa matano. Atafanya hivyo kila siku kwa muda wa wiki moja.

Kisunzi Na Maumivu Ya Sikio

Tone moja la mafuta ya Habbat-Sawdaa ndani ya sikio husafisha sikio, pamoja na kuyanywa na kusugua sehemu za panda na nyuma ya kichwa, humaliza kisunzi.

Upaa Na Mabaka

Utachukua kijiko cha unga wa Habbat-Sawdaa, siki kiasi cha kikombe kimoja na juisi ya kitunguu saumu kiasi cha kijiko kidogo, vyote hivyo utavichanganya na vitakua namna ya   marhamu, utajipaka baada ya kunyoa sehemu  ya nywele na kuchanja kidogo – kisha utafunga bendeji, utaiacha mpaka asubuhi, baadae utajipaka mafuta ya Habbat-Sawdaa,utaendelea hivyo kwa muda wa wiki moja.

Malengelenge ya Neva katika Ngozi

Atajipaka – sehemu ya malengelenge – mafuta ya Habbat-Sawdaa mara tatu kila siku mpaka iondoke kwa Uwezo wa Allah.

Maradhi Ya Wanawake Na Uzazi

Dawa kubwa inayosahilisha kuzaa ni Habbat-Sawdaa iliochemshwa ikachanganywa na asali na kiziduo cha babunaji (chamomile). H abat sawdaa  ni kama burashi katika uke wa mwanamke yenye faida kubwa kwao pamoja na kutumua mafuta ya Habbat-Sawdaa katika kila kinywaji cha moto kwa maradhi yote ya wanawake.

Meno Na Maumivu Ya Mafido na Koo

Kiziduo cha Habbat-Sawdaa na kutumia kwa kusukutua kwa kugogomoa, husaidia mno maradhi yote ya mdomo na koo, vivyo hivyo pamoja na kubugia kijiko cha Habbat-Sawdaa na kumeza kwa maji yenye vuguvugu kila siku na kujipaka mafuta yake sehemu ya koo kwa nje na kuusugua ufizi kwa ndani.

Maradhi Ya Tezi

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa na aukande kwa asali na mkate wa nyuki kila siku, kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Chunusi (Acne)

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa aukande katika mafuta ya ufuta (simsimu) pamoja na kijiko cha unga wa ngano. Vyote hivyo atajipaka usoni kuanzia jioni hadi asubuhi, halafu ataosha kwa maji yenye vuguvugu kwa sabuni. Ataendelea kufanya hivyo kwa muda wa wiki moja. Na awe akinywa mafuta ya Habbat-Sawdaa katika kinywaji chochote cha moto.

Maradhi Yote ya Ngozi

Atachukua mafuta ya Habbat-Sawdaa, mafuta ya waridi (marashi jabali) na unga wa ngano asili, vyote hivyo  kwa viwango sawa, ule unga wa ngano uwe zaidi kuliko mafuta, halafu aukande vizuri. Kabla ya kujipaka, apanguse sehemu yenye ungonjwa kwa kitambaa kilichoroweshwa siki nyepesi, halafu aketi kwenye jua, baadae ajipake dawa hio kila siku. Lakini ajizuie na kila chenye kuchochea hisia kama vile, samaki, mayai, maembe na mfano wake.

Sugu (Chunjua) (Wart)

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa aukande katika siki nzito na asugue kwa kitambaa cha sufi au katani mahala pa sugu asubuhi na jioni kwa muda wa wiki moja.

Kuung`arisha Uso Na Kuurembesha

Ataukanda unga wa Habbat-Sawdaa katika mafuta ya zeituni, na atajipaka usoni halafu apigwe na mwanga wa jua kidogo. Tiba hiyo ataifanya wakati wowote katika mchana na siku yoyote.

Kuunganisha Mvunjiko Haraka

Supu ya adesi (dengu), kitunguu maji pamoja na yai la kuchemsha na kijiko kikubwa cha unga wa Habbat-Sawdaa , utachanganya na supu hiyo japo siku baada ya siku; halafu anywe. Na atasugua sehemu zilizo karibu na mvunjiko kwa mafuta ya Habbat-Sawdaa, na baada ya kufungua bendeji atajisugua kwa mafuta ya Habbat-Sawdaa yenye vuguvugu; kila siku.

Mvilio Wa Damu (Contusion)

Atachemsha vizuri konde moja la Habbat-Sawdaa katika chombo cha maji, kisha atakiingiza kiungo kilichovilia damu ndani ya maji hayo- yenye vuguvugu- kwa muda wa robo-saa au zaidi pamoja na kukitaharakisha kiungo hicho. Baada ya hapo atajipaka mafuta ya Habbat-Sawdaa bila ya kufunga kitu. Lakini hatakiwi kukipa uzito kiungo hicho au kukitaabisha. Tiba hiyo ataifanya kila siku kabla ya kulala.

Baridi Yabisi (Rheumatism)

Atachemsha mafuta ya Habbat-Sawdaa na atasugua kwayo ile sehemu yenye ugonjwa, atasugua kwa nguvu kama kwamba yuwasugua mfupa wala sio ngozi! Na atayanywa baada ya kuyachemsha vyema na kuyachanganya na asali kidogo. Ataendelea na tiba hiyo huku akiwa ni mwenye imani na yakini kuwa Allah Atamponya.

(Ki) Sukari (Diabetes)

Utachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kikombe kimoja, manemane (myrrh) iliosagwa kiasi cha kijiko kikubwa, habbarrashad nusu kikombe, komamanga iliosagwa kiasi cha kikombe kimoja, mzizi wa kabichi uliosagwa baada ya kukaushwa kiasi cha kikombe kimoja na kijiko kidogo cha mvuje. Vyote hivyo atavichanganya na atakula kabla ya kula chakula kiasi cha kijiko kimoja, atakula na maziwa lala ili iwe rahisi kumeza.

Shinikizo la Damu (High Blood)

Kila unywapo kinywaji cha moto, tia matone machache ya mafuta ya Habbat-Sawdaa. Pia ujipake mafuta hayo mwili wote, japo wiki mara moja.

Uvimbe Wa Figo(Nephritis)

Atatengeneza kibandiko (cha kitambaa) kutokana na unga wa Habbat-Sawdaa uliokandwa katika mafuta ya zeituni, atabandika sehemu yenye maumivu ya figo pamoja na kubugia funda la kijiko cha Habbat-Sawdaa kila siku kabla ya kula chakula kwa muda wa wiki moja tu; uvimbe utakwisha insha Allah.

Kuvunjavunja Vijiwe Vya Tumboni

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kikombe kimoja kisha aukande katika kikombe cha asali, na atasaga kitungu u saumu punje tatu; atakua akichukua nusu yake akila kabla ya kula chakula kila siku. Pia itakua bora lau atakula limau kila baada ya kula dawa; kwani husafisha kabisa.

Kukojoa Kwa Maumivu (Dysuria)

Atapaka mafuta ya Habbat-Sawdaa juu ya kinena kabla ya kulala pamoja na kunywa kikombe cha mafuta hayo yaliochemshwa na kutiwa asali; kila siku kabla ya kulala.

Kukojoa Bila Kukusudia

Atachukua Habbat-Sawdaa na maganda ya mayai yaliosafishwa na yakaokwa na kusagwa halafu yakachanganywa na Habbat-Sawdaa kisha yakaokwa na kusagwa halafu yakachanganywa na Habbat-Sawdaa kisha aingize kwenye maziwa; hatimae anywe kiasi cha kikombe kimoja kila siku na wakati wowote.

Jongo (Edema)

Ataweka kibandiko (cha kitambaa) cha unga wa Habbat-Sawdaa uliokandwa katika siki juu ya kitovu, kwanza ataweka kitambaa. Pia atakula Habbat-Sawdaa kijiko kimoja asubuhi na jioni kwa muda wa wiki moja.

Kifuko Cha Nyongo Na Vijiwe Vyake

Atachukua Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja, manemane iliosagwa robo kijiko na asali kiasi cha kikombe kimoja; vyote hivyo atavichanganya viwe mraba (kama jamu); halafu awe akila kila asubuhi na jioni.

Wengu

Ataweka kibandiko (kilichopashwa moto) cha Habbat-Sawdaa iliokandwa katika mafuta ya zeti katika ubavu wa kushoto; jioni. Na wakati huo huo ata kunywa kikombe cha kiziduo cha uwatu kilichochanganywa asali na mafuta ya Habbat-Sawdaa kidogo, ataendalea na dawa hiyo kwa muda wa wiki mbili mfululizo.

Maradhi Yote ya Kifua na Baridi

Atachukua mafuta ya Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kikubwa atie kwenye maji halafu ayaweke juu ya moto mpaka ianze kufuka moshi, hapo aanze kuuvuta ule moshi puani huku akiwa amejifunika kichwa ili ule moshi usiende upande mwingine. Atafanya hivyo kila siku kabla ya kulala, pamoja na kunywa kiziduo cha zaatari kilichochanganywa na unga wa Habbat-Sawdaa; asubuhi na jioni.

Moyo na Mzungukoa wa Damu

Kuwa na imani katika maneno ya Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wa sallam) Kwa sababu jambo hili ni katika muktadha wa imani. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wa sallam) alipotuambia kuwa Habbat-Sawdaa ni dawa ya kila ugonjwa, basi hakuna shaka hata chembe kuwa ni dawa ya maradhi yote yanayomfika mwanaaadamu. Mgonjwa wa moyo asikate tamaa kutokana na rehma ya Allah; ni juu yake akithirishe kutumia Habbat-Sawdaa kwa namna yoyote iwayo; iwe ni kwa kula nzima au kwa kunywa wakati wowote uwao.

Mchango (Msokoto Wa Tumbo) (Colic)

Atachemsha vyema anisunikamun na nana kwa vipimo sawa na atatia asali kidogo, halafu atie matone saba ya Habbat-Sawdaa ; atakunywa kinywaji hicho kikiwa na vuguvugu pamoja na kupaka mafuta ya Habbat-Sawdaa mahala panaposokota. Baada ya muda mchache maumivu yataondoka.

Kuhara

Atachukua juisi ya chirichiri iliochanganywa na unga wa Habbat-Sawdaa kijiko kikumbwa, atakunywa kiasi cha kikombe kimoja mara tatu kwa siku.

Uziwi

Atachemsha Habbat-Sawdaa pamoja na karafuu, na atakunywa bila ya kuongeza kitu; mara tatu kwa siku.

Gesi Na Maumivu

Atabugia unga laini wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja kabla ya kula chakula akifwatisha gilasi ya maji yenye vuguvugu iliotiwa asali ya muwa kiasi cha vijiko vitatu; atakariri kila siku kwa muda wa wiki moja

————————————————————————

Matumizi Ya Kunufaisha Ya Asidi (Acidness)

Motone kadhaa ya mafuta ya Habbat-Sawdaa yaliotiwa kwenye maziwa ya moto na asali; humaliza asidi.

Uvimbe Wa Tumbo

Atachukuwa unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja na kijiko cha urkusus (licorice) hivyo atavichanganya na juisi ya pea iliotengenezwa pamoja na kokwa zake; halafu anywe; ataona nafuu kubwa.

Maradhi Ya Macho

Atapaka mafuta ya Habbat-Sawdaa sehemu za panda kandokando ya macho na kope, atafanya hivyo kabla ya kulala pamoja na kunywa matone kadhaa ya mafuta ya Habbat-Sawdaa katika kinywaji chochote cha moto au katika juisi ya karoti.

Amiba (Vijidudu) (Amebiasis)

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja pamoja na kijiko cha kitunguusaumu kilichosagwa, atachangana katika kikombe cha juisi ya nyanya iliotiwa chumvi kidogo; atakunywa kila siku kabla ya kula chakula kwa muda wa wiki mbili mfululizo.

Kichocho (Bilharziasis)

Atakula Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja asubuhi na jioni, yawezekana kuila Habbat-Sawdaa katika chakula kama vile mkate pamoja na kujipaka mafuta yake katika ubavu wa kulia. Ataendelea na dawa hio kwa muda wa miezi mitatu mfululizo. Baadae atapata nguvu na nishati.

Kutoa Wadudu Tumboni

Atakula sandwichi moto ya vitu hivi: kijiko kimoja cha unga wa Habbat-Sawdaa, punje tatu za vitunguu, kijiko kimoja cha mafuta ya zeti, pilipilimanga kidogo na punje kumi za boga (calabash), asubuhi atakunywa kinywaji cha shimari au mafuta ya mbono mara moja pekee.

Utasa

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa, unga wa uwatu na mbegu ya figili kwa vipimo sawa, atakula kijiko kimoja asubuhi na jioni ilihali imekorogwa katika nusu kikombe cha asali, baadae atafuatisha kunywa kikombe kikubwa cha maziwa ya ngamia; basi inshaAllaah itakuwa kheri.

Tezikibofu (Prostate gland)

Atajipaka mafuta ya Habbat-Sawdaa chini ya mgongo na atajipaka chini ya korodani (mapumbu) na kusugua kwa mzunguko pamoja na kula unga wa Habbat-Sawdaa kijiko kimoja, na robo kijiko kidogo cha manemane katika nusu gilasi ya asali iliotiwa katika maji yenye vuguvugu; kila siku na wakati wowote apendao.

Pumu (Asthma)

Atanusa moshi wa mafuta a Habbat-Sawdaa asubuhi na jioni. Pia atakula unga wake asubuhi na jioni kabla ya kula chakula kila siku na pia kujipaka mafuta yake kifuani na kooni kabla ya kulala kila siku.

Kidonda

Atayachanganya matone kumi ya mafuta ya Habbat-Sawdaa, katika kikombe cha asali na kijiko kimoja cha maganda ya komamanga yaliyokaushwa na kusagwa. Atakula kila siku kabla ya kula chakula; baadae atakunywa gilasi ya maziwa yasiyotiwa chochote.

Saratani (Cancer)

Atapaka mafuta ya Habbat-Sawdaa mara tatu kila siku na kula kijiko cha unga wake kila amalizapo kula katika kikombe cha juisi ya karoti. Ataendelea hivyo kwa muda wa miezi mitatu.

Nguvu Za Kiume

Atachukua  unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja achanganye na kitunguu saumu kilicho twangwa,tangawizi mbichi,na asali.kisha chemsha maji nusu lita na kuchanganyia huko vitu vyote,chuja na utumia kwa siku moja kutwa mara 3 kwa kipimo hcho fanya hvyo wiki mara mbili

Udhaifu kwa Ujumla

Atachukua unga wa habat sosa kiasi cha kikombe kimoja, uwatu mfano wake na ambari ilioyeyushwa kiasi cha kijiko kidogo, vyote atavichanganya katika chombo chenye asali iwe kama jamu; halafu awe akila kama jamu kila siku na wakati wowote apendao lakini kwa mkate wa ngano asili.

Kuleta Hamu Ya Kula

Kabla ya kuanza kula, jipatie Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kidogo na uitafune kwa meno yako, na unywe maji ya kawaida yaliochanganywa na siki kidogo.

Kutibu Ulegevu Na Uvivu

Atakunywa- kabla ya kula – juisi ya machungwa iliochanganywa matone kumi ya mafuta ya Habbat-Sawdaa. Ataendelea hivyo kwa muda wa siku kumi.  Baada ya hapo ataona nishati na uchangamfu.

Nishati akilini Na Wepesi Wa Kuhifadhi

Atachemsha nanaa (mint leaf), aichanganye na asali na aingize matone saba ya mafuta ya Habbat-Sawdaa; anywe kinywaji hiki kikiwa na vuguvugu wakati wowote apendao. Basi ataionea namna fahamu itakavofanya kazi

Jumamosi, 29 Oktoba 2016

JE UNAISHI VEMA KWA KUBANA MATUMIZI NA KUWAZA UWEKEZAJI ?

Mara nyingi watu wengi hatuweki bajeti ya vitu,sababu hatuna lengo kuu la msingi na maisha
,
*PASIPO MAONO WATU HUACHA KUJIZUIA*
Maono,malengo,mipango,mikakati ya maisha ndo kitu kitakachokufanya namna gani ufanye matumizi yako

Je matumizi yako na kipato chako vinalingana??

A)MATUMIZI NYUMBANI 1.Epuka kununua vitu vya rejareja kwa "Mangi".Ukinunua nusu nusu kwa Mangi unauziwa bei ya juu japo utaona ni hela ndogo!

2.Weka daftari la matumizi nyumbani. kila kinachotumika kiandikwe iwe ni pesa au kiasi cha unga, mchele kilichotumika: itasaidia kudhibiti matumizi

3.Dhibiti pesa za "chenji" zinazorudi dukani hasa sarafu kwa kuziweka mahali maalum.Hizi wengi "huzipotezea" na ukipata dada wa kazi mjanja basi hizi hizi mpaka mwisho wa mwezi anajikuta amekusanya nusu ya mshahara wake bila wewe kujua! Ndio unashangaa unakaa nae miaka na miaka,Wewe unajisifu"nimeishi nae mwaka wa 7 huu,tunaishi kama ndugu ??kumbuka ndugu zake wako kijijini huko, hapo yeye anapiga hela wewe kaa tu unashangaa shangaa, kashangae kigamboni daraja jipya ila wezi wa zamani!

4.Nunua mizani ndogo ya kupimia uzito(bei rahisi) ili kupimia vitu nyumbani.Kuna wakati unapika chakula kingi kwa kukosa kipimo sahihi

5.Kuwa mbunifu kwa kupendelea mapishi yanayobana matumizi mf: badala ya chips kuku, unaweza kupika viazi rosti, utakuwa umefidia mafuta! utajiuliza ukipika rosti si nyanya, vitunguu vitahitajika? hata chips kuku utahitaji tomato source/kachumbari

6.Usinunue soda, tengeneza juice "simpo" mfano juice ya ukwaju. Watu10 ukiwanunulia soda utakuwa umetumia gharama zaidi kuliko ukitengeneza juice ya ukwaju

7.Mgeni asikulazimishe uharibu bajeti yako, Usijivimbishe sana kama alama ya kuuliza kwa kuleta ufahari na kulijaza friji ndiii! yani mpaka mgeni akiondoka una madeni kwa mangi ya mishahara miwili!.Simaanishi usimkirimu mgeni ila "cheza kwa step"

8.Usinunue maandazi kwa jirani, pika hata chapati za maji asubuhi,utabana matumizi kuliko kununua vitafunwa nje,chemsha vitu vya asili viazi na mengineyo.

9.Usizoeshe watoto tabia ya kuwapa hela hovyo!Kuwa na utaratibu maalumu,sio huyu amekuja anasema umpe mia ya pipi huyu anataka miatano ya chips..Hata kama unazo jifunze kuwapa kwa utaratibu na hakikisha unaandika.

10.Kama nyumbani nyote mnaondoka asubuhi,mwambie dada wa kazi azime umeme na awashe tu pale anapohitaji!Mara nyingi kuna kuwa na "lose connections" ambazo wakati mwingine zinakula umeme bila kujua, na hii ni kwa sababu hatuna utamaduni wa kufanya checkup ya mifumo ya umeme!

11.Taa izimwe kila mtu atokapo chumbani, taa iwashwe pale tu watu walipo. mf kwa nini taa ya chooni iwashwe wakati chooni hakuna mtu?haimaanishi tu giza likiingia basi kila taa iwashwe.Vitu vinavyotumia umeme vizimwe kabla ya kulala isipokuwa vya muhimu kama friji na taa za nje za usalama.

12.Nunua vifaa original-itakupunguzia gharama za matengenezo mara kwa mara

13.Jifunze kufanya matengenezo madogo madogo wewe mwenyewe sio hata bulb ikiungua kubadilisha mpaka uite fundi.

Ijumaa, 28 Oktoba 2016

Mambo 7 muhimu ya kuzingatia kutoka kuajiriwa hadi kujiajiri

Kuna sababu mbalimbali kwanini mtu atake kuajiri, badala ya kuajiriwa, mfano kipato kidogo anachopata katika kazi husika, hitaji la kutaka uhuru zaidi binafsi wa kufanya kazi, hitaji la kuweza kutoa ajira kwa wengine na zaidi sana kuweza kutumia vema kipaji na uwezo wa kuzalisha ambao katika kazi ya sasa mtu hapati nafasi ya kufanya hivyo. 

Kujiajiri ni jambo linalohitaji maandalizi ya muda mrefu na kuna mambo ya msingi kuyafahamu, haiwezekani tuu , ukaacha kazi na kusema ok, acha nijiajiri.

Makala hii inachambua mambo ya msingi ya kujiandaa na kuyafahamu kabla mtu hajaamua kuacha kuajiriwa.

Mkakati ni muhimu
Wazo au ndoto isiyo na mkakati wa kuitimiza ni upuuzi yaani ndoto hiyo au wazo hilo halina maana, hivyo basi ndoto yako ya kujiajiri siku moja, ni lazima iwekewe mkakati wa kuifanikisha ikiwa ni pamoja na muda hasa wa lini utaitimiza hiyo ndoto.

Katika kuweka mkakati huu wa kutimiza ndoto yako, fanya utafiti wa kina kuhusu mipango yako binafsi ya maisha, mtazamo wako kuhusu maisha, mpenzi/mke wako, familia yako, na hali ya jamii kwa ujumla inavyoenda kama vile mabadiliko ya hali ya kisiasa, teknolojia, na uchumi.

Tengeneza malengo ya aina ya shughuli unayotaka kuifanya ukiacha kuajiriwa, na pima uwezekano wa shughuli hiyo kufanyika kweli na kama itakulipa. Utambue pia aina ya watu na rasilimali nyingine utakazozihitaji, na jinsi utakavyozipata

1.unahitaji fedha
Ndio, unahitaji kiasi cha fedha za kutosha kununua vifaa na malighafi za kutengenezea bidhaa yako. Pia unahitaji fedha za kuwalipa wafanyakazi wako, na zaidi sana , unahitaji fedha za kuendesha maisha yako na familia yako , kwa kipindi fulani kabla ya biashara kuanza kukulipa mshahara. Hivyo kabla haujaacha kibarua chako, hakikisha umetengeneza bajeti ya kutosha na una akiba ya kutimiza mahitaji ya bajeti yako. Usingependa uache kazi halafu uanze kuwa omba omba kwa rafiki na jamaa, au uanze kujuta.

2.Network ni muhimu
Kumbuka katika kujiajiri kwako, utahitaji wateja, washirika, wafanyakazi na hata washauri mbalimbali ili mambo yako yaende vizuri. Hivyo, wakati ukiwa umeajiriwa ndio wakati wako muafaka wa kutengeneza na kupanua wigo wako wa watu unaowafahamu na waliokaribu nawe.

Kumbuka kuendeleza mawasiliano kwani watu hawapendi kuona wewe unataka kuwatumia tuu kisha unawatupa. Endeleza mawasiliano walau hata kwa salamu tuu. Zaidi sana, heshimu watu wote, hata usiowafahamu au wale unaodhani 'sio watu muhimu'.

Jenga taswira nzuri kwa jamii kwa lugha fasaha, picha na matukio mengine, usifanye watu wakufikirie vibaya.

3.Usipitwe na wakati:
Hakikisha kuwa unafuatilia taarifa za matukio, dili na watu wanaohusiana na aina ya shughuli unayopanga kuifanya wakati utakapojiajiri. Hii itakusaidia kupata uzoefu na kusoma alama za nyakati, na pengine kutambua fursa nyingine zaidi.

Endelea kujifunza zaidi kuhusu kazi yako, watu na jamii kwa ujumla kwani kujiajiri kunahitaji uzoefu zaidi, na zaidi sana uwezo wa kupambana na changamoto nyingi ambazo nyingine haujawahi kukutana nazo kabisa, ila taarifa za awali na kujua jinsi mambo yanavyoenda kwa ujumla katika jamii vitakufanya ushinde changamoto.

4.Maana halisi ya biashara
Baada ya kuacha kuajiriwa, hautarajii kuwa mtu wa ‘kuganga njaa’ yaani kufanya biashara ili mradi tuu hela iingie, lakini haujui mwelekeo wa biashara yako upoje, na wala hakuna mkakati wa kuikuza na kuimarisha biashara husika.

Biashara inahusu kutimiza mahitaji ya watu, kwahiyo ili mradi utakuwa na uwezo mkubwa wa kutimiza mahitaji ya watu, na kuendelea kuhamasisha watu zaidi kuja kwako uweze kutimiza mahitaji yao , basi biashara itakua, na itaendelea kuwa endelevu.

Kinyume cha hapo, ushindani utakutoa katika biashara kwani wateja watakambilia kwa wengine. Biashara sio tuu kupata wateja, ni vile kuweza kuendelea kupata wateja na kuendelea kupanua biashara.

Inabidi uipende shughuli husika unayoifanya, na uweze kutimiza mahitaji ya wateja kupitia biashara husika.

Muda wako mwingi utautumia katika shughuli yako mpya utakayojiajiri hivyo, kama ambavyo kazi uliyonayo pengine ‘inakuboa’, hakikisha ajira yako binafsi ‘haikuboi’.

5.Umuhimu wa wafanyakazi
Watendaji wa shughuli husika za biashara yako utakayoianzisha ni muhimu wawe wenye ujuzi na uzoefu wa kutosha wa kufanya shughuli husika, na uweke mikakati ya kuwapatia nyenzo zote muhimu za kufanyia kazi ikiwemo teknolojia na mazingira mazuri ya kazi. Hivyo basi wakati unajiandaa kujiajiri tilia maanani hili katika bajeti yako ya kuajiri. Usingependa wafanyakazi wao wajisikie vibaya kama vile wewe ulivyojisikia vibaya katika ajira yako fulani (pengine ajira yako ya sasa). Muda huu ambao umeajiriwa, ndio muda pia muafaka wa kusaka 'vipaji'- yaani watu ambao utafanya nao kazi utakapojiajiri.

6.Inakuhusu wewe 
Mafanikio yako katika kujiajiri yanategemea mambo mengi ila zaidi sana yanakutegemea wewe. Je, nini hasa sababu yako ya kutaka kujiajiri?

Ni kweli una bidhaa au huduma haswa ya kupeleka sokoni itakayokufanya iendeshe maisha yako na kuiendeleza biashara husika au ni hasira tuu za jinsi bosi wako anavyokuchulia hapo ofisini kwako, au kwakuwa mshahara uliopo sasa haukutoshi. Je, mipango yako mingine ya maisha ipoje?

Ndoto zako za kusoma, au kuishi sehemu tofauti tofauti, pengine mkoa mwingine tofauti na uliopo sasa, au pengine hata nchi husika. Je, yote hayo yanaathiri vipi mipango na mikakati yako ya kujiajiri, bila kusahau msukumo toka kwa familia yako.

7.Ndoto sahihi
Ni kweli kuwa upo sahihi kufikiria au kuota kufanya biashara kubwa na yenye mafanikio sana, lakini kumbuka mafanikio hayaji kwa usiku mmoja, na hata kama yatakuja kwa usiku mmoja, inahitajika kazi ya muda mrefu kuyafanya yawe endelevu.

Hivyo basi, usingoje wakati ‘muafaka’ wa wewe kuwa na kiasi kikubwa cha fedha au kwamba ‘umeyaset’ vema mambo yote.

Anza kidogo kidogo, kubali kufanya makosa, na tambua kuwa hata kama utafanya uchambuzi na uchunguzi wa kutosha kuhusu soko, jamii na teknolojia, hali halisi unayoenda kukumbana nayo inaweza kuwa tofauti na ile uliyojifunza wakati wa uchambuzi au uchunguzi wako kwakuwa hicho unachoenda kufanya ni kipya hakikufanyiwa uchambuzi, bali unakifanya kutokana na uchambuzi uliofanya hapo awali.

Kuna mtu mwingine atakuja kutumia makosa au mafanikio yako kupanga mambo yake.

Alhamisi, 27 Oktoba 2016

FAIDA KUMI ZA KUNYWA MAJI MOTO YENYE LIMAO

FAIDA KUMI ZA KUNYWA MAJI MOTO YENYE LIMAO KILA UNAPOAMKA ASUBUHI




1.Huongeza Kinga yako ya mwili hasa kupambana na magonjwa madogo kama mafua, na kikohozi kutokana na kuwa na vitamin C

2. Husafisha Mfumo wako wa chakula, kuondoa sumu mwilini na kuzuia tumbo kujaa gesi mara kwa mara

3. Huleta hewa safi kinywani. Ni Muhimu sana kwa watu wanaonuka midomo

4. Hukuongezea uchangamfu na kufanya siku yako ianze vizuri sana

5. Husaidia majeraha kupona kwa haraka kutokana na kuwa na ascorbic acid ya kutosha. Pia huimarisha mifupa

6. Husaidia mmeng’enyo wa chakula utakachokula asubuhi au mchana kwa kuondoa vikwazo vyote vinavyoweza kuzuia umeng’enyaji wa chakula.

7. Huimarisha Ngozi yako, kuondoa makunyanzi na kukupa muonekano mzuri.

8. Husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uzito kwani maji moto ya limao huyeyusha mafuta ya kutosha.

9. Huyapa macho yako afya nzuri na kuimarisha kuona.

10. Huondoa hali ya kuhitaji kahawa kila asubuhi ambayo si nzuri kiafya.

MATUMIZI tumia glas moja ya limao asubuhi baada ya kuswaki,au jioni kabla ya kula chochote.

Jumatano, 26 Oktoba 2016

WALIMU NA HARAKATI ZA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA.



WALIMU NA HARAKATI ZA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA.

Harakati za uhuru zimefanyika karibu nchi zote za Afrika,Tanganyika ni moja miongoni mwa nchi zilizotawaliwa na wakoloni wa Kijerumani na baadae wa kiingereza baada ya vita ya kwanza ya dunia.

Kwa miongo kadhaa nchi za Afrika zimekuwa chini ya uatawala wa kikoloni.Kipindi hiki cha Ukoloni kilikuwa kipindi kigumu sana kwa Waafrika kilichohusisha adha za kila aina.

Kwa Waafrika hawakupendezwa na ujio wa wakoloni,Hivyo toka awali Wafrika walianza kuonyesha hasira zao dhidi ya wavamizi katika ardhi yao tukufu.

Baada ya kipindi kirefu cha mateso na taabu kwenye kipindi cha ukoloni ndipo walipoibuka wanaharakati mbali mbali wa kupigani uhuru.

Harakati za kupigania uhuru zilianza tangu pale tu wakoloni walipoingia ingawaje harakati hizo za awali hazikuratibiwa kwa uzuri,pia hazikuongozwa na wasomi na nyingi ya harakati hizo zilifanywa kikabila Zaidi kuliko kitaifa.

Baada ya vita ya kwanza ya dunia harakati madhubuti za kupigania uhuru zilianza na baada ya vita ya pili ya dunia harakati hizi zilipamba moto safari hii zikiongozwa na wasomi pamoja na wazalendo waliotoka kupigana vita vya kwanza na vita vya pili vya dunia.

Wasomi wa kada mbali mbali walishiriki harakati za ukombozi wa Tangayika lakini Makala hii imejikita kwenye mchango wa walimu katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Walimu ni watu ambao wanakutana na watu wengi kwa wakati mmoja na hupata muda mwingi wa kuzungumza nao hivyo huweza tumia nafasi hiyo kupandikiza kile ambacho mwalimu anakiamini.

Mbali na vipawa vya kuzaliwa navyo lakini walimu wamejifunza saikolojia za watu hivyo hutumia nyenzo hiyo kama sehemu ya ushawishi na kukamilisha lile ambalo mwalimu anataka liwafikie watu,mfano kwenye filamu ya Sarafina Mwalimu Mary Masombuko alikuwa mwalimu mwenye ushawishi mkubwa na kufanikmiwa kupandikiza hisia za kizalendo kwa watoto wa kiafrika.

Katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika safari inaanza na Mwalimu Cecil Matola ambaye alikuwa mmoja ya waanzilishi wa African Association katika miaka ya 1927 pia vitabu vingine vimeandika 1929.Mwalimu Cecil Matola alipata braka zote za aliyekuwa gavana wa Uingereza kwa kipindi kile Sir David Cameroon.TAA iliundwa na watu 9 akiwemo Mwalimu Cecil Matola,Kleist Sykes,Mzee Bin Sud,Ibrahim Hamisi,Zibe Kidasi,Ali Said Mpima,Suleiman Majisu,Raikes Kusi na Rawson Watts.Mwalimu Cecil Matola mabaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa African Association alifariki dunia mwaka 1933 na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa katibu wake Ndugu Kleist Sykes.

Mwlimu James Aggrey ,Huyu ni mgana ambaye alikuatana na Kleist Sykes wakati huo Kleist Sykes ametoka vitani na akawa anafanya kazi Tanganyika Railways.Dr James Aggrey inasemekana ndiye aliyemuamasisha Kleist Sykes kwenda kuanzisha African Association ambayo baadae ikawa TAA kisha TANU.

Mwalimu Thomas Sauti Plantan,Huyu atakumbukwa kwa nafasi yake ya uraisi wa TAA miaka 1950s,katibu wake akiwa Mzee Clement Mohammed Mtamila walikumbana na mtihani wa kupinduliwa kwenye uongozi na vijana.Baada ya kupinduliwa kwenye madaraka Dr Vedasto Kyaruzi akawa rais wa TAA na Abdulwahiid Sykes mtoto wa Kleist Sykes akawa ndio katibu wake.

Mwalimu Kahere wa Tanga,Huyu atakumbukwa katika mchakato wa safari ya mwalimu Nyerere ya mwaka 1955 kwenda UNO Kwa ajili ya kudai Uhuru.Itakumbuka kuwa nauli ya kwenda Marekani wakati ule ilikuwa shilingi 12,000.Watu mbali mbali walichangia nauli pamoja na maradhi ya Mwalimu Nyerere kwa ajili ya kwenda UNO. Lakini pesa hazikutosha na ndipo Mwalimu Kahere wa Tanga alipowaambia viongozi wa TANU waende Tanga kuchukua pesa.Special branch(usalama wa taifa wa zama za mkoloni) walitaka kuzuia upatikani wa pesa hizo lakini walishindwa na hatimaye Idd Faizi Mafongo alifanikiwa kuzikabdidhi pesa kwa viongozi wa TANU na hatimaye Mwalimu Nyerere akaenda UNO tarehe 05/03/1955 ingawaje habari hii inapingana na anachoeleza Yericko Nyerere kwenye kitabu chake cha Ujasusi wa Kidola(2016) kwamba kwamba kanisa katoliki lililipia nauli ya tiketi ya ndege kwa kwenda na kurudi.

Mwalimu Kambarage Julius Nyerere,huyu ndio shujaa wa mwisho kwa walimu ambaye alifunga safari ya kwenda Umoja wa mataifa kwenda kudai uhuru wa Tanganyika na kwa jitihada zake huku akishirikiana na viongozi wengine wa TANU uhuru wa Tanganyika ulipatikana tarehe 9/12/1961.

Mwalimu Nyerere amefanya mambo mengi kutoka uhuru mpaka kifo chake kilichotokea tarehe 14/10/1999 katika hospitali St. Thomas huko nchini Uingereza.

Hivyo leo katika kumbukumbu ya kifo cha mwalimu Nyerere na pia tunawakumbuka wazalendo wengine ambao kwa namana moja au nyingine walifanikisha upatikanaji wa uhuru wa Tanganyika ingawaje wamesahaulika kwenye vitabu vyetu(kiada na ziada) vya kuwafundishia watoto mashuleni.

Makala hii imeandikwa kwa rejea za kitabu kiitwacho Maisha ya Abdulwahiid Sykes,Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi,ripoti ya Tadasu TSURUTA na mtandao wa wikipedia

JIFUNZE ASILI YA WACHAGA NA DESTURI YAO

WACHAGA ni kabila la kibantu linalopatikana Kaskazini mwa Tanzania katika mkoa wa Kilimanjaro.

Wachaga wanajishughulisha na kilimo cha viazi, ndizi na mtama. Zao la kahawa lilianzishwa na wakoloni karne ya 19 na kuendelezwa hadi leo kama zao la biashara. Pia wachagga hujihusisha na ufugaji wa ng'ombe, mbuzi na kondoo ili kupata samadi ya kurutubisha mashamba, nyama, maziwa.

Miaka ya nyuma ufugaji wa mbuzi au kondoo ulikuwa wa lazima ili kupata wanyama wa kutambika. Ilikuwa ni mwiko kutambika kwa kutumia mnyama wa kununua au kutoka nyumba nyingine. Kutokana na uhaba wa ardhi katika makao yao ya asili, Wachaga wametawanyika sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi wakijishughulisha na kazi mbalimbali ili kupambana na umasikini.

Ingawa baadhi ya hadithi za kale zinaeleza kuwa Wachaga walikuwepo eneo la Kilimanjaro na dua zao ndizo zilizorefusha mlima Kilimanjaro ili waweze kuwa karibu na Mungu, utafiti unaonesha kuwa Wachaga ni wahamiaji waliofika Kilimanjaro miaka 600 kabla ya ujio wa Kristo. Hivi sasa ni zaidi ya miaka 2000 baada ya Kristo.

Tafiti kuhusu makabila zinasema endapo Wachaga wataamua kutafuta asili yao kwa kuzingatia kizazi cha kale ni lazima wabishe hodi kwenye jamii za makabila mbalimbali hasa kwa Wakamba, Wamaasai na Wataita nchini Kenya, pia kwa Wapare, Wasambaa nchini Tanzania.

Tofauti na makabila mengine ambayo asili yao inatokana na kizazi kimoja, Wachaga wanaweza kujua asili ya kizazi chao kwa kufuatilia historia ya ukoo au historia ya makundi kulingana na eneo. Historia ya kale inasema kuwa jamii ya wachaga inatokana na watu wa makabila mbalimbali ambao walihamia kwenye mteremko wa mlima Kilimanjaro baada ya kukimbia vita na wengine kukimbia baa la njaa.

Pia wapo waliohamia eneo hilo baada ya kuvutiwa na ardhi yenye rutuba na hali nzuri ya hewa na inasemekana kuwa wahamiaji hao waliwazidi nguvu wenyeji wa eneo hilo ambao walijulikana kama Koningo au Konyingo. Baadhi ya wenyeji walihama ila inasemekana kuwa wengine walibaki na kujumuika na wahamiaji na baada ya kuishi pamoja kwa muda mrefu waliunda kabila jipya la wachaga.

Ingawa hakuna ushahidi wa kisayansi kuwa Wachaga walitokana na makabila mengine, simulizi za kale na mfumo wao wa maisha unadhihirisha kuwa hawatokani na kizazi kimoja wala wazee na viongozi wao hawajawahi kuwa na uhusiano wa karibu.

Ingawa watu hao huitwa wachaga wenyewe ni vigumu kujua nani hasa ni Mchaga kwa kuwa wenyeji hutambuana kwa kutumia lugha ya eneo husika kama vile
Mrombo,
Mmachame,
Muuru,
Mkibosho au Muanjo akimaanisha mchaga wa Marangu. Uongozi wa jamii ya Wachaga ulitumia mfumo wa machifu, maarufu kama Mangi.

Kila eneo lilikuwa na mangi wake, ila Mangi Sina wa Kibosho, Rindi wa Moshi na Marealle wa Marangu walipata umaarufu mkubwa, kutokana na jitihada zao za kutaka kuwa wafalme ili kutawala himaya nzima ya wachaga. Hata hivyo, jitihada hizo ziligonga mwamba kwa kuwa hakuna Mangi aliyekuwa tayari kutawaliwa na kiongozi kutoka kundi jingine.

Hali ya kujihami na kuogopana inachukuliwa kama kielelezo kuwa chimbuko la wachaga linatokana na jamii za makabila tofauti yenye historia tofauti.

Mfumo wa uongozi miongoni mwa wachaga umeathiri kizazi kipya kwa kuwa uzoefu unaonesha kuwa wachaga ni miongoni mwa jamii chache zinazopenda siasa za upinzani na hupenda kuchagua kiongozi kwa kupima uwezo wa mtu badala ya chama.

Kati ya mwaka 1750 na mwaka 1890 Wachaga walikuwa na vita vya mara kwa mara, ambapo kila Mangi alitaka kutwaa eneo la mwenzake ili kuongeza ukubwa wa ardhi na kuimarisha ngome yake kiuchumi.

Hadi Mwanzoni mwa Karne ya 19 , wachaga waligawanyika katika makundi 30 na kila kundi lilikuwa na Mangi wake na walijitegemea mithili ya nchi 30 katika kisiwa kidogo chenye udongo wenye rutuba, hali ya hewa safi na chemchemi za maji kila baada ya hatua chache.

Wachaga walikuwa na bendera yao na siku maalumu ya mapumziko, maarufu kama Siku ya Wachaga, ambapo watu walikutana kwa ajili ya kula na kucheza pamoja ili kuimarisha mshikamano upendo na mshikamano. Makundi hayo yalizungumza lugha tofauti na lahaja tofauti, kulingana na jiografia ya eneo husika.

Watu hao waliwindana kila mmoja akimnyooshea mwenzake kidole kwa uchokozi na tamaa ya kutwaa mali na ardhi ya kundi jingine. Vita vya wachaga viliimarika baada ya kuingia kwa Wamisionari, ambao walifika Kilimanjaro na kueneza dini ya Kikristo pamoja na kuanzisha zao la kahawa.

Hivyo, machifu waliweka silaha chini na kuelekeza nguvu zao kwenye kilimo cha kahawa. Wakoloni walifurahi hali ya utengano miongoni mwa Wachaga hivyo walitumia fursa hiyo kuwalaghai machifu ili waweze kupata ardhi kubwa na rasilimali nyingi. Kila chifu alijitahidi kuwakarimu wageni ili aweze kupata msaada wa kujiimarisha kiuchumi na kisiasa.

Kwa mujibu wa historia ya Wachaga, iliyoandikwa na Stanl Kathleem mwaka 1962, kabila hilo lilikuwa na viongozi wengi, ila wachache walipata umaarufu kutokana na aina ya uongozi wao.

Mwaka 1800 chifu aliyejulikana kama Mangi Horombo kutoka Mashariki mwa mlima Kilimanjaro, alikuwa na nguvu zaidi na aliweza kutwaa maeneo yaliyokuwa na wachaga wasiokuwa na nguvu kiuchumi wala kisiasa.

Hata hivyo baada ya kifo cha Horombo himaya yake iligawanyika na kuunda vikundi vidogo vinavyojitegemea. Wakati Muingereza wa kwanza, Johannes Rebmann, alipofika Kilimanjaro mwaka 1848 alikuta mangi wa Machame na Mangi wa Kilema wakiwa na nguvu kubwa kisiasa na kiuchumi, lakini alififia kutokana na sababu mbalimbali.

Kathleem anasema Mangi Oromba alikuwa kiongozi jasiri katika eneo la Mashariki mwa Mlima Kilimanjaro na aliogopwa na watu wake kwa kuwa alikuwa mtu mwenye msimamo. Kiongozi huyo aliishi eneo ambalo hivi sasa linafahamika kama wilaya ya Rombo. Alikuwa Mangi wa kwanza kuanzisha wazo la kujenga himaya ya Wachaga.

Alijenga ngome yake katika kijiji cha Keni na kuunja jeshi, ambalo lilivamia himaya za machifu wengine na kufanikiwa kuteka eneo la Vunjo hadi mto Nanga. Hata hivyo, baada ya kifo chake himaya yake iligawanyika na kurudi katika vikundi vidogo vidogo kwa kizingatia asili na chimbuko la kila kikundi.

Mangi Sina alikuwa jasiri kama Orombo na aliyongoza himaya ili- yokuwa Magharibi mwa mlima Kilimanjaro hadi mpakani kwenye mto Nanga. Alijenga ngome yake katika eneo la Kibosho, ila alitawala hadi eneo la Marangu na Uru. Mwaka 1870 alijenga mji wa kibiashara kati ya Waafrika na Waarabu, ambapo waarabu walimpa nguo na silaha kisha akatoa pembe za ndovu vitu vingine vya thamani.

Utawala wa Mangi Sina ulififia mwaka 1891 wakati waingereza walipoamua kumuongezea nguvu Mangi Rindi wa Moshi, kisha kumtumia kudidimiza utawala wa Mangi Sina. Mangi Rindi ambaye alijulikana kwa jina la Mandara, alikuwa kiongozi wa Moshi mwaka 1860. Alikuwa miongoni mwa viongozi waliokuwa na ndoto ya kutawala eneo lote la Kilimanjaro.

Ili kufanikisha mikakati yake aliungana na viongozi wa kabila la Arusha eneo la mlima Meru na waswahili kutoka Pwani, kisha kusaini mkataba wa Wajerumani kwa lengo la kuiweka Kilimanjaro chini ya Utawala wa kijerumani katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Mwaka 1891 alifanikiwa kuhifadhi ngome ya kijeshi ya Wajerumani kwa ajili ya kusambaratisha utawala wa Mangi Sina wa Kibosho. Uhusiano wa Mangi Rindi na Wajerumani, uliwezesha Moshi kuwa makao makuu ya mkoa wa Kilimanjaro hadi mwaka 1919 wakati makao ya mji huo yalipohamishiwa eneo la kudumu ulipo mji wa Moshi hivi sasa.

Mangi Marealle wa Marangu alisimikwa na Mangi Sina mwaka 1880 wakati eneo la Marangu lilipokuwa sehemu ya himaya ya Kibosho.

Mangi Marialle wa kwanza alikuwa kijana mwerevu na mwenye shauku ya kuwa kiongozi bora kuliko waliomtangulia Kwa kuwa Mangi Marealle hakuwa mtu wa kutumia mitutu, aliamua kujifunza lugha ya kigeni ili kuweza kuwasiliana moja kwa moja na viongozi wa Kiarabu na wakoloni wa Kiingereza na kuwaalika kuwekeza katika eneo la Marangu.

Pia, alijaribu kujenga urafiki na uongozi wa utawala wa Kijerumani na inadaiwa inadaiwa kuwa 1890 Mangi Marealle alifanikiwa kushawishi uongozi wa jeshi la Kijerumani, kuamini kuwa kuwa watu wa kibosho na Moshi walikuwa na njama ya kuangusha kutawala wa Kijerumani, jambo ambalo lilisababisha machifu wa Kibosho na Moshi kunyongwa na utawala wa Kijerumani.

Himaya ya Watu wa Machame ilijengwa na Mangi Abdiel Shangali, ambaye aliingia madarakani mwaka 1923 na kuongoza mfululizo hadi mwaka 1946 alipopandishwa cheo na kuwa chifu wa jimbo la Hai, kwa kujumuisha eneo la Machame na kibosho.

Mangi Shangali alitawala kipindi cha amani, hivyo alifanikiwa kubadilisha mfumo wa uongozi kutoka utawala wa kichifu wa kuridhishana hadi utawala wa mfumo wa kisasa kwa kuchagua viongozi kwa njia ya demokrasia.

Hata hivyo, wachaga hawakuacha kuzozana kuhusu uhaba wa ardhi na hali hiyo iliendelea hadi Tanganyika ilipopata uhuru na kufunja mfumo wa utawala kitemi na kuunda serikali ya umoja wa Kitaifa. Baada ya Uhuru wachaga waliendelea kukodoleana macho kila kundi likitamani ardhi ya kundi jingine.

Hata hivyo Rais Nyerere alifanikiwa kumaliza tatizo hilo kwa kuwahimiza wachagga watawanyike na kushika ardhi katika maeneo mengine katika ardhi ya Tanzania badala ya kung'an'gania ardhi ndogo katika mteremko wa mlima Kilimanjaro.

Hali hiyo iliwafanya Wachaga kuamua kuwekeza katika elimu ili kuwawezesha watoto wao kujenga uwezo wa kujitegemea na kwenda kutafuta maisha sehemu nyingine. Hali hiyo imewawesha wachagga kutawanyika sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi kujitafutia maisha kwa kushiriki katika nyanja mbalimbali hasa katika uongozi wa mashirika, ualimu na biashara.

Watafiti wa masuala la kisiasa wanasema mfumo wa maisha ya Wachaga, umesababisha watu wa kabila hilo kuwa washabiki wa siasa zenye upinzani kutokana na tabia yao ya kujihami kisiasa.

Ingawa viongozi kadhaa wa juu wa vyama vya upinzani wanatoka mkoa wa Kilimanjaro, inaelezwa kuwa ni vigumu viongozi hao kuunganisha vyama vyao na kuunda chama kimoja chenye nguvu, kutokana na ukweli kuwa hata Machifu wa zama za kale, walishindwa kuungana na kuchagua mtawala mmoja.

NB:Kama ilivyo kwa Watanzania wengine, Wachaga wanapokuwa katika mikoa au nchi tofauti, husahau tofauti zao za nyumbani na kushirikiana kama ndugu wa mama mmoja. Hali hiyo imewezesha wachagga kuishi popote na kushirikiana na watu wa makabila mengine bila kusahau utamaduni wa kwenda kwao angalau mara moja kila mwaka.

Naamini umejifunza kitu kipya ama umeongeze ufahamu kuhusu wachaga

JIFUNZE KUWEKA AKIBA KWA FAIDA YA MAISHA YA MBELENI

Mtu kuweka akiba, ni muhimu sana kama vile ilivyo kwa taifa. Saikolojia ya matumizi ya fedha inaonyesha kuwa mtu hupenda kutumia sasa kuliko kusubiri baadaye ambapo ingeongeza faida na thamani zaidi.

Fedha ni kitu ambacho kipo tu kwa muda kama mtu aliyekuwa nayo sasa akishindwa kuidhibiti leo, kesho hatakuwa nayo. Suala mtambuka hapa ni je, kwa nini niweke akiba au niwekeze kwa jambo lingine?

Ningependa nizungumzie juu ya njia mbalimbali za kuweka akiba ambapo zikitumika zinaweza kukuletea faida kwa karne hii, japo kiuhalisia kwa Waafrika kuweka fedha ni tatizo sugu kwa walio wengi. Hali kama hii inatokana na uwezo mdogo wa kudhibiti fedha kwa mitindo ya kisasa na kibiashara pia. Elimu juu ya jambo hili haijafika au haijakaa vizuri katika upande wa ubongo iliyo wazi kwa mazingira ya hapa nchini.

Zipo njia ambazo ni nzuri zikitumika kwa kuweka akiba kwa faida zitaongeza maendeleo ya wengi. Njia hizo ni:

1», ni kununua fedha za kigeni. Mara nyingi fedha za kigeni mfano Dola za Marekani, Euro, Pound ya Uingereza na fedha kutoka Bara la Asia kama vile za Saudi Arabia, huwa zinapanda thamani ukilinganisha na za Tanzania.

Mfano, ulinunua Dola moja ya Marekani Novemba, mwaka jana kwa Sh1,300. Mwaka huu unaiuza kwa Sh2,100. Ukipiga hesabu umepata faida ya Sh800. Kama ulinunua Dola 10,000, leo hii ikiziuza una faida ya Sh1 milioni, na kadhalika.

Mtindo wa kununua dola kwanza unapunguza kubeba lundo la fedha nyingi, inakuzuia kuitumia bila sababu, hivyo kuendelea kuwa akiba, kukulinda na kukuwezesha uwe na faida pale mfumuko wa bei unapoongezeka na inaweza kukusaidia iwapo itakulazimu usafiri nje ya nchi. Ukisafiri nje ya nchi itakufanya usitumie fedha nyingi za kununua za kigeni kwa gharama kubwa.

2», ni simu benki. Huu ni mfumo ambao upo sana siku hizi eneo la Afrika Mashariki. Siku hizi kampuni za simu zimewezesha mtu kuweka akiba.

Huduma imeboreshwa zaidi kwa kuweza kuzihamishia kwenye akaunti za benki, kulipia huduma na bidhaa au kuzitoa katika nchi nyingine kulingana na aina ya fedha za eneo husika.

Hii inamuwezesha hata kama mtu akiwa mbali na benki na kuwa na uwezo wa kuokoa muda kwa kutumia pesa alizoweka kwenye simu yake kwa kuzitoa kwa wakala aliye karibu naye.

Vilevile, kwa kutumia simu waweza kuvuta fedha kutoka kwenye akaunti yako ya benki na kuziingiza kwenye simu yako na kuwa huru kuzitoa ili kuzitumia eneo lolote kwa kutumia mawakala.

Siku hizi pia kwa kutumia akiba kwenye simu unaweza kupata huduma nyingine kupitia simu hiyo kama vile kununua umeme, kulipia bili ya maji, matibabu, king’amuzi na hata tiketi za kuingia kwenye michezo ya soka au tamasha. Mtu aweza kudunduliza fedha kidogokidogo kwenye simu yake.

3» kuweka akiba kwa kutumia benki na taasisi nyingine za kifedha. Hii husaidia sana kuhamasisha huduma za kuweka akiba kwa malengo kama vile kumsomesha mtoto au amana.

Uwekaji wa fedha za namna hiyo pia huweza kusaidia kuwa na fedha za kukabili dharura na kuwa na mitaji mikubwa ya kibiashara na hatimaye kuleta maendeleo makubwa yaliyokusudiwa.

4», ni kumkopesha mtu na kurudisha kwa riba. Siku hizi aina hii ya ukopeshaji imeenea sana, hasa mijini na vyuoni. Hii imetokana na watu kuzidi kukua sana kiuelewa, wamebadili mwelekeo kutoka kumkopesha mtu pasipo riba hadi kuwa na faida.

Watu wameerevuka na kufahamu kuwa fedha ya mwezi au wiki hii ni tofauti na ya mwezi au wiki lijalo. Tatizo lililopo ni kwamba hakuna maandishi ya kukopeshana kwa walio wengi kwa sababu za kujali utu. Lakini ukweli ni kwamba wanadamu wengi wana tabia ya kubadilika. Kama huna maandishi ya kukopeshana itakuwa vigumu kupata fedha zako pale anapokuwa si mwaminifu.
5», ni kuwekea bima mali zako na biashara yako. Hii ni njia ambayo ni muhimu sana maana hakuna mtu anayeweza kuzuia majanga ambayo ni ya asili au ya kawaida, hivyo bima hasaidia sana siku ukipata ajali ya biashara kwa kuibiwa au kuungua.

6», ni kununua vitu kama nyumba, ardhi na vifaa vya gharama vyenye kudumu muda mrefu. Hivi waweza kuviuza baadaye kwa bei ya juu.

NB.
Maendeleo ya mtu mmojammoja ni mafanikio ya taifa.
Taifa lenye akiba ya kutosha kwa kawaida linakuwa imara na wananchi wenye akiba kwa njia mbalimbali kama nilivyoorodhesha, ni watu wenye maisha ya uhakika. Dharura zote wanaweza kuzikabili na hapa ndipo pia mitaji mikubwa ya biashara inatokea. Kuweka akiba ni jambo la msingi.

ASANTENI

Jumanne, 25 Oktoba 2016

MAMBO YA KUFANYA ILI FIKRA ZAKO ZITUMIKE KUFANIKISHA MAISHA YAKO


MWL: C. MWAKASEGE

AWAMU YA PILI

SOMO:5

MAMBO YA KUFANYA ILI FIKRA ZAKO ZITUMIKE KUFANIKISHA MAISHA YAKO

▶Lengo
Kuweka maarifa ya Kibiblia ndani yako yatakayokuwezesha kutumia FIKRA zako ili ufanikiwe ktk maisha yako

*Mith 23:7(a)*

*HATUA AMBAZO UNAHITAJI KUZIFUATA KAMA UNATAKA KUTUMIA FIKRA ZIKUSOGEZE KIMAISHA*

➡Tumeshaangalia hatua 2 tuko tumeanza seminar. Leo tuendelee na ya 3

3⃣Panga FIKRA zako kwa upya ili zisikupitishe tena mahali pabaya ulipokwisha pitia.

✅FIKRA zinapangika
✅Mfano kwa mama mjane baada ya kusaidiwa na Elisha akitaka hali ile ya mwanzo isijirudie tena lazima abadiri kufikiri kwake la sivyo ile hali atarudi tu

*2Falm 5:7*
Mama mjane alipanga FIKRA zake kwa upya..lazima ujifunze kupanga FIKRA zako kwa upya
Tuonaona mstari wa 7

➡...Nenda kauze mafuta...
Si FIKRA tu kutumika bali MUNGU alitaka Mama mjane ajuaje na akubali ndani yake kuwa MUNGU ndiye amfundishaye kupata faida.

*Isy 48:17*
✅MUNGU hakufunsidhi tu kuhubiri au kuimba bali pia hukufundisha na hupanga FIKRA zako ili zipate kujua MUNGU ndiye akupaye faida

✅FIKRA lazima zipate msaada wa kufundishwa jinsi ya kupata faida

✅Pata tofauti sana kati ya kufundishwa kupata faida na kufundishwa Biashara. Ni sawa na ilivyo tofauti kati ya kufundishwa kufaulu mtihani darasani na kufundishwa juu ya kufaulu mtihani wa kimaisha

✅Maana si kila mtu aliyeko darasani atafaulu maisha, na si kila afanyaye Biashara atapata faida..lazima ujifunze kuvuka hapa

*MAENEO MUHIMU YA KUTAKIWA KUBADILIKA*

*1).* Weka FIKRA zako zikubali MUNGU ndiye anayekufundisha kupata faida

▶Watu wengi wakikwama kiroho hukimbilia kanisani ila uchumi wao ukikwama huwaoni kanisani hukimbilia Benki, sasa sisemi Benki ni mbaya au usiende Benki ila wanasahau kuwa

▶ROHO MTAKATIFU ni mwalimu mzuri sana wa kukufundisha ujasiriamali wenye kupata faida

*2).* Lipa Deni
✅Elisha alimwambia Mama mjane ....kauze kisha lipa deni....

✅Alikuwa anatafuta kitu gani?
▶Alikuwa anapandikiza nidhamu za kutumia fedha ambazo MUNGU amempa kwa sababu zake alizokupa au ulizomwomba tena kwa mwongozo wake!

▶Mama mjane alikwenda kutaka msaada wa watoto wake kutokuchukuliwa watumwa(Alitaka kupata fedha za kuwakomboa watoto wake)

▶Hakuwa na FIKRA zilizojengeka kulipa deni maana Biblia haituonyeshi aliwahi kukopa. Kama huna FIKRA za kukopa huwezi ukawa na (nidhamu) FIKRA za kulipa deni.

*Mama mjane alikabidhiwa matumizi ya fedha ktk maeneo haya*
⚫Kulipa deni
⚫Gharama za kwake na zile za baadaye
⚫Gharama za watoto na za wakati ule wa baadaye
⚫Kuhakikisha ya kwamba hamalizi faida lazima abaki na mtaji.

✳Je unamwomba MUNGU pesa kwa ajili ya nini au kwa ajili gani?
▶Kumbuka pesa huyumbisha mawazo na kujikuta watumia nje ya lile kusudio

▶Ukikorofisha hapo MUNGU hukaa pembeni. FIKRA zinahitaji nidhamu kwenye matumizi ya pesa. Kama MUNGU anakupa kwa ajili ya kitu fulani hakikisha unaielekezea hyo pesa kwenye hicho kitu.

▶Tofauti na hapo utaona ROHO MTAKATIFU anakuhimiza TOBA

*Mith 13:22*
▶Watu wengi wana FIKRA za kujitazama wenyewe tu kwenye upande wa pesa wanajikuta kusahau kuwa wana familia na watoto!

▶Biblia inatuhimiza kuweka akiba mpaka za wajukuu!

▶Usitazame kukwama kwa mme/mke wako ama wazazi wako, usifike mahali hata pa kuwakasirikia badili FIKRA zako ili wewe uvuke hapo kisha mrushie kamba naye atoke hapo oooh hallelujah Hallelujah

*HOME WORK*
➡Orodhesha madeni yako

*Zab 37:21*
✳Umuhimu wa kuorodhesha madeni

▶Usipolipa mikopo MUNGU haji kukupigania katika haki zako.
▶Unapoteza haki katika haki
▶Mikopo isiyolipwa ugeuka deni
▶Deni ubeba vitu (rehani) ili akili zako ziamke. Na baada ya kutaka kuja kuvichukua ndipo akili zako zitaamka
▶Si kila ambaye anashindwa kulipa deni hana hela bali hana mpangilio mzuri wa matumizi na ulipaji

*Yer 22:21*
✅Si kwamba hapendi kusikia bali hataki kusikia maana yake hataki kutekeleza alichoambiwa

✅Gharama kubwa ya kutokufaulu mipango yako ni kupoteza utulivu wa MUNGU kukusemesha

✅Wengi wakisha kopa kwenye kulipa hulipa nusu na nusu wanaweka mfukoni wanasahau MUNGU ndiye aliwafundisha kupata faida na au walipewa kibali cha kupata mkopo

✅Usije ukasahau na kusema huu utajiri ni nguvu zangu wakati ni MUNGU ndiye aliyekupa nguvu za kupata utajiri

*UNAFIKIRI KWANINI MUNGU ALILETA SADAKA*
▶Si kwamba ana shida na pesa yako
▶Lengo la kwanza lilikuwa kutumia sadaka kukutengenezea FIKRA sahihi ndani yako
✳Tazama maana ya
⚫Malimbuko=MUNGU anataka umfikirie yeye kwanza
⚫Zaka ya kwanza=MUNGU anataka kupewa heshima ktk maisha yako

✅Watu wengi kwenye kipindi kigumu na chenye kibano wako tayari kutafuta hela kulipa Benki lakini si kwa MUNGU. Kwa MUNGU excuses zitakuwa nyingi sana na hata kusema "MUNGU we si unajua nilivyobanwa"

✅MUNGU hana maana wala hataki kukufirisi bali anataka kukutengenezea FIKRA zenye Nidhamu

✅Jifunze kumpa MUNGU 100% naye anakurudishia 100%

✅Muulize MUNGU kwanza kwenye kila kitu, ratiba zako, muda wako na mambo yako mkabidhi na mfikirie MUNGU kwanza

✅Usitamani kuiga maisha na FIKRA za mtu mwingine hakikisha MUNGU anakupa mbinu za kujenga FIKRA za kwako mwenyewe.

✅FIKRA zenye kujenga nidhamu ndani yako.zitakufanya utende haki wala hazitakupeleka kwenye kupokea rushwa

✅FIKRA hizi zitakuwekea unyenyekevu ndani yako, kujishusha na kujifunza kutoka kwa wengine

✅Usijaribu ku copy na ku paste kutoka kwa mtu mwingine BWANA atakupa mikakati sahihi ndani yako

*MAOMBI*

*..."Jesus Up"...*

*****SIKU YA TANO*****

SOMO:6

NAMNA YA KUFANYA ILI FIKRA ZAKO ZITUMIKE KUFANIKISHA MAISHA YAKO

▶Lengo
Kuweka maarifa ya Kiblia ndani yako yatakayokuwezesha kutumia FIKRA zako ili ufanikiwe ktk maisha yako.

*Mith 23:7(a)*

▶Tunaendelea na *HATUA....*

4⃣Omba MUNGU akusaidie uweze kupata kutoka kwenye vitabu maarifa yanayohitajika ili uhitajike

*Dan 12:4*
✅Tutazame hatua kwa hatua ktk mtirirko ufuatao:-

*1).* Ni vyepesi mtu kuhitajika akiwa na maarifa yanayohitajika ktk kipindi husika

*Dan 1:17-21*
➡Watu hawakuajiri sababu ya Cheti bali ujajiri maarifa uliyonayo

➡Wakikuajiri sababu ya Cheti na kukaa nawe muda wakagundua una Elimu lakini huna maarifa utashushwa cheo

➡Hatuambiwi kina Daniel walikuwa wangapi, ila walisomeshwa na kupimwa ktk mtihani. Kuanza kwako chuo walikuwa tayari na mtaji..swali la kujiuliza kile walichosomea kiliwasaidia kupata maarifa?

*Dan 1:3-4*
➡Walikuwa na Elimu pamoja na maarifa kwa kiwango fulani.

➡Ilibidi wakae darasani miaka 3 wapate maarifa juu ya maarifa. Haijalishi Elimu na maarifa waliyokuwa nayo awali.

*Mwz 41:37-40*
➡Yusufu alipewa nafasi ya Uwaziri Mkuu akiwa jera baada ya kugundua kuwa ana maarifa

➡Haijalishi uko wapi, jera? Umefunikwa? Umefungiwa au wapi lakini ROHO MTAKATIFU ni mwaminifu atakukutanisha tu na kusudi kama una maarifa yanayohitajika

➡Usiende shule au usisome kwa ajili ya kupata.Cheti bali soma ili upate maarifa. Maarifa yatakusaidia kutoka maishani ila si cheti

*2).* Kuna Vitabu vilivyobeba maarifa yanayotakiwa kwa muda husika

*Dan 12:4*
➡Muda ndiyo unaodai aina ya maarifa

➡MUNGU aliumba kwanza nyakati(muda) kisha mtu

*Mwz 1:1*
➡NENO mwanzo=aliumba muda kwanza kisha mbingu na nchi

➡Muda na maarifa zinaenda pamoja

➡Daniel aliambiwa yatie muhuri= Mtu yeyote akisoma asipate maarifa yaliyomo ndani yake kwa sasa mpaka kwa muda ulioamriwa. Hata yeye kwa kipindi kile asingeelewa hata kama angesoma

*Dan 1:4*
➡Mfalme aliagiza wafundishwe Elimu ya wakaldayo maana yake walikuwa tayari na kiwango fulani cha uelewa.

➡Ni sawa na kuchukua mtoto wa darasa la kwanza kumpeleka Chuo Kikuu haiwezekani maana kuna ngazi tofauti tofauti maana *Umri uenda na aina fulani ya kufikiri*

➡Ni hatari sana kusoma na kuwa na Elimu halafu huna lugha ya kutafsiri maarifa hayo(Wasoma kiswahili halafu interview kichina)

➡Kumbuka lugha inakunyima kazi

➡Njia yako uendana na lugha vilevile yaani kuchukua maarifa Ujerumani siri imefichwa kwenye kitabu hicho cha lugha ya kijerumani. Lazima usome mwaka mzima kijerumani kwanza kuweza kutoa maarifa yaliyoko humo.

*Ayb 35:16*, *34:35*
➡Kuna maneno hayana maarifa.
➡Si kila kitabu chenye maarifa chaweza kukusaidia isipokuwa kwa wakati sahihi na muda ulioamriwa!

*3).* Vitabu vilivyobeba maarifa uwa vingine vinafungwa visitoe maarifa hadi muda/wakati wa kuhitajika kutoa maarifa au muda umekaribia au umewadia

*Dan 12:4*
*Dan 9:1-3*
➡Kitabu chochote chenye sababu hii ya (3) lazima ukishakisoma utapata msukumo wa kuyaweka kwenye matendo yale yote uliyoyasoma

➡Nunua Vitabu Chini ya msaada wa ROHO MTAKATIFU, mwombe MUNGU akupe hekima kununua vitabu ambavyo.vina maarifa unayoyahitaji. Hii ni nidhamu unahitaji kujiwekea

➡Kumbuka kitabu chichote kilicho na maarifa ya wakati huo na sahihi kinakupelekea kupata msukumo ndani yako kuweka kwenye matendo hayo uliyosoma na kupata msukumo wa kuyaombea.

*4).* Ni muhimu kwa kitabu kufunguliwa na akili ya msomaji kufunguliwa kwa pamoja ili maarifa yaliyomo ndani ya kitabu yawe msaada ktk muda husika kwa ajili ya msomaji huyo

*Luk 24:44-49*
➡Kitabu kilikuwa kimefunguliwa lakini akili zao zilikuwa zimefungwa

➡Kitabu kilifunguliwa kwa ajili yao na YESU alijua akisema nao waweze kuoanisha kutoka kwenye vitabu vya torati na zaburi ndiyo maana akili zao zilifunguliwa na kufunuliwa wapate kuelewa walichokisema manabii waliotangulia kinatimia sasa

*5).* Mwombe MUNGU akukutanishe na Vitabu vilivyobeba maarifa unayoyahitaji na avifungue kama bado vimefungwa ili upate maarifa unayostahili kama hayo

*Uf 5:1-5*, *10:1-11*
➡Simba wa Yuda (YESU) alipata nafasi ya kukifungua kitabu.

➡Kitabu kinaweza kikawa kimefungwa ukaomba kifunguliwe

➡Pia kinaweza kikawa kimefunguliwa, sasa omba maarifa ukifunguliwa akili uweze kukielewa

➡Tazama Biblia ni kitabu bora na ni ileile inabeba maarifa ya kukusaidia bila kujali muda uliowekwa maana muda ukifika unafunguliwa tu

➡Jiulize ni kwanini watu wengi wanasoma shule lakini si wabunifu? Mfano waliosoma Administration waambie waanzishe ofisi binafsi uone..wanasubiri ku copy na ku paste ila leo MUNGU anakutafuta kukupa maarifa ukagunguliwe akili...oooh hallelujah!

*MAOMBI*
Orodhesha madeni yako maombi yataendelea siku ya 7(leo)

✅Maelfu ya watu walimpokea YESU pia

*..."Jesus Up"...*

*****SIKU YA SITA*****

SOMO:7

NAMNA YA KUFANYA ILI FIKRA ZAKO ZITUMIKE KUFANIKISHA MAISHA YAKO

▶Lengo
Kuweka ndani yako maarifa ya Kiblia yatakayokuwezesha kutumia fikra zako ili ufanikiwe ktk maisha yako

*Mith 23:7(a)*

*Summary*
✅Kubadili maisha yako badili kufikiri kwako
✅Maana ya fikra...rejea day 1
✅Hatua ambazo unahitaji kuzifuata kama unataka kutumia fikra zikusogeze kimaisha..rejea day 1-6
✅Jana tuliangalia mtiririko wa mambo kama 5 hivi, lile la 5 tuliangalia; uhusiano kati ya maneno na Vitabu maana kitabu kimebeba maneno, muda na maarifa *Dan 12:4*
✅Maarifa ndani vitabu uachiliawa kufuata na uhitajika wake kipindi husika
✅Wazo la vitabu lilianzia rohoni si mwilini

..Tuendele na mtiririko huo..

*6).* Zijue njia za kupata maarifa kutoka ndani ya maneno yaliyomo ndani ya kitabu

*Josh 1:8-9*
▶Maneno ya MUNGU alizungumza na Joshua baada ya Musa kufa

▶Alikuwa akimtia moyo kuendelea mbele na watu wake ili kusudi litimie.

▶Joshua alitazama kazi aliyopewa na kuangalia kufanikiwa pamoja na kustawi kwake pamoja na watu wake hakika kwake halikuwa jukumu jepesi ndiyo maana alipewa njia ya kunsaidia...mstari wa 8

▶Aliambiwa chukua kitabu maana humo ndiko kuna maarifa ya kushinda kwako.

▶Maana miaka 400 walikaa bila kuwa na utaratibu wa KIMUNGU, MUNGU baada ya kukumbuka Agano alilofanya na Ibrahim na Yacobo akawatoa utumwani, walipofika Sinai akatengeneza utaratibu ambao utafananafanana na yeye ili kukaa nao. Lilikuwa jambo jipya sana kwako

▶MUNGU akija na kuamua kukaa mazingira take ubadilika kabisa ndo maana akatengeneza kitabu na ndani yake kuna maarifa, kuna masuala ya ujenzi, kilimo, uchumi, mahusiano ya kila aina, kitabu kukusaidia kustawi sana na uweze kuishi pamoja naye

*JOSHUA ALIAMBIWA VITU 3 VYA MUHIMU ILI UWEZE KUTOA MAARIFA NDANI YA KITABU, NA NI KITABU CHOCHOTE KILE*

1⃣Kisiondoke kinywani mwako
✅Jifunze kufikiri kila ambacho unakiona na kukisoma ndani ya kitabu na kutaka kitokee kwako

✅Jifunze kusema kila unachokiamini ndani ya kitabu *Mark 11:23*

✅Yale uliyonayo utegemea sana kile unachosoma na kukisema

*Rum 10:8-10*
✅Ukitaka kupata kilichopo kwenye kitabu lazima ukiri. Ukikuta mtu anapinga kilichopo ndani ya kitabu jua hakitatokea kwake

*Zab 45:1*
✅Ulimi unaandika
✅Kuzungumza ni kuandika kwenye mioyo na vibao vya nyama kwako.

✅Ndiyo maana ni rahisi tukikutazama tukajua nani kaandika ndani yako

✅Unaposema unaandika kwenye nafsi yako
✅Haitoshi kusoma jifunze kusema maana uanzia kuandikwa ndani. Maana sauti ninayoisikia kuongea si sauti ninayoisikia kuongea

2⃣Yatafakari maneno take mchana na usiku
✅Ni zaidi ya kusoma, kukariri
✅Tamka kutoka moyoni. (Meditation)

✅Tafakari=Tafuna
✅Kukariri=Kumeza na hii so guarantee zitafanya kazi

✅Huwezi ukatoa maarifa ndani ya kitabu bila kutafakari= fikra na akili zako kuchanganya ili utakapotembea utakuwa neno linatembea. Maana NENO alifanyika mwili akaa kwetu

✅Kutafakari NENO kuna kupa nafasi ya kutafuna na kupata nafasi ya kuwa na maswali mengi sana utakuwa mtu wa kutembea na note book na kalamu Mara nyingi si Ku copy na kupaste bali utapata maarifa zaidi

3⃣Upate kuangalia na kutenda sawasawa na maneno yaliyoandikwa humo
✅Utendaji unahitaji nidhamu ya kiwango cha juu sana

✅MUNGU anapoachilia wazo la biashara ndani yako usiwe na haraka kushirikisha watu maana kufanya hivyo kesho utamkuta mwenzako katekeleza..unahitaji nidhamu ktk hili

✅Swala si wazo au utekelezaji bali anahitaji kukuweka utaratibu wenye nidhamu kwanza

*Muh 12:9*
Tuongezee jambo jingine
4⃣Tafuta waalimu ambao wanakufundisha upate maarifa si wale watakaokufundisha upate darasa=cheti

✅Hata ktk vyuo vya kuandaa walimu lazima waandaliwe kutoa maarifa ndani ya Vitabu na si tu wawafundishe wanafunzi kunaliza shule

✅Binafsi nitamsikiliza na kumfuatilia mwalimu yule kesho na kesho kutwa kila nikimsikiliza nitapata maarifa=lugha ya mjini ninamwelewa sana

✅Paul alipokuwa na kiu ya kumtumikia MUNGU alipata waalimu walikuwa wanatoa maarifa ya Dini si maarifa ya KRISTO

✅Jiulize kwanza waalimu gani wanakufundisha? Unapeleka watoto shule jiulize ina walimu wa namna gani

*7).* Uwe mwangalifu na Vitabu unavyosoma

✅Si kila Vitabu vina uwezo wa kutoa maarifa
✅Kuna vingine haviendani na njozi yako. Hivyo usipoteze muda mwingi kusoma visivyo vya kwako maana muda hautoshi na huna muda wote ukifikiri ni wa kusoma

*Muh 12:12*
✅Vutabu ukisoma vinakuchosha
✅Usijaribukushindana na watunzi wa Vitabu ktk kusoma maana utakufa na wataendelea kutunga tu

✅Pia kuwa mawangalifu sana na Vitabu vya hadithi maana hutoa maarifa ndani ya mtu na pia utoa maarifa kwa njia ya hadithi *1Tim 1:3-4*

*Matendo 19:19*
✅Vilichomwa Vitabu hivyo maana maarifa yake yalikuwa hayatakiwi

✅Kama Vitabu vimepitwa na wakati wasomaji wakisoma fikra zao urudishwa nyuma ila vipo vile Vya zamani ambavyo maarifa yake ni ya mbele

*8).* Jizoeze kwa maombi kunyunyizia DAMU YA YESU juu ya kitabu unachosoma

*Ebr 9:19-22*
✅Maana si kila kitu unachosema kitakuzalishia jambo ulitakalo

*Ayb 38:2*
✅Maneno yasiyokuwa na maarifa uachilia giza

✅Mfano angalia ukitaka kusoma Biblia sekunde chake umechoka, umelala, uelewi lakini tazama ukitaka kusoma msg kwenye Simu au gazeti, waweza soma msg zote na magroup yote bila kuchoka na kuwa active zaidi

✅Ukigundua hili unajua ni vita na DAWA YAKE NI DAMU YA YESU PEKEE

✅Kabla ya kusoma achilia DAMU ya YESU kuondoa Giza na kufunga fikra usielewe

✅Jifunze kuombea miguu ya waalimu
✅Jifunze kuombea eneo unalopatia elimu. Mussa aliambiwa vua viatu

✅Kuna uhusiano mkubwa kati ya miguu na sikio na kichwa pia

✅Hatua unazokanyaga na jinsi unavyofikiri kuna uhusiano mkubwa sana

✅Miguu lazima ifungwe utayari maana waweza pata maarifa halafu ukapata uzito kutekeleza.

✅Shetani akiweza kukubana kwenye miguu yako na masikio yako huwezi kufanikiwa hata kidogo.

✅Jiulize Mara ya mwisho kusoma Biblia tena unayo kwenye Simu yako ni lini? Ila Mara ya mwisho kusoma msgs ndani ya Simu ni lini?

*MAOMBI*
✳Masikio yako vs Simu yako

*..."Jesus Up"...*

*****SIKU YA SABA*****

SOMO 8

NAMNA YA KUFANYA ILI FIKRA ZAKO ZIFANIKISHE MAISHA YAKO*

Tumekuwa na semina nzuri sana na kama ni siku yako ya kwanza tafuta kanda.  Na somo hili hapa ndio nilikuwa naanza tu kwenda ndani kwa hiyo omba kwa Mungu ili atupe tena nafasi nyingine maana somo bado linaendelea.Pia ombea na kamati maana muda wetu wa kufanya semina hapa Dar es Salaam ni kipindi cha mvua hasa ile semina ya Kwanza kwa hiyo omba tupate muda mwingine au kiwanja kingine.

Tumesoma neno kutoka Mithali 23:7a   Maana aonavyo mtu nafsini mwake. Na tumeangalia tafsiri mbali mbali, moja inasema atafsirivyo, na nyingine imesema anavyotafakari . na pia ukisoma Zaidi ndipo utajua na tafsiri zingine nyingi. 

Na nilikuambia kuwa  *Fikra ni mkusanyiko au mtirirko wa mawazo yanayotengeneza msimamo wa kiutekelezaji ndani ya mtu* na Fikra zina tafsiri mbali mbali. Kwenye siasa/ Uchumi tunaweza sema ni *sera* na kwenye makabila tunaweza sema ni mila.

*Hatua ya Tano*.  *```Jizoeze kijiuliza maswali yanayofanya Fikra zako zifikiri kiubunifu```*

*1* *Jifunze kufikiri juu ya soko kwanza kabla kitu unachofikiri kuuza*

Tafuta soko kwanza hata kama, yaani demand ya kitu chako kwa sababu biblia inasema *anatanga mwisho tangu mwanzo*. Start with end in mind. Usianze kulima shamba lako kama hujui unalima kwa ajili ya nini yaani unalima kwa ajili ya chakula au kwa ajili ya biashara. Na kama hujajibu swali hili kuwa unalima kwa ajili ya nini ujue tayari umefeli.

*MFANO* Kuna wakati nilitaka kulima maparachichi kwenye shamba ambalo baba alituachia urithi. Na nilitafuta watu wanaotaka tulime kwa mkataba yaani tukivuna wao ndio wananunua  na alikuwepo mzungu mmoja ananunua hayo maparachichi. Nilitafuta mawasiano yake nikayapata na  nikaongea nae ila sikupata majibu sahihi kwa hiyo nikaamua kumfuata kule kule aliko.  Na Nilikuwa na maswali ambayo nataka kujua kwa sababu ukilima maparachichi baada ya miaka miwili unavuna na uzalishaji wa mti ulioupanda unaanza kupungua mwaka wa sita. Yaani baada ya miaka sita uzalishaji unashuka.  Na kuanza hicho kilimo ilikuwa inahitaji hela nyingi kidogo, ili kuwekeza. Na kwa kuwa kuuza kutaanza baada ya mwaka wa tatu kwa hiyo nikamuuliza baada ya mwaka wa tatu (yaani tokea ukipanda itakuwa imepita miaka 3 hadi unaanza kuvuna)  bei yake itakuwa sh ngapi? Akasema hajui sasa nikamauuliza tena je wewe utakuwa unauza wapi? Akasema Uingereza, sasa nikamauuliza kama wewe utakuwa unauza uingereza basi ni kuwa lazima umepiga hesabu za bei na ndio maana umekuza kuwekeza huku kununua maparachchi.

Na hakupenda sana maswali yangu maana hakutegemea kama kuna mtu atamuuliza maswali kama yale kwa sababu walikuwepo wengine wanalima tu kwa kuwa wamesikia mzungu ananunua. Na mimi nilimwambia kuwa *nahitaji kupiga mahesabu* kwa sababu hata kama nataka nikakope benki lazima wajue kuwa je huu mradi ninaoutaka kufanya je utakuwa na faida? Na je utaweza kuerejesha mkopo wao na je mimi mwenyewe ntapata faida?

Mradi wowote hata kama unaweka pesa za kwako jaribu kupiga mahesabu na jaribu kuwauliza na watu wa benki kama wanaweza toa mkopo kwenye aina hiyo ya mradi? Kwa sababu benki huwa wanaangalia kama huo mradi unaweza rudisha hizo hela zao unazotaka kukopa.  Na ukiona benki wanakaa basi ujue kuwa mahali hapo ni hatari kuwekeza kwa lugha ya kitalaamu tunaita *risk*  na hata kama unalipa vipi uwe makini nao sana au acha usiweke hela yako hapo maana inaweza ipotee.

Kwa hiyo nikaenda kuwauliza Wafanyakazi wake na wao pia waliweza kujibu kwa sehemu basi, nikaa chini nikapiga mahesabu na nikagundua baada ya mwaka ya 5 ndio naweza pata faida ya laki 7 (700,000) yaani hiyo ndiyo faida na wakati uwekezaji wake umenigharimu mamilioni ya pesa. Kwa hiyo nikamwambia yule mzungu kuwa siwezi kulima kwa sababu kama nalima kwa ajili ya biashara nahitaji faida na kama maparachichi ya kula ntanunua sokoni.  Kwa hiyo *Fikiri kwanza soko kwa sababu ile chupa ya mafuta ingekuwa haina thamani kama hamna soko*

*2* *Zizoeze fikra zako kufikiri kiubunifu*

Fikra za aina hiyo ndizo zinaoleta viwanda, kwa sababu viwanda vinakuja kwa njia ya ubunifu.  Na kasome uingereza , Ujerumani na Afrika ya Kusini.  Utajua hiki nianchokummbia,

*3*  *Tafuta kujua mahitaji ya muda*

Biblia siku  ilitoa kabisa mwongozo kuwa maarifa siku za mwisho yatakuwa mengi sana na yatenda kwa spidi sana. Kwa hiyo ukijua mahitaji muda husika iatkusaidia sana, Kwa mfano, Mwanvuli ni kwa ajili ya kipindi cha mvua na ukitumika kipindi cha kiangazi utatumika kwa kazi zingine kabisa.

Tulikuwa na mkutano mmoja huko marekani na moyor wa lile jiji alitangaza kuwa kutakuwa na barafu *Storm* na hali ya hewa ingebadilika sana na nikawa natazama kwenye television wakawa wanatabiri kuwa hata safari za ndege zataahirishwa na hata wanafunzi walitangaziwa kuwa hakuna kwenda shule kwa sababu ya barafu itakayoshuka.   Na sisi ilikuwa inatakiwa tuondoke siku hiyo. Basi nikaingia kwenye maombi kama masaa mawili hivi ili kusemesha mbingu za mahali pale ili kuzuia hiyo barafu na niweze kuondoka na ndege yetu pia iweze kuwepo yaani *flight isiwe cancelled* yaani iahirishwe. 

Walifanya kila maandalizi na magari yaliliyokuwa na chumvi tayari kwa ajili ya kuyeyusha barafu huko barabarani na pia hata magari ya kwenda airport  ilikuwa ni tabu sana kwa sababu walishatangaziwa kuwa watu wabaki nyumbani kwao . Basi tulifanikiwa kutoka na tukaenda airport na tuliikuta ndege yetu ipo na safari za ndege zingine ziliahirishwa.

Na tulikopokuwa tunatazama television tena na zile saa walizotabiri kutokea kwa hizo storm  hazikutokea na walishindwa kutoa sababu, na tuliwaambia watu wawili tu wa ule mji. Na baada ya sisi kuaondoka ilishuka storm kubwa sana.  Hawakujua kuwa ni sisi ndio tulibadilisha hali ya hewa ya mahali pale.

Na tulipoondoka rafiki yetu mmoja alituambia kuwa ile chumvi yote imeharibika kwa sababu chumvi iliandaliwa kwa masaa  na haikuandaliwa kwa ajili ya chakula. Na ndio maana iliharibika . ndio  maana nakuambia kuwa *zizoeze fikra zako kufikiria mahitaji ya muda*

*1* *Ukisikia malalamiko popote   usizizoeze fikra zako kulalamika, Bali fikra zako zijue kujibu juu ya
~~ *nani analalamika*
~~ *Kwanini analalamika*
~~ *Anamlalamikia nani*
~~ * Muda gani analalamika*
~~ *Malalamiko yake huwa yanajirudia kipindi gani*

>>Hata kama ni halali kiasi gani, wakati wenzio wanalalamika chukua fikra zako kufanya utafiti  na ujue ni akina nani wanalalamika, kwanini, lini na wanamlalamikia nani.
*MFANO*  Hesabu 13-14
Habari za wapelelezi, ambao walitumwa kwenda kuipeleleza nchi ya Kanani na walitumwa kwa sababu za kiuchumi kabisa kwa sababu hawakutumwa habari za kiroho kujua wale watu wanasali wapi au la.
*SABABU WALIZOTUMWA*
>>  _Hesabu 13:17-20  17 Musa akawapeleka ili waipeleleze nchi ya Kanaani, akawaambia, Pandeni sasa katika Negebu mkapande milimani,

18mkaitazame nchi ni ya namna gani; na watu wanaokaa ndani yake, kwamba ni hodari au dhaifu, kwamba ni wachache au wengi;

19na nchi wanayoikaa kwamba ni njema au mbaya; kwamba wanakaa katika matuo au katika ngome;

20nayo nchi ni ya namna gani, kwamba ni nchi ya unono au ya njaa, kwamba ina msitu au sivyo. Iweni na moyo mkuu, mkayalete matunda ya nchi. Basi wakati ule ulikuwa wakati wa kuiva zabibu za kwanza.

Angali pia na katika iingereza (NIV) hii mistari
*Numbers 13:17-20 17When Moses sent them to explore Canaan, he said, “Go up through the Negev and on intothe hill country. 18See what the land is like and whether the people who live there are strong orweak, few or many. 19What kind of land do theylive in? Is it good or bad? What kind of towns dothey live in? Are they unwalled or fortified? 20 How is the soil? Is it fertile or poor? Are theretrees in it or not? Do your best to bring back someof the fruit of the land.” (It was the season for thefirst ripe grapes.)* 

Hawa wapelelezi walitumwa kwa masuala ya kiuchumi kabisa  na walitumia siku 40 kufanya utafiti na aliwaambia waliete na matunda ya zabibu ili wasije na cooked data yaani wangeweza wasiende maana wangefanya utafiti wa kuitungia. Kazi ya utafiti ni kuwasaidia watu kuweza kufikiri. 

Angalia  Majibu ya Utafiti wao mstari 33 *Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi*.  Soma sura zote mbili ndiponutaelewa vizuri. 

Fikra zao zilishindwa kutafsiri kile kitu ambacho Mungu alitaka waone. Na Mungu alisema hawa watu nitachukuliana nao hadi lini?

*VITU VYA KUJIFUNZA KATIKA HABARI HII*
a). Mungu alikuwa anataka kuwaonesha tatizo ina maana alikuwa anawaandaa kifikra ili waweze kutafsiri na kujua namna ya kutatua tatizo maana kutatua tatizo ndio chakula chao.
*Mithali 3:5-6  Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako*

Fikra zako inabidi zikae mkao wa kutafuta suluhu ya tatizo, na akili zako zikifanya kazi na Mungu ujue kuwa lazima utafanikiwa.

b). Mungu aliijua Kanani vizuri sana, kwa sababu aliwaambia kuwa  ni nchi ya maziwa na asali. Na hawakujua kuwa maziwa na asali ni processed  products

*2* * Kulalamika ni ishara ya kuwa fikra zako hajioni jibu bali zinaona kikwazo*

*3* *Fikra ziliumbwa ziweze  kutafsiri changamoto ili ziwe fursa*

Ukisoma 2 Wakorintho 4:3-4 utona habari za kuwa ibilisi hupofusha fikra za watu . maana Mungu alipoumba changamoto au matatizo ni ili watu waweze kula.  Kwa sababu ukisoma biblia mwadamu aliumbwa na hamna mahali alipewa kitanda cha kulala. Maisha ya Mwanadamu 1/3 ni anatakiwa kulala. Sasa inatetegemea yeye mwenyewe atalala wapi kama kwenye majani, au kwenye ngozi au kama kitanda kizuri au ni banko. Ni wewe mwenyewe, kwenye biblia huwezi kuta kuna mahali Mungu alisema pawe kitanda.  Sasa ni jukumu lako kutengeneza kitanda. Sasa unapohitaji muujiza wa kitanda fikiri kwanza.

Katika biblia huwezi kuta kuna neno maendeleo, nilitafuta kwenye concordance (itifaki ya biblia) ni kitabu chenye kuonesha maneno yaliyomo kwenye biblia.  Sasa katika biblia neno maendeleo limefichwa kwenye neno *nuru* maana yake aliposema kuwe Nuru ina maana kuwe na maendeleo.

*4* *Ile kwamba mtu amekutangulia haina maana kuwa anafikiri vizuri kuliko wewe*  

Wana wa Israel walipokuwa jangwani, na wenzao waliotumwa kwenda kanani kupeleleza nchi ina maana ilitakiwa waweze  kufikiria mbele kuliko  wenzao.  Lakini Fikra zao zilikwama na wao waliishia jangwani. Na katikati ya Jangwani na Kanani kulikuwa na Fikra, japo imani walikuwa nayo ila fikra zao ziliwakwamisha na waliishia pale. Ila watoto wao ndio alienda kwenye nchi ya Kanani. Kwa hiyo angalia kinachokutoka katika kinywa chako.

Ukifikiri kama ni watu wanaokaa jangwani na wewe utabaki jangwani maana unaweza kwama hapa walipokwamia.  Kwa hiyo mtu anaweza akawa mkubwa lakini fikra zake bado ni ndogo.

*5* *Palipo na Malalamiko hapo ni fursa ya chakula fanya utafiti wa kulalamika kwako 
~~ *nani analalamika*
~~ *Kwanini analalamika*
~~ *Anamlalamikia nani*
~~ * Muda gani analalamika*
~~ *Malalamiko yake huwa yanajirudia kipindi gani*

Ukiona watu wanalalamika, basi wewe zifanye fikra zako ziweze kufikiri na fanya utafiti maana kuna chakula hapo.  Na hii ndiyo iliyotoa fursa kwa akina Kalebu na Joshua. Maana Mungu alipowaonesha matatizo wao walitafsiri kwa matatizo kama Fursa,

Kule kulalamika kwa wana wa Israel, kulisababisha wao kutokwenda Kanani ila watu wawili tu. Sasa piga hesabu watu waliotoka Misri walikuwa ni zaid ya million 2 lakini walioingia Kanani ni Wawili tu. Na hawa  ni watu walioweza kutafsiri na fikra zao zilifikiri tofauti na wengine.

Hata huko mbinguni naamini huwa wanacheka sana maana kuna wengine wanaona kuna majitu Mungu tunaomba kuyaondoa na wengine wanaona chakula.

*MFANO WA 2* *Hesabu 11:11-15* 
Hapa tunaona habari za Musa kuwa alianza kulalamika na alipokuwa anamlalamikia Mungu na katika kulalamika kwake kulitengeneza ajira ya watu 70.  Na ukiona kiongozi analalamika kuwa kazi zake zimemzidi basi anza kukaa mkao mzuri maana kutakuwa na kazi hapo.  Na wewe ukiungana na kulalamika kwake basi wakati anatangaza kazi zingine atakuacha kwa sababu wewe ni mlalamishi.

*MFANO WA 3* *Habakuki 1-2*
Sura ya kwanza tunaona Habakuki akilalamika kutokana na kutokuwepo haki. Na baada ya kulalamika Mungu alijibu kulalamika kwake.  Na alimjibu kuwa kwa njozi na njozi inamfanya aweze kufikiri.  Kwa sababu ukipewa njozi bila matatizo  inakuwa haina maana. *Vision must have problem to solve or must have value*
Na kama akili yako inaweza kusolve  matatizo ya watu basi ujue kuwa kuwa utakuwa demanded . na ndivyo ilivyotunavyouza kahawa ambayo bado iko katika hali ya kuwa ghafi. Na ukiweza kufikiri ina maana unaweza kubuni kiwanda cha kuweza kuprocess .
Fikra zako ili ziweze kufanya kazi Zaidi inatakiwa unapokuwa unaomba kwa Mungu unganisha na matatizo yaliyopo kwenye jamii yako na omba Mungu akuwezeshe kukusaidia kujibu hayo matatizo na ukienda na kanuni hii basi ujue utapata business idea,. Thamani ya Mwalimu ni uhitaji wa Kiroho wa wanafunzi. 

*Ombea Fikra zako mara kwa Mara ili Mungu aweze kuzifungua.  Na hapa ni mwanzo omba Mungu ataoe tena kibali cha somo hili ili tuweze kuendelea. Homework Tafuta mahali penye malalamiko maana pana chakula*
SEMINA ZIJAZO.


- 6 Novemba 2016 - Birmingham, Alabama USA
11 - 13 Novemba 2016 - Washington DC USA
Kumbuka kuziombea semina hizi,kusudi la Mungu lifanyike. Mbarikiwe!!
Kusoma Zaidi Mafundisho ya Mwl Mwakasege tembelea
*Facebook*
https://www.facebook.com/Christopher-Diana-MwakasegeMana-Ministry-132462780111984/
Youtube
https://www.youtube.com/channel/UC4p4lrpgpNd-9bHPgHJ4xWw
Ustream
http://www.ustream.tv/channel/mwakasegemanaministry
website
www.mwakasege.org

SEMINA IKO ITAKUWA LIVE YOUTUBE USTREM NA KWENYE www.mwakasege.org na www.kicheko.com
BARIKIWA NA YESU.
Felix…..