MWL: C. MWAKASEGE
AWAMU YA PILI
SOMO:5
MAMBO YA KUFANYA ILI FIKRA ZAKO ZITUMIKE KUFANIKISHA MAISHA YAKO
▶Lengo
Kuweka maarifa ya Kibiblia ndani yako yatakayokuwezesha kutumia FIKRA zako ili ufanikiwe ktk maisha yako
*Mith 23:7(a)*
*HATUA AMBAZO UNAHITAJI KUZIFUATA KAMA UNATAKA KUTUMIA FIKRA ZIKUSOGEZE KIMAISHA*
➡Tumeshaangalia hatua 2 tuko tumeanza seminar. Leo tuendelee na ya 3
3⃣Panga FIKRA zako kwa upya ili zisikupitishe tena mahali pabaya ulipokwisha pitia.
✅FIKRA zinapangika
✅Mfano kwa mama mjane baada ya kusaidiwa na Elisha akitaka hali ile ya mwanzo isijirudie tena lazima abadiri kufikiri kwake la sivyo ile hali atarudi tu
*2Falm 5:7*
Mama mjane alipanga FIKRA zake kwa upya..lazima ujifunze kupanga FIKRA zako kwa upya
Tuonaona mstari wa 7
➡...Nenda kauze mafuta...
Si FIKRA tu kutumika bali MUNGU alitaka Mama mjane ajuaje na akubali ndani yake kuwa MUNGU ndiye amfundishaye kupata faida.
*Isy 48:17*
✅MUNGU hakufunsidhi tu kuhubiri au kuimba bali pia hukufundisha na hupanga FIKRA zako ili zipate kujua MUNGU ndiye akupaye faida
✅FIKRA lazima zipate msaada wa kufundishwa jinsi ya kupata faida
✅Pata tofauti sana kati ya kufundishwa kupata faida na kufundishwa Biashara. Ni sawa na ilivyo tofauti kati ya kufundishwa kufaulu mtihani darasani na kufundishwa juu ya kufaulu mtihani wa kimaisha
✅Maana si kila mtu aliyeko darasani atafaulu maisha, na si kila afanyaye Biashara atapata faida..lazima ujifunze kuvuka hapa
*MAENEO MUHIMU YA KUTAKIWA KUBADILIKA*
*1).* Weka FIKRA zako zikubali MUNGU ndiye anayekufundisha kupata faida
▶Watu wengi wakikwama kiroho hukimbilia kanisani ila uchumi wao ukikwama huwaoni kanisani hukimbilia Benki, sasa sisemi Benki ni mbaya au usiende Benki ila wanasahau kuwa
▶ROHO MTAKATIFU ni mwalimu mzuri sana wa kukufundisha ujasiriamali wenye kupata faida
*2).* Lipa Deni
✅Elisha alimwambia Mama mjane ....kauze kisha lipa deni....
✅Alikuwa anatafuta kitu gani?
▶Alikuwa anapandikiza nidhamu za kutumia fedha ambazo MUNGU amempa kwa sababu zake alizokupa au ulizomwomba tena kwa mwongozo wake!
▶Mama mjane alikwenda kutaka msaada wa watoto wake kutokuchukuliwa watumwa(Alitaka kupata fedha za kuwakomboa watoto wake)
▶Hakuwa na FIKRA zilizojengeka kulipa deni maana Biblia haituonyeshi aliwahi kukopa. Kama huna FIKRA za kukopa huwezi ukawa na (nidhamu) FIKRA za kulipa deni.
*Mama mjane alikabidhiwa matumizi ya fedha ktk maeneo haya*
⚫Kulipa deni
⚫Gharama za kwake na zile za baadaye
⚫Gharama za watoto na za wakati ule wa baadaye
⚫Kuhakikisha ya kwamba hamalizi faida lazima abaki na mtaji.
✳Je unamwomba MUNGU pesa kwa ajili ya nini au kwa ajili gani?
▶Kumbuka pesa huyumbisha mawazo na kujikuta watumia nje ya lile kusudio
▶Ukikorofisha hapo MUNGU hukaa pembeni. FIKRA zinahitaji nidhamu kwenye matumizi ya pesa. Kama MUNGU anakupa kwa ajili ya kitu fulani hakikisha unaielekezea hyo pesa kwenye hicho kitu.
▶Tofauti na hapo utaona ROHO MTAKATIFU anakuhimiza TOBA
*Mith 13:22*
▶Watu wengi wana FIKRA za kujitazama wenyewe tu kwenye upande wa pesa wanajikuta kusahau kuwa wana familia na watoto!
▶Biblia inatuhimiza kuweka akiba mpaka za wajukuu!
▶Usitazame kukwama kwa mme/mke wako ama wazazi wako, usifike mahali hata pa kuwakasirikia badili FIKRA zako ili wewe uvuke hapo kisha mrushie kamba naye atoke hapo oooh hallelujah Hallelujah
*HOME WORK*
➡Orodhesha madeni yako
*Zab 37:21*
✳Umuhimu wa kuorodhesha madeni
▶Usipolipa mikopo MUNGU haji kukupigania katika haki zako.
▶Unapoteza haki katika haki
▶Mikopo isiyolipwa ugeuka deni
▶Deni ubeba vitu (rehani) ili akili zako ziamke. Na baada ya kutaka kuja kuvichukua ndipo akili zako zitaamka
▶Si kila ambaye anashindwa kulipa deni hana hela bali hana mpangilio mzuri wa matumizi na ulipaji
*Yer 22:21*
✅Si kwamba hapendi kusikia bali hataki kusikia maana yake hataki kutekeleza alichoambiwa
✅Gharama kubwa ya kutokufaulu mipango yako ni kupoteza utulivu wa MUNGU kukusemesha
✅Wengi wakisha kopa kwenye kulipa hulipa nusu na nusu wanaweka mfukoni wanasahau MUNGU ndiye aliwafundisha kupata faida na au walipewa kibali cha kupata mkopo
✅Usije ukasahau na kusema huu utajiri ni nguvu zangu wakati ni MUNGU ndiye aliyekupa nguvu za kupata utajiri
*UNAFIKIRI KWANINI MUNGU ALILETA SADAKA*
▶Si kwamba ana shida na pesa yako
▶Lengo la kwanza lilikuwa kutumia sadaka kukutengenezea FIKRA sahihi ndani yako
✳Tazama maana ya
⚫Malimbuko=MUNGU anataka umfikirie yeye kwanza
⚫Zaka ya kwanza=MUNGU anataka kupewa heshima ktk maisha yako
✅Watu wengi kwenye kipindi kigumu na chenye kibano wako tayari kutafuta hela kulipa Benki lakini si kwa MUNGU. Kwa MUNGU excuses zitakuwa nyingi sana na hata kusema "MUNGU we si unajua nilivyobanwa"
✅MUNGU hana maana wala hataki kukufirisi bali anataka kukutengenezea FIKRA zenye Nidhamu
✅Jifunze kumpa MUNGU 100% naye anakurudishia 100%
✅Muulize MUNGU kwanza kwenye kila kitu, ratiba zako, muda wako na mambo yako mkabidhi na mfikirie MUNGU kwanza
✅Usitamani kuiga maisha na FIKRA za mtu mwingine hakikisha MUNGU anakupa mbinu za kujenga FIKRA za kwako mwenyewe.
✅FIKRA zenye kujenga nidhamu ndani yako.zitakufanya utende haki wala hazitakupeleka kwenye kupokea rushwa
✅FIKRA hizi zitakuwekea unyenyekevu ndani yako, kujishusha na kujifunza kutoka kwa wengine
✅Usijaribu ku copy na ku paste kutoka kwa mtu mwingine BWANA atakupa mikakati sahihi ndani yako
*MAOMBI*
*..."Jesus Up"...*
*****SIKU YA TANO*****
SOMO:6
NAMNA YA KUFANYA ILI FIKRA ZAKO ZITUMIKE KUFANIKISHA MAISHA YAKO
▶Lengo
Kuweka maarifa ya Kiblia ndani yako yatakayokuwezesha kutumia FIKRA zako ili ufanikiwe ktk maisha yako.
*Mith 23:7(a)*
▶Tunaendelea na *HATUA....*
4⃣Omba MUNGU akusaidie uweze kupata kutoka kwenye vitabu maarifa yanayohitajika ili uhitajike
*Dan 12:4*
✅Tutazame hatua kwa hatua ktk mtirirko ufuatao:-
*1).* Ni vyepesi mtu kuhitajika akiwa na maarifa yanayohitajika ktk kipindi husika
*Dan 1:17-21*
➡Watu hawakuajiri sababu ya Cheti bali ujajiri maarifa uliyonayo
➡Wakikuajiri sababu ya Cheti na kukaa nawe muda wakagundua una Elimu lakini huna maarifa utashushwa cheo
➡Hatuambiwi kina Daniel walikuwa wangapi, ila walisomeshwa na kupimwa ktk mtihani. Kuanza kwako chuo walikuwa tayari na mtaji..swali la kujiuliza kile walichosomea kiliwasaidia kupata maarifa?
*Dan 1:3-4*
➡Walikuwa na Elimu pamoja na maarifa kwa kiwango fulani.
➡Ilibidi wakae darasani miaka 3 wapate maarifa juu ya maarifa. Haijalishi Elimu na maarifa waliyokuwa nayo awali.
*Mwz 41:37-40*
➡Yusufu alipewa nafasi ya Uwaziri Mkuu akiwa jera baada ya kugundua kuwa ana maarifa
➡Haijalishi uko wapi, jera? Umefunikwa? Umefungiwa au wapi lakini ROHO MTAKATIFU ni mwaminifu atakukutanisha tu na kusudi kama una maarifa yanayohitajika
➡Usiende shule au usisome kwa ajili ya kupata.Cheti bali soma ili upate maarifa. Maarifa yatakusaidia kutoka maishani ila si cheti
*2).* Kuna Vitabu vilivyobeba maarifa yanayotakiwa kwa muda husika
*Dan 12:4*
➡Muda ndiyo unaodai aina ya maarifa
➡MUNGU aliumba kwanza nyakati(muda) kisha mtu
*Mwz 1:1*
➡NENO mwanzo=aliumba muda kwanza kisha mbingu na nchi
➡Muda na maarifa zinaenda pamoja
➡Daniel aliambiwa yatie muhuri= Mtu yeyote akisoma asipate maarifa yaliyomo ndani yake kwa sasa mpaka kwa muda ulioamriwa. Hata yeye kwa kipindi kile asingeelewa hata kama angesoma
*Dan 1:4*
➡Mfalme aliagiza wafundishwe Elimu ya wakaldayo maana yake walikuwa tayari na kiwango fulani cha uelewa.
➡Ni sawa na kuchukua mtoto wa darasa la kwanza kumpeleka Chuo Kikuu haiwezekani maana kuna ngazi tofauti tofauti maana *Umri uenda na aina fulani ya kufikiri*
➡Ni hatari sana kusoma na kuwa na Elimu halafu huna lugha ya kutafsiri maarifa hayo(Wasoma kiswahili halafu interview kichina)
➡Kumbuka lugha inakunyima kazi
➡Njia yako uendana na lugha vilevile yaani kuchukua maarifa Ujerumani siri imefichwa kwenye kitabu hicho cha lugha ya kijerumani. Lazima usome mwaka mzima kijerumani kwanza kuweza kutoa maarifa yaliyoko humo.
*Ayb 35:16*, *34:35*
➡Kuna maneno hayana maarifa.
➡Si kila kitabu chenye maarifa chaweza kukusaidia isipokuwa kwa wakati sahihi na muda ulioamriwa!
*3).* Vitabu vilivyobeba maarifa uwa vingine vinafungwa visitoe maarifa hadi muda/wakati wa kuhitajika kutoa maarifa au muda umekaribia au umewadia
*Dan 12:4*
*Dan 9:1-3*
➡Kitabu chochote chenye sababu hii ya (3) lazima ukishakisoma utapata msukumo wa kuyaweka kwenye matendo yale yote uliyoyasoma
➡Nunua Vitabu Chini ya msaada wa ROHO MTAKATIFU, mwombe MUNGU akupe hekima kununua vitabu ambavyo.vina maarifa unayoyahitaji. Hii ni nidhamu unahitaji kujiwekea
➡Kumbuka kitabu chichote kilicho na maarifa ya wakati huo na sahihi kinakupelekea kupata msukumo ndani yako kuweka kwenye matendo hayo uliyosoma na kupata msukumo wa kuyaombea.
*4).* Ni muhimu kwa kitabu kufunguliwa na akili ya msomaji kufunguliwa kwa pamoja ili maarifa yaliyomo ndani ya kitabu yawe msaada ktk muda husika kwa ajili ya msomaji huyo
*Luk 24:44-49*
➡Kitabu kilikuwa kimefunguliwa lakini akili zao zilikuwa zimefungwa
➡Kitabu kilifunguliwa kwa ajili yao na YESU alijua akisema nao waweze kuoanisha kutoka kwenye vitabu vya torati na zaburi ndiyo maana akili zao zilifunguliwa na kufunuliwa wapate kuelewa walichokisema manabii waliotangulia kinatimia sasa
*5).* Mwombe MUNGU akukutanishe na Vitabu vilivyobeba maarifa unayoyahitaji na avifungue kama bado vimefungwa ili upate maarifa unayostahili kama hayo
*Uf 5:1-5*, *10:1-11*
➡Simba wa Yuda (YESU) alipata nafasi ya kukifungua kitabu.
➡Kitabu kinaweza kikawa kimefungwa ukaomba kifunguliwe
➡Pia kinaweza kikawa kimefunguliwa, sasa omba maarifa ukifunguliwa akili uweze kukielewa
➡Tazama Biblia ni kitabu bora na ni ileile inabeba maarifa ya kukusaidia bila kujali muda uliowekwa maana muda ukifika unafunguliwa tu
➡Jiulize ni kwanini watu wengi wanasoma shule lakini si wabunifu? Mfano waliosoma Administration waambie waanzishe ofisi binafsi uone..wanasubiri ku copy na ku paste ila leo MUNGU anakutafuta kukupa maarifa ukagunguliwe akili...oooh hallelujah!
*MAOMBI*
Orodhesha madeni yako maombi yataendelea siku ya 7(leo)
✅Maelfu ya watu walimpokea YESU pia
*..."Jesus Up"...*
*****SIKU YA SITA*****
SOMO:7
NAMNA YA KUFANYA ILI FIKRA ZAKO ZITUMIKE KUFANIKISHA MAISHA YAKO
▶Lengo
Kuweka ndani yako maarifa ya Kiblia yatakayokuwezesha kutumia fikra zako ili ufanikiwe ktk maisha yako
*Mith 23:7(a)*
*Summary*
✅Kubadili maisha yako badili kufikiri kwako
✅Maana ya fikra...rejea day 1
✅Hatua ambazo unahitaji kuzifuata kama unataka kutumia fikra zikusogeze kimaisha..rejea day 1-6
✅Jana tuliangalia mtiririko wa mambo kama 5 hivi, lile la 5 tuliangalia; uhusiano kati ya maneno na Vitabu maana kitabu kimebeba maneno, muda na maarifa *Dan 12:4*
✅Maarifa ndani vitabu uachiliawa kufuata na uhitajika wake kipindi husika
✅Wazo la vitabu lilianzia rohoni si mwilini
..Tuendele na mtiririko huo..
*6).* Zijue njia za kupata maarifa kutoka ndani ya maneno yaliyomo ndani ya kitabu
*Josh 1:8-9*
▶Maneno ya MUNGU alizungumza na Joshua baada ya Musa kufa
▶Alikuwa akimtia moyo kuendelea mbele na watu wake ili kusudi litimie.
▶Joshua alitazama kazi aliyopewa na kuangalia kufanikiwa pamoja na kustawi kwake pamoja na watu wake hakika kwake halikuwa jukumu jepesi ndiyo maana alipewa njia ya kunsaidia...mstari wa 8
▶Aliambiwa chukua kitabu maana humo ndiko kuna maarifa ya kushinda kwako.
▶Maana miaka 400 walikaa bila kuwa na utaratibu wa KIMUNGU, MUNGU baada ya kukumbuka Agano alilofanya na Ibrahim na Yacobo akawatoa utumwani, walipofika Sinai akatengeneza utaratibu ambao utafananafanana na yeye ili kukaa nao. Lilikuwa jambo jipya sana kwako
▶MUNGU akija na kuamua kukaa mazingira take ubadilika kabisa ndo maana akatengeneza kitabu na ndani yake kuna maarifa, kuna masuala ya ujenzi, kilimo, uchumi, mahusiano ya kila aina, kitabu kukusaidia kustawi sana na uweze kuishi pamoja naye
*JOSHUA ALIAMBIWA VITU 3 VYA MUHIMU ILI UWEZE KUTOA MAARIFA NDANI YA KITABU, NA NI KITABU CHOCHOTE KILE*
1⃣Kisiondoke kinywani mwako
✅Jifunze kufikiri kila ambacho unakiona na kukisoma ndani ya kitabu na kutaka kitokee kwako
✅Jifunze kusema kila unachokiamini ndani ya kitabu *Mark 11:23*
✅Yale uliyonayo utegemea sana kile unachosoma na kukisema
*Rum 10:8-10*
✅Ukitaka kupata kilichopo kwenye kitabu lazima ukiri. Ukikuta mtu anapinga kilichopo ndani ya kitabu jua hakitatokea kwake
*Zab 45:1*
✅Ulimi unaandika
✅Kuzungumza ni kuandika kwenye mioyo na vibao vya nyama kwako.
✅Ndiyo maana ni rahisi tukikutazama tukajua nani kaandika ndani yako
✅Unaposema unaandika kwenye nafsi yako
✅Haitoshi kusoma jifunze kusema maana uanzia kuandikwa ndani. Maana sauti ninayoisikia kuongea si sauti ninayoisikia kuongea
2⃣Yatafakari maneno take mchana na usiku
✅Ni zaidi ya kusoma, kukariri
✅Tamka kutoka moyoni. (Meditation)
✅Tafakari=Tafuna
✅Kukariri=Kumeza na hii so guarantee zitafanya kazi
✅Huwezi ukatoa maarifa ndani ya kitabu bila kutafakari= fikra na akili zako kuchanganya ili utakapotembea utakuwa neno linatembea. Maana NENO alifanyika mwili akaa kwetu
✅Kutafakari NENO kuna kupa nafasi ya kutafuna na kupata nafasi ya kuwa na maswali mengi sana utakuwa mtu wa kutembea na note book na kalamu Mara nyingi si Ku copy na kupaste bali utapata maarifa zaidi
3⃣Upate kuangalia na kutenda sawasawa na maneno yaliyoandikwa humo
✅Utendaji unahitaji nidhamu ya kiwango cha juu sana
✅MUNGU anapoachilia wazo la biashara ndani yako usiwe na haraka kushirikisha watu maana kufanya hivyo kesho utamkuta mwenzako katekeleza..unahitaji nidhamu ktk hili
✅Swala si wazo au utekelezaji bali anahitaji kukuweka utaratibu wenye nidhamu kwanza
*Muh 12:9*
Tuongezee jambo jingine
4⃣Tafuta waalimu ambao wanakufundisha upate maarifa si wale watakaokufundisha upate darasa=cheti
✅Hata ktk vyuo vya kuandaa walimu lazima waandaliwe kutoa maarifa ndani ya Vitabu na si tu wawafundishe wanafunzi kunaliza shule
✅Binafsi nitamsikiliza na kumfuatilia mwalimu yule kesho na kesho kutwa kila nikimsikiliza nitapata maarifa=lugha ya mjini ninamwelewa sana
✅Paul alipokuwa na kiu ya kumtumikia MUNGU alipata waalimu walikuwa wanatoa maarifa ya Dini si maarifa ya KRISTO
✅Jiulize kwanza waalimu gani wanakufundisha? Unapeleka watoto shule jiulize ina walimu wa namna gani
*7).* Uwe mwangalifu na Vitabu unavyosoma
✅Si kila Vitabu vina uwezo wa kutoa maarifa
✅Kuna vingine haviendani na njozi yako. Hivyo usipoteze muda mwingi kusoma visivyo vya kwako maana muda hautoshi na huna muda wote ukifikiri ni wa kusoma
*Muh 12:12*
✅Vutabu ukisoma vinakuchosha
✅Usijaribukushindana na watunzi wa Vitabu ktk kusoma maana utakufa na wataendelea kutunga tu
✅Pia kuwa mawangalifu sana na Vitabu vya hadithi maana hutoa maarifa ndani ya mtu na pia utoa maarifa kwa njia ya hadithi *1Tim 1:3-4*
*Matendo 19:19*
✅Vilichomwa Vitabu hivyo maana maarifa yake yalikuwa hayatakiwi
✅Kama Vitabu vimepitwa na wakati wasomaji wakisoma fikra zao urudishwa nyuma ila vipo vile Vya zamani ambavyo maarifa yake ni ya mbele
*8).* Jizoeze kwa maombi kunyunyizia DAMU YA YESU juu ya kitabu unachosoma
*Ebr 9:19-22*
✅Maana si kila kitu unachosema kitakuzalishia jambo ulitakalo
*Ayb 38:2*
✅Maneno yasiyokuwa na maarifa uachilia giza
✅Mfano angalia ukitaka kusoma Biblia sekunde chake umechoka, umelala, uelewi lakini tazama ukitaka kusoma msg kwenye Simu au gazeti, waweza soma msg zote na magroup yote bila kuchoka na kuwa active zaidi
✅Ukigundua hili unajua ni vita na DAWA YAKE NI DAMU YA YESU PEKEE
✅Kabla ya kusoma achilia DAMU ya YESU kuondoa Giza na kufunga fikra usielewe
✅Jifunze kuombea miguu ya waalimu
✅Jifunze kuombea eneo unalopatia elimu. Mussa aliambiwa vua viatu
✅Kuna uhusiano mkubwa kati ya miguu na sikio na kichwa pia
✅Hatua unazokanyaga na jinsi unavyofikiri kuna uhusiano mkubwa sana
✅Miguu lazima ifungwe utayari maana waweza pata maarifa halafu ukapata uzito kutekeleza.
✅Shetani akiweza kukubana kwenye miguu yako na masikio yako huwezi kufanikiwa hata kidogo.
✅Jiulize Mara ya mwisho kusoma Biblia tena unayo kwenye Simu yako ni lini? Ila Mara ya mwisho kusoma msgs ndani ya Simu ni lini?
*MAOMBI*
✳Masikio yako vs Simu yako
*..."Jesus Up"...*
*****SIKU YA SABA*****
SOMO 8
NAMNA YA KUFANYA ILI FIKRA ZAKO ZIFANIKISHE MAISHA YAKO*
Tumekuwa na semina nzuri sana na kama ni siku yako ya kwanza tafuta kanda. Na somo hili hapa ndio nilikuwa naanza tu kwenda ndani kwa hiyo omba kwa Mungu ili atupe tena nafasi nyingine maana somo bado linaendelea.Pia ombea na kamati maana muda wetu wa kufanya semina hapa Dar es Salaam ni kipindi cha mvua hasa ile semina ya Kwanza kwa hiyo omba tupate muda mwingine au kiwanja kingine.
Tumesoma neno kutoka Mithali 23:7a Maana aonavyo mtu nafsini mwake. Na tumeangalia tafsiri mbali mbali, moja inasema atafsirivyo, na nyingine imesema anavyotafakari . na pia ukisoma Zaidi ndipo utajua na tafsiri zingine nyingi.
Na nilikuambia kuwa *Fikra ni mkusanyiko au mtirirko wa mawazo yanayotengeneza msimamo wa kiutekelezaji ndani ya mtu* na Fikra zina tafsiri mbali mbali. Kwenye siasa/ Uchumi tunaweza sema ni *sera* na kwenye makabila tunaweza sema ni mila.
*Hatua ya Tano*. *```Jizoeze kijiuliza maswali yanayofanya Fikra zako zifikiri kiubunifu```*
*1* *Jifunze kufikiri juu ya soko kwanza kabla kitu unachofikiri kuuza*
Tafuta soko kwanza hata kama, yaani demand ya kitu chako kwa sababu biblia inasema *anatanga mwisho tangu mwanzo*. Start with end in mind. Usianze kulima shamba lako kama hujui unalima kwa ajili ya nini yaani unalima kwa ajili ya chakula au kwa ajili ya biashara. Na kama hujajibu swali hili kuwa unalima kwa ajili ya nini ujue tayari umefeli.
*MFANO* Kuna wakati nilitaka kulima maparachichi kwenye shamba ambalo baba alituachia urithi. Na nilitafuta watu wanaotaka tulime kwa mkataba yaani tukivuna wao ndio wananunua na alikuwepo mzungu mmoja ananunua hayo maparachichi. Nilitafuta mawasiano yake nikayapata na nikaongea nae ila sikupata majibu sahihi kwa hiyo nikaamua kumfuata kule kule aliko. Na Nilikuwa na maswali ambayo nataka kujua kwa sababu ukilima maparachichi baada ya miaka miwili unavuna na uzalishaji wa mti ulioupanda unaanza kupungua mwaka wa sita. Yaani baada ya miaka sita uzalishaji unashuka. Na kuanza hicho kilimo ilikuwa inahitaji hela nyingi kidogo, ili kuwekeza. Na kwa kuwa kuuza kutaanza baada ya mwaka wa tatu kwa hiyo nikamuuliza baada ya mwaka wa tatu (yaani tokea ukipanda itakuwa imepita miaka 3 hadi unaanza kuvuna) bei yake itakuwa sh ngapi? Akasema hajui sasa nikamauuliza tena je wewe utakuwa unauza wapi? Akasema Uingereza, sasa nikamauuliza kama wewe utakuwa unauza uingereza basi ni kuwa lazima umepiga hesabu za bei na ndio maana umekuza kuwekeza huku kununua maparachchi.
Na hakupenda sana maswali yangu maana hakutegemea kama kuna mtu atamuuliza maswali kama yale kwa sababu walikuwepo wengine wanalima tu kwa kuwa wamesikia mzungu ananunua. Na mimi nilimwambia kuwa *nahitaji kupiga mahesabu* kwa sababu hata kama nataka nikakope benki lazima wajue kuwa je huu mradi ninaoutaka kufanya je utakuwa na faida? Na je utaweza kuerejesha mkopo wao na je mimi mwenyewe ntapata faida?
Mradi wowote hata kama unaweka pesa za kwako jaribu kupiga mahesabu na jaribu kuwauliza na watu wa benki kama wanaweza toa mkopo kwenye aina hiyo ya mradi? Kwa sababu benki huwa wanaangalia kama huo mradi unaweza rudisha hizo hela zao unazotaka kukopa. Na ukiona benki wanakaa basi ujue kuwa mahali hapo ni hatari kuwekeza kwa lugha ya kitalaamu tunaita *risk* na hata kama unalipa vipi uwe makini nao sana au acha usiweke hela yako hapo maana inaweza ipotee.
Kwa hiyo nikaenda kuwauliza Wafanyakazi wake na wao pia waliweza kujibu kwa sehemu basi, nikaa chini nikapiga mahesabu na nikagundua baada ya mwaka ya 5 ndio naweza pata faida ya laki 7 (700,000) yaani hiyo ndiyo faida na wakati uwekezaji wake umenigharimu mamilioni ya pesa. Kwa hiyo nikamwambia yule mzungu kuwa siwezi kulima kwa sababu kama nalima kwa ajili ya biashara nahitaji faida na kama maparachichi ya kula ntanunua sokoni. Kwa hiyo *Fikiri kwanza soko kwa sababu ile chupa ya mafuta ingekuwa haina thamani kama hamna soko*
*2* *Zizoeze fikra zako kufikiri kiubunifu*
Fikra za aina hiyo ndizo zinaoleta viwanda, kwa sababu viwanda vinakuja kwa njia ya ubunifu. Na kasome uingereza , Ujerumani na Afrika ya Kusini. Utajua hiki nianchokummbia,
*3* *Tafuta kujua mahitaji ya muda*
Biblia siku ilitoa kabisa mwongozo kuwa maarifa siku za mwisho yatakuwa mengi sana na yatenda kwa spidi sana. Kwa hiyo ukijua mahitaji muda husika iatkusaidia sana, Kwa mfano, Mwanvuli ni kwa ajili ya kipindi cha mvua na ukitumika kipindi cha kiangazi utatumika kwa kazi zingine kabisa.
Tulikuwa na mkutano mmoja huko marekani na moyor wa lile jiji alitangaza kuwa kutakuwa na barafu *Storm* na hali ya hewa ingebadilika sana na nikawa natazama kwenye television wakawa wanatabiri kuwa hata safari za ndege zataahirishwa na hata wanafunzi walitangaziwa kuwa hakuna kwenda shule kwa sababu ya barafu itakayoshuka. Na sisi ilikuwa inatakiwa tuondoke siku hiyo. Basi nikaingia kwenye maombi kama masaa mawili hivi ili kusemesha mbingu za mahali pale ili kuzuia hiyo barafu na niweze kuondoka na ndege yetu pia iweze kuwepo yaani *flight isiwe cancelled* yaani iahirishwe.
Walifanya kila maandalizi na magari yaliliyokuwa na chumvi tayari kwa ajili ya kuyeyusha barafu huko barabarani na pia hata magari ya kwenda airport ilikuwa ni tabu sana kwa sababu walishatangaziwa kuwa watu wabaki nyumbani kwao . Basi tulifanikiwa kutoka na tukaenda airport na tuliikuta ndege yetu ipo na safari za ndege zingine ziliahirishwa.
Na tulikopokuwa tunatazama television tena na zile saa walizotabiri kutokea kwa hizo storm hazikutokea na walishindwa kutoa sababu, na tuliwaambia watu wawili tu wa ule mji. Na baada ya sisi kuaondoka ilishuka storm kubwa sana. Hawakujua kuwa ni sisi ndio tulibadilisha hali ya hewa ya mahali pale.
Na tulipoondoka rafiki yetu mmoja alituambia kuwa ile chumvi yote imeharibika kwa sababu chumvi iliandaliwa kwa masaa na haikuandaliwa kwa ajili ya chakula. Na ndio maana iliharibika . ndio maana nakuambia kuwa *zizoeze fikra zako kufikiria mahitaji ya muda*
*1* *Ukisikia malalamiko popote usizizoeze fikra zako kulalamika, Bali fikra zako zijue kujibu juu ya
~~ *nani analalamika*
~~ *Kwanini analalamika*
~~ *Anamlalamikia nani*
~~ * Muda gani analalamika*
~~ *Malalamiko yake huwa yanajirudia kipindi gani*
>>Hata kama ni halali kiasi gani, wakati wenzio wanalalamika chukua fikra zako kufanya utafiti na ujue ni akina nani wanalalamika, kwanini, lini na wanamlalamikia nani.
*MFANO* Hesabu 13-14
Habari za wapelelezi, ambao walitumwa kwenda kuipeleleza nchi ya Kanani na walitumwa kwa sababu za kiuchumi kabisa kwa sababu hawakutumwa habari za kiroho kujua wale watu wanasali wapi au la.
*SABABU WALIZOTUMWA*
>> _Hesabu 13:17-20 17 Musa akawapeleka ili waipeleleze nchi ya Kanaani, akawaambia, Pandeni sasa katika Negebu mkapande milimani,
18mkaitazame nchi ni ya namna gani; na watu wanaokaa ndani yake, kwamba ni hodari au dhaifu, kwamba ni wachache au wengi;
19na nchi wanayoikaa kwamba ni njema au mbaya; kwamba wanakaa katika matuo au katika ngome;
20nayo nchi ni ya namna gani, kwamba ni nchi ya unono au ya njaa, kwamba ina msitu au sivyo. Iweni na moyo mkuu, mkayalete matunda ya nchi. Basi wakati ule ulikuwa wakati wa kuiva zabibu za kwanza.
Angali pia na katika iingereza (NIV) hii mistari
*Numbers 13:17-20 17When Moses sent them to explore Canaan, he said, “Go up through the Negev and on intothe hill country. 18See what the land is like and whether the people who live there are strong orweak, few or many. 19What kind of land do theylive in? Is it good or bad? What kind of towns dothey live in? Are they unwalled or fortified? 20 How is the soil? Is it fertile or poor? Are theretrees in it or not? Do your best to bring back someof the fruit of the land.” (It was the season for thefirst ripe grapes.)*
Hawa wapelelezi walitumwa kwa masuala ya kiuchumi kabisa na walitumia siku 40 kufanya utafiti na aliwaambia waliete na matunda ya zabibu ili wasije na cooked data yaani wangeweza wasiende maana wangefanya utafiti wa kuitungia. Kazi ya utafiti ni kuwasaidia watu kuweza kufikiri.
Angalia Majibu ya Utafiti wao mstari 33 *Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi*. Soma sura zote mbili ndiponutaelewa vizuri.
Fikra zao zilishindwa kutafsiri kile kitu ambacho Mungu alitaka waone. Na Mungu alisema hawa watu nitachukuliana nao hadi lini?
*VITU VYA KUJIFUNZA KATIKA HABARI HII*
a). Mungu alikuwa anataka kuwaonesha tatizo ina maana alikuwa anawaandaa kifikra ili waweze kutafsiri na kujua namna ya kutatua tatizo maana kutatua tatizo ndio chakula chao.
*Mithali 3:5-6 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako*
Fikra zako inabidi zikae mkao wa kutafuta suluhu ya tatizo, na akili zako zikifanya kazi na Mungu ujue kuwa lazima utafanikiwa.
b). Mungu aliijua Kanani vizuri sana, kwa sababu aliwaambia kuwa ni nchi ya maziwa na asali. Na hawakujua kuwa maziwa na asali ni processed products
*2* * Kulalamika ni ishara ya kuwa fikra zako hajioni jibu bali zinaona kikwazo*
*3* *Fikra ziliumbwa ziweze kutafsiri changamoto ili ziwe fursa*
Ukisoma 2 Wakorintho 4:3-4 utona habari za kuwa ibilisi hupofusha fikra za watu . maana Mungu alipoumba changamoto au matatizo ni ili watu waweze kula. Kwa sababu ukisoma biblia mwadamu aliumbwa na hamna mahali alipewa kitanda cha kulala. Maisha ya Mwanadamu 1/3 ni anatakiwa kulala. Sasa inatetegemea yeye mwenyewe atalala wapi kama kwenye majani, au kwenye ngozi au kama kitanda kizuri au ni banko. Ni wewe mwenyewe, kwenye biblia huwezi kuta kuna mahali Mungu alisema pawe kitanda. Sasa ni jukumu lako kutengeneza kitanda. Sasa unapohitaji muujiza wa kitanda fikiri kwanza.
Katika biblia huwezi kuta kuna neno maendeleo, nilitafuta kwenye concordance (itifaki ya biblia) ni kitabu chenye kuonesha maneno yaliyomo kwenye biblia. Sasa katika biblia neno maendeleo limefichwa kwenye neno *nuru* maana yake aliposema kuwe Nuru ina maana kuwe na maendeleo.
*4* *Ile kwamba mtu amekutangulia haina maana kuwa anafikiri vizuri kuliko wewe*
Wana wa Israel walipokuwa jangwani, na wenzao waliotumwa kwenda kanani kupeleleza nchi ina maana ilitakiwa waweze kufikiria mbele kuliko wenzao. Lakini Fikra zao zilikwama na wao waliishia jangwani. Na katikati ya Jangwani na Kanani kulikuwa na Fikra, japo imani walikuwa nayo ila fikra zao ziliwakwamisha na waliishia pale. Ila watoto wao ndio alienda kwenye nchi ya Kanani. Kwa hiyo angalia kinachokutoka katika kinywa chako.
Ukifikiri kama ni watu wanaokaa jangwani na wewe utabaki jangwani maana unaweza kwama hapa walipokwamia. Kwa hiyo mtu anaweza akawa mkubwa lakini fikra zake bado ni ndogo.
*5* *Palipo na Malalamiko hapo ni fursa ya chakula fanya utafiti wa kulalamika kwako
~~ *nani analalamika*
~~ *Kwanini analalamika*
~~ *Anamlalamikia nani*
~~ * Muda gani analalamika*
~~ *Malalamiko yake huwa yanajirudia kipindi gani*
Ukiona watu wanalalamika, basi wewe zifanye fikra zako ziweze kufikiri na fanya utafiti maana kuna chakula hapo. Na hii ndiyo iliyotoa fursa kwa akina Kalebu na Joshua. Maana Mungu alipowaonesha matatizo wao walitafsiri kwa matatizo kama Fursa,
Kule kulalamika kwa wana wa Israel, kulisababisha wao kutokwenda Kanani ila watu wawili tu. Sasa piga hesabu watu waliotoka Misri walikuwa ni zaid ya million 2 lakini walioingia Kanani ni Wawili tu. Na hawa ni watu walioweza kutafsiri na fikra zao zilifikiri tofauti na wengine.
Hata huko mbinguni naamini huwa wanacheka sana maana kuna wengine wanaona kuna majitu Mungu tunaomba kuyaondoa na wengine wanaona chakula.
*MFANO WA 2* *Hesabu 11:11-15*
Hapa tunaona habari za Musa kuwa alianza kulalamika na alipokuwa anamlalamikia Mungu na katika kulalamika kwake kulitengeneza ajira ya watu 70. Na ukiona kiongozi analalamika kuwa kazi zake zimemzidi basi anza kukaa mkao mzuri maana kutakuwa na kazi hapo. Na wewe ukiungana na kulalamika kwake basi wakati anatangaza kazi zingine atakuacha kwa sababu wewe ni mlalamishi.
*MFANO WA 3* *Habakuki 1-2*
Sura ya kwanza tunaona Habakuki akilalamika kutokana na kutokuwepo haki. Na baada ya kulalamika Mungu alijibu kulalamika kwake. Na alimjibu kuwa kwa njozi na njozi inamfanya aweze kufikiri. Kwa sababu ukipewa njozi bila matatizo inakuwa haina maana. *Vision must have problem to solve or must have value*
Na kama akili yako inaweza kusolve matatizo ya watu basi ujue kuwa kuwa utakuwa demanded . na ndivyo ilivyotunavyouza kahawa ambayo bado iko katika hali ya kuwa ghafi. Na ukiweza kufikiri ina maana unaweza kubuni kiwanda cha kuweza kuprocess .
Fikra zako ili ziweze kufanya kazi Zaidi inatakiwa unapokuwa unaomba kwa Mungu unganisha na matatizo yaliyopo kwenye jamii yako na omba Mungu akuwezeshe kukusaidia kujibu hayo matatizo na ukienda na kanuni hii basi ujue utapata business idea,. Thamani ya Mwalimu ni uhitaji wa Kiroho wa wanafunzi.
*Ombea Fikra zako mara kwa Mara ili Mungu aweze kuzifungua. Na hapa ni mwanzo omba Mungu ataoe tena kibali cha somo hili ili tuweze kuendelea. Homework Tafuta mahali penye malalamiko maana pana chakula*
SEMINA ZIJAZO.
- 6 Novemba 2016 - Birmingham, Alabama USA
11 - 13 Novemba 2016 - Washington DC USA
Kumbuka kuziombea semina hizi,kusudi la Mungu lifanyike.Mbarikiwe!!
Kusoma Zaidi Mafundisho ya Mwl Mwakasege tembelea
*Facebook*
https://www.facebook.com/Christopher-Diana-MwakasegeMana-Ministry-132462780111984/
Youtube
https://www.youtube.com/channel/UC4p4lrpgpNd-9bHPgHJ4xWw
Ustream
http://www.ustream.tv/channel/mwakasegemanaministry
website
www.mwakasege.org
SEMINA IKO ITAKUWA LIVE YOUTUBE USTREM NA KWENYE www.mwakasege.org na www.kicheko.com
BARIKIWA NA YESU.
Felix…..
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni