Ijumaa, 28 Oktoba 2016

Mambo 7 muhimu ya kuzingatia kutoka kuajiriwa hadi kujiajiri

Kuna sababu mbalimbali kwanini mtu atake kuajiri, badala ya kuajiriwa, mfano kipato kidogo anachopata katika kazi husika, hitaji la kutaka uhuru zaidi binafsi wa kufanya kazi, hitaji la kuweza kutoa ajira kwa wengine na zaidi sana kuweza kutumia vema kipaji na uwezo wa kuzalisha ambao katika kazi ya sasa mtu hapati nafasi ya kufanya hivyo. 

Kujiajiri ni jambo linalohitaji maandalizi ya muda mrefu na kuna mambo ya msingi kuyafahamu, haiwezekani tuu , ukaacha kazi na kusema ok, acha nijiajiri.

Makala hii inachambua mambo ya msingi ya kujiandaa na kuyafahamu kabla mtu hajaamua kuacha kuajiriwa.

Mkakati ni muhimu
Wazo au ndoto isiyo na mkakati wa kuitimiza ni upuuzi yaani ndoto hiyo au wazo hilo halina maana, hivyo basi ndoto yako ya kujiajiri siku moja, ni lazima iwekewe mkakati wa kuifanikisha ikiwa ni pamoja na muda hasa wa lini utaitimiza hiyo ndoto.

Katika kuweka mkakati huu wa kutimiza ndoto yako, fanya utafiti wa kina kuhusu mipango yako binafsi ya maisha, mtazamo wako kuhusu maisha, mpenzi/mke wako, familia yako, na hali ya jamii kwa ujumla inavyoenda kama vile mabadiliko ya hali ya kisiasa, teknolojia, na uchumi.

Tengeneza malengo ya aina ya shughuli unayotaka kuifanya ukiacha kuajiriwa, na pima uwezekano wa shughuli hiyo kufanyika kweli na kama itakulipa. Utambue pia aina ya watu na rasilimali nyingine utakazozihitaji, na jinsi utakavyozipata

1.unahitaji fedha
Ndio, unahitaji kiasi cha fedha za kutosha kununua vifaa na malighafi za kutengenezea bidhaa yako. Pia unahitaji fedha za kuwalipa wafanyakazi wako, na zaidi sana , unahitaji fedha za kuendesha maisha yako na familia yako , kwa kipindi fulani kabla ya biashara kuanza kukulipa mshahara. Hivyo kabla haujaacha kibarua chako, hakikisha umetengeneza bajeti ya kutosha na una akiba ya kutimiza mahitaji ya bajeti yako. Usingependa uache kazi halafu uanze kuwa omba omba kwa rafiki na jamaa, au uanze kujuta.

2.Network ni muhimu
Kumbuka katika kujiajiri kwako, utahitaji wateja, washirika, wafanyakazi na hata washauri mbalimbali ili mambo yako yaende vizuri. Hivyo, wakati ukiwa umeajiriwa ndio wakati wako muafaka wa kutengeneza na kupanua wigo wako wa watu unaowafahamu na waliokaribu nawe.

Kumbuka kuendeleza mawasiliano kwani watu hawapendi kuona wewe unataka kuwatumia tuu kisha unawatupa. Endeleza mawasiliano walau hata kwa salamu tuu. Zaidi sana, heshimu watu wote, hata usiowafahamu au wale unaodhani 'sio watu muhimu'.

Jenga taswira nzuri kwa jamii kwa lugha fasaha, picha na matukio mengine, usifanye watu wakufikirie vibaya.

3.Usipitwe na wakati:
Hakikisha kuwa unafuatilia taarifa za matukio, dili na watu wanaohusiana na aina ya shughuli unayopanga kuifanya wakati utakapojiajiri. Hii itakusaidia kupata uzoefu na kusoma alama za nyakati, na pengine kutambua fursa nyingine zaidi.

Endelea kujifunza zaidi kuhusu kazi yako, watu na jamii kwa ujumla kwani kujiajiri kunahitaji uzoefu zaidi, na zaidi sana uwezo wa kupambana na changamoto nyingi ambazo nyingine haujawahi kukutana nazo kabisa, ila taarifa za awali na kujua jinsi mambo yanavyoenda kwa ujumla katika jamii vitakufanya ushinde changamoto.

4.Maana halisi ya biashara
Baada ya kuacha kuajiriwa, hautarajii kuwa mtu wa ‘kuganga njaa’ yaani kufanya biashara ili mradi tuu hela iingie, lakini haujui mwelekeo wa biashara yako upoje, na wala hakuna mkakati wa kuikuza na kuimarisha biashara husika.

Biashara inahusu kutimiza mahitaji ya watu, kwahiyo ili mradi utakuwa na uwezo mkubwa wa kutimiza mahitaji ya watu, na kuendelea kuhamasisha watu zaidi kuja kwako uweze kutimiza mahitaji yao , basi biashara itakua, na itaendelea kuwa endelevu.

Kinyume cha hapo, ushindani utakutoa katika biashara kwani wateja watakambilia kwa wengine. Biashara sio tuu kupata wateja, ni vile kuweza kuendelea kupata wateja na kuendelea kupanua biashara.

Inabidi uipende shughuli husika unayoifanya, na uweze kutimiza mahitaji ya wateja kupitia biashara husika.

Muda wako mwingi utautumia katika shughuli yako mpya utakayojiajiri hivyo, kama ambavyo kazi uliyonayo pengine ‘inakuboa’, hakikisha ajira yako binafsi ‘haikuboi’.

5.Umuhimu wa wafanyakazi
Watendaji wa shughuli husika za biashara yako utakayoianzisha ni muhimu wawe wenye ujuzi na uzoefu wa kutosha wa kufanya shughuli husika, na uweke mikakati ya kuwapatia nyenzo zote muhimu za kufanyia kazi ikiwemo teknolojia na mazingira mazuri ya kazi. Hivyo basi wakati unajiandaa kujiajiri tilia maanani hili katika bajeti yako ya kuajiri. Usingependa wafanyakazi wao wajisikie vibaya kama vile wewe ulivyojisikia vibaya katika ajira yako fulani (pengine ajira yako ya sasa). Muda huu ambao umeajiriwa, ndio muda pia muafaka wa kusaka 'vipaji'- yaani watu ambao utafanya nao kazi utakapojiajiri.

6.Inakuhusu wewe 
Mafanikio yako katika kujiajiri yanategemea mambo mengi ila zaidi sana yanakutegemea wewe. Je, nini hasa sababu yako ya kutaka kujiajiri?

Ni kweli una bidhaa au huduma haswa ya kupeleka sokoni itakayokufanya iendeshe maisha yako na kuiendeleza biashara husika au ni hasira tuu za jinsi bosi wako anavyokuchulia hapo ofisini kwako, au kwakuwa mshahara uliopo sasa haukutoshi. Je, mipango yako mingine ya maisha ipoje?

Ndoto zako za kusoma, au kuishi sehemu tofauti tofauti, pengine mkoa mwingine tofauti na uliopo sasa, au pengine hata nchi husika. Je, yote hayo yanaathiri vipi mipango na mikakati yako ya kujiajiri, bila kusahau msukumo toka kwa familia yako.

7.Ndoto sahihi
Ni kweli kuwa upo sahihi kufikiria au kuota kufanya biashara kubwa na yenye mafanikio sana, lakini kumbuka mafanikio hayaji kwa usiku mmoja, na hata kama yatakuja kwa usiku mmoja, inahitajika kazi ya muda mrefu kuyafanya yawe endelevu.

Hivyo basi, usingoje wakati ‘muafaka’ wa wewe kuwa na kiasi kikubwa cha fedha au kwamba ‘umeyaset’ vema mambo yote.

Anza kidogo kidogo, kubali kufanya makosa, na tambua kuwa hata kama utafanya uchambuzi na uchunguzi wa kutosha kuhusu soko, jamii na teknolojia, hali halisi unayoenda kukumbana nayo inaweza kuwa tofauti na ile uliyojifunza wakati wa uchambuzi au uchunguzi wako kwakuwa hicho unachoenda kufanya ni kipya hakikufanyiwa uchambuzi, bali unakifanya kutokana na uchambuzi uliofanya hapo awali.

Kuna mtu mwingine atakuja kutumia makosa au mafanikio yako kupanga mambo yake.

Alhamisi, 27 Oktoba 2016

FAIDA KUMI ZA KUNYWA MAJI MOTO YENYE LIMAO

FAIDA KUMI ZA KUNYWA MAJI MOTO YENYE LIMAO KILA UNAPOAMKA ASUBUHI




1.Huongeza Kinga yako ya mwili hasa kupambana na magonjwa madogo kama mafua, na kikohozi kutokana na kuwa na vitamin C

2. Husafisha Mfumo wako wa chakula, kuondoa sumu mwilini na kuzuia tumbo kujaa gesi mara kwa mara

3. Huleta hewa safi kinywani. Ni Muhimu sana kwa watu wanaonuka midomo

4. Hukuongezea uchangamfu na kufanya siku yako ianze vizuri sana

5. Husaidia majeraha kupona kwa haraka kutokana na kuwa na ascorbic acid ya kutosha. Pia huimarisha mifupa

6. Husaidia mmeng’enyo wa chakula utakachokula asubuhi au mchana kwa kuondoa vikwazo vyote vinavyoweza kuzuia umeng’enyaji wa chakula.

7. Huimarisha Ngozi yako, kuondoa makunyanzi na kukupa muonekano mzuri.

8. Husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uzito kwani maji moto ya limao huyeyusha mafuta ya kutosha.

9. Huyapa macho yako afya nzuri na kuimarisha kuona.

10. Huondoa hali ya kuhitaji kahawa kila asubuhi ambayo si nzuri kiafya.

MATUMIZI tumia glas moja ya limao asubuhi baada ya kuswaki,au jioni kabla ya kula chochote.

Jumatano, 26 Oktoba 2016

WALIMU NA HARAKATI ZA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA.



WALIMU NA HARAKATI ZA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA.

Harakati za uhuru zimefanyika karibu nchi zote za Afrika,Tanganyika ni moja miongoni mwa nchi zilizotawaliwa na wakoloni wa Kijerumani na baadae wa kiingereza baada ya vita ya kwanza ya dunia.

Kwa miongo kadhaa nchi za Afrika zimekuwa chini ya uatawala wa kikoloni.Kipindi hiki cha Ukoloni kilikuwa kipindi kigumu sana kwa Waafrika kilichohusisha adha za kila aina.

Kwa Waafrika hawakupendezwa na ujio wa wakoloni,Hivyo toka awali Wafrika walianza kuonyesha hasira zao dhidi ya wavamizi katika ardhi yao tukufu.

Baada ya kipindi kirefu cha mateso na taabu kwenye kipindi cha ukoloni ndipo walipoibuka wanaharakati mbali mbali wa kupigani uhuru.

Harakati za kupigania uhuru zilianza tangu pale tu wakoloni walipoingia ingawaje harakati hizo za awali hazikuratibiwa kwa uzuri,pia hazikuongozwa na wasomi na nyingi ya harakati hizo zilifanywa kikabila Zaidi kuliko kitaifa.

Baada ya vita ya kwanza ya dunia harakati madhubuti za kupigania uhuru zilianza na baada ya vita ya pili ya dunia harakati hizi zilipamba moto safari hii zikiongozwa na wasomi pamoja na wazalendo waliotoka kupigana vita vya kwanza na vita vya pili vya dunia.

Wasomi wa kada mbali mbali walishiriki harakati za ukombozi wa Tangayika lakini Makala hii imejikita kwenye mchango wa walimu katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Walimu ni watu ambao wanakutana na watu wengi kwa wakati mmoja na hupata muda mwingi wa kuzungumza nao hivyo huweza tumia nafasi hiyo kupandikiza kile ambacho mwalimu anakiamini.

Mbali na vipawa vya kuzaliwa navyo lakini walimu wamejifunza saikolojia za watu hivyo hutumia nyenzo hiyo kama sehemu ya ushawishi na kukamilisha lile ambalo mwalimu anataka liwafikie watu,mfano kwenye filamu ya Sarafina Mwalimu Mary Masombuko alikuwa mwalimu mwenye ushawishi mkubwa na kufanikmiwa kupandikiza hisia za kizalendo kwa watoto wa kiafrika.

Katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika safari inaanza na Mwalimu Cecil Matola ambaye alikuwa mmoja ya waanzilishi wa African Association katika miaka ya 1927 pia vitabu vingine vimeandika 1929.Mwalimu Cecil Matola alipata braka zote za aliyekuwa gavana wa Uingereza kwa kipindi kile Sir David Cameroon.TAA iliundwa na watu 9 akiwemo Mwalimu Cecil Matola,Kleist Sykes,Mzee Bin Sud,Ibrahim Hamisi,Zibe Kidasi,Ali Said Mpima,Suleiman Majisu,Raikes Kusi na Rawson Watts.Mwalimu Cecil Matola mabaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa African Association alifariki dunia mwaka 1933 na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa katibu wake Ndugu Kleist Sykes.

Mwlimu James Aggrey ,Huyu ni mgana ambaye alikuatana na Kleist Sykes wakati huo Kleist Sykes ametoka vitani na akawa anafanya kazi Tanganyika Railways.Dr James Aggrey inasemekana ndiye aliyemuamasisha Kleist Sykes kwenda kuanzisha African Association ambayo baadae ikawa TAA kisha TANU.

Mwalimu Thomas Sauti Plantan,Huyu atakumbukwa kwa nafasi yake ya uraisi wa TAA miaka 1950s,katibu wake akiwa Mzee Clement Mohammed Mtamila walikumbana na mtihani wa kupinduliwa kwenye uongozi na vijana.Baada ya kupinduliwa kwenye madaraka Dr Vedasto Kyaruzi akawa rais wa TAA na Abdulwahiid Sykes mtoto wa Kleist Sykes akawa ndio katibu wake.

Mwalimu Kahere wa Tanga,Huyu atakumbukwa katika mchakato wa safari ya mwalimu Nyerere ya mwaka 1955 kwenda UNO Kwa ajili ya kudai Uhuru.Itakumbuka kuwa nauli ya kwenda Marekani wakati ule ilikuwa shilingi 12,000.Watu mbali mbali walichangia nauli pamoja na maradhi ya Mwalimu Nyerere kwa ajili ya kwenda UNO. Lakini pesa hazikutosha na ndipo Mwalimu Kahere wa Tanga alipowaambia viongozi wa TANU waende Tanga kuchukua pesa.Special branch(usalama wa taifa wa zama za mkoloni) walitaka kuzuia upatikani wa pesa hizo lakini walishindwa na hatimaye Idd Faizi Mafongo alifanikiwa kuzikabdidhi pesa kwa viongozi wa TANU na hatimaye Mwalimu Nyerere akaenda UNO tarehe 05/03/1955 ingawaje habari hii inapingana na anachoeleza Yericko Nyerere kwenye kitabu chake cha Ujasusi wa Kidola(2016) kwamba kwamba kanisa katoliki lililipia nauli ya tiketi ya ndege kwa kwenda na kurudi.

Mwalimu Kambarage Julius Nyerere,huyu ndio shujaa wa mwisho kwa walimu ambaye alifunga safari ya kwenda Umoja wa mataifa kwenda kudai uhuru wa Tanganyika na kwa jitihada zake huku akishirikiana na viongozi wengine wa TANU uhuru wa Tanganyika ulipatikana tarehe 9/12/1961.

Mwalimu Nyerere amefanya mambo mengi kutoka uhuru mpaka kifo chake kilichotokea tarehe 14/10/1999 katika hospitali St. Thomas huko nchini Uingereza.

Hivyo leo katika kumbukumbu ya kifo cha mwalimu Nyerere na pia tunawakumbuka wazalendo wengine ambao kwa namana moja au nyingine walifanikisha upatikanaji wa uhuru wa Tanganyika ingawaje wamesahaulika kwenye vitabu vyetu(kiada na ziada) vya kuwafundishia watoto mashuleni.

Makala hii imeandikwa kwa rejea za kitabu kiitwacho Maisha ya Abdulwahiid Sykes,Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi,ripoti ya Tadasu TSURUTA na mtandao wa wikipedia

JIFUNZE ASILI YA WACHAGA NA DESTURI YAO

WACHAGA ni kabila la kibantu linalopatikana Kaskazini mwa Tanzania katika mkoa wa Kilimanjaro.

Wachaga wanajishughulisha na kilimo cha viazi, ndizi na mtama. Zao la kahawa lilianzishwa na wakoloni karne ya 19 na kuendelezwa hadi leo kama zao la biashara. Pia wachagga hujihusisha na ufugaji wa ng'ombe, mbuzi na kondoo ili kupata samadi ya kurutubisha mashamba, nyama, maziwa.

Miaka ya nyuma ufugaji wa mbuzi au kondoo ulikuwa wa lazima ili kupata wanyama wa kutambika. Ilikuwa ni mwiko kutambika kwa kutumia mnyama wa kununua au kutoka nyumba nyingine. Kutokana na uhaba wa ardhi katika makao yao ya asili, Wachaga wametawanyika sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi wakijishughulisha na kazi mbalimbali ili kupambana na umasikini.

Ingawa baadhi ya hadithi za kale zinaeleza kuwa Wachaga walikuwepo eneo la Kilimanjaro na dua zao ndizo zilizorefusha mlima Kilimanjaro ili waweze kuwa karibu na Mungu, utafiti unaonesha kuwa Wachaga ni wahamiaji waliofika Kilimanjaro miaka 600 kabla ya ujio wa Kristo. Hivi sasa ni zaidi ya miaka 2000 baada ya Kristo.

Tafiti kuhusu makabila zinasema endapo Wachaga wataamua kutafuta asili yao kwa kuzingatia kizazi cha kale ni lazima wabishe hodi kwenye jamii za makabila mbalimbali hasa kwa Wakamba, Wamaasai na Wataita nchini Kenya, pia kwa Wapare, Wasambaa nchini Tanzania.

Tofauti na makabila mengine ambayo asili yao inatokana na kizazi kimoja, Wachaga wanaweza kujua asili ya kizazi chao kwa kufuatilia historia ya ukoo au historia ya makundi kulingana na eneo. Historia ya kale inasema kuwa jamii ya wachaga inatokana na watu wa makabila mbalimbali ambao walihamia kwenye mteremko wa mlima Kilimanjaro baada ya kukimbia vita na wengine kukimbia baa la njaa.

Pia wapo waliohamia eneo hilo baada ya kuvutiwa na ardhi yenye rutuba na hali nzuri ya hewa na inasemekana kuwa wahamiaji hao waliwazidi nguvu wenyeji wa eneo hilo ambao walijulikana kama Koningo au Konyingo. Baadhi ya wenyeji walihama ila inasemekana kuwa wengine walibaki na kujumuika na wahamiaji na baada ya kuishi pamoja kwa muda mrefu waliunda kabila jipya la wachaga.

Ingawa hakuna ushahidi wa kisayansi kuwa Wachaga walitokana na makabila mengine, simulizi za kale na mfumo wao wa maisha unadhihirisha kuwa hawatokani na kizazi kimoja wala wazee na viongozi wao hawajawahi kuwa na uhusiano wa karibu.

Ingawa watu hao huitwa wachaga wenyewe ni vigumu kujua nani hasa ni Mchaga kwa kuwa wenyeji hutambuana kwa kutumia lugha ya eneo husika kama vile
Mrombo,
Mmachame,
Muuru,
Mkibosho au Muanjo akimaanisha mchaga wa Marangu. Uongozi wa jamii ya Wachaga ulitumia mfumo wa machifu, maarufu kama Mangi.

Kila eneo lilikuwa na mangi wake, ila Mangi Sina wa Kibosho, Rindi wa Moshi na Marealle wa Marangu walipata umaarufu mkubwa, kutokana na jitihada zao za kutaka kuwa wafalme ili kutawala himaya nzima ya wachaga. Hata hivyo, jitihada hizo ziligonga mwamba kwa kuwa hakuna Mangi aliyekuwa tayari kutawaliwa na kiongozi kutoka kundi jingine.

Hali ya kujihami na kuogopana inachukuliwa kama kielelezo kuwa chimbuko la wachaga linatokana na jamii za makabila tofauti yenye historia tofauti.

Mfumo wa uongozi miongoni mwa wachaga umeathiri kizazi kipya kwa kuwa uzoefu unaonesha kuwa wachaga ni miongoni mwa jamii chache zinazopenda siasa za upinzani na hupenda kuchagua kiongozi kwa kupima uwezo wa mtu badala ya chama.

Kati ya mwaka 1750 na mwaka 1890 Wachaga walikuwa na vita vya mara kwa mara, ambapo kila Mangi alitaka kutwaa eneo la mwenzake ili kuongeza ukubwa wa ardhi na kuimarisha ngome yake kiuchumi.

Hadi Mwanzoni mwa Karne ya 19 , wachaga waligawanyika katika makundi 30 na kila kundi lilikuwa na Mangi wake na walijitegemea mithili ya nchi 30 katika kisiwa kidogo chenye udongo wenye rutuba, hali ya hewa safi na chemchemi za maji kila baada ya hatua chache.

Wachaga walikuwa na bendera yao na siku maalumu ya mapumziko, maarufu kama Siku ya Wachaga, ambapo watu walikutana kwa ajili ya kula na kucheza pamoja ili kuimarisha mshikamano upendo na mshikamano. Makundi hayo yalizungumza lugha tofauti na lahaja tofauti, kulingana na jiografia ya eneo husika.

Watu hao waliwindana kila mmoja akimnyooshea mwenzake kidole kwa uchokozi na tamaa ya kutwaa mali na ardhi ya kundi jingine. Vita vya wachaga viliimarika baada ya kuingia kwa Wamisionari, ambao walifika Kilimanjaro na kueneza dini ya Kikristo pamoja na kuanzisha zao la kahawa.

Hivyo, machifu waliweka silaha chini na kuelekeza nguvu zao kwenye kilimo cha kahawa. Wakoloni walifurahi hali ya utengano miongoni mwa Wachaga hivyo walitumia fursa hiyo kuwalaghai machifu ili waweze kupata ardhi kubwa na rasilimali nyingi. Kila chifu alijitahidi kuwakarimu wageni ili aweze kupata msaada wa kujiimarisha kiuchumi na kisiasa.

Kwa mujibu wa historia ya Wachaga, iliyoandikwa na Stanl Kathleem mwaka 1962, kabila hilo lilikuwa na viongozi wengi, ila wachache walipata umaarufu kutokana na aina ya uongozi wao.

Mwaka 1800 chifu aliyejulikana kama Mangi Horombo kutoka Mashariki mwa mlima Kilimanjaro, alikuwa na nguvu zaidi na aliweza kutwaa maeneo yaliyokuwa na wachaga wasiokuwa na nguvu kiuchumi wala kisiasa.

Hata hivyo baada ya kifo cha Horombo himaya yake iligawanyika na kuunda vikundi vidogo vinavyojitegemea. Wakati Muingereza wa kwanza, Johannes Rebmann, alipofika Kilimanjaro mwaka 1848 alikuta mangi wa Machame na Mangi wa Kilema wakiwa na nguvu kubwa kisiasa na kiuchumi, lakini alififia kutokana na sababu mbalimbali.

Kathleem anasema Mangi Oromba alikuwa kiongozi jasiri katika eneo la Mashariki mwa Mlima Kilimanjaro na aliogopwa na watu wake kwa kuwa alikuwa mtu mwenye msimamo. Kiongozi huyo aliishi eneo ambalo hivi sasa linafahamika kama wilaya ya Rombo. Alikuwa Mangi wa kwanza kuanzisha wazo la kujenga himaya ya Wachaga.

Alijenga ngome yake katika kijiji cha Keni na kuunja jeshi, ambalo lilivamia himaya za machifu wengine na kufanikiwa kuteka eneo la Vunjo hadi mto Nanga. Hata hivyo, baada ya kifo chake himaya yake iligawanyika na kurudi katika vikundi vidogo vidogo kwa kizingatia asili na chimbuko la kila kikundi.

Mangi Sina alikuwa jasiri kama Orombo na aliyongoza himaya ili- yokuwa Magharibi mwa mlima Kilimanjaro hadi mpakani kwenye mto Nanga. Alijenga ngome yake katika eneo la Kibosho, ila alitawala hadi eneo la Marangu na Uru. Mwaka 1870 alijenga mji wa kibiashara kati ya Waafrika na Waarabu, ambapo waarabu walimpa nguo na silaha kisha akatoa pembe za ndovu vitu vingine vya thamani.

Utawala wa Mangi Sina ulififia mwaka 1891 wakati waingereza walipoamua kumuongezea nguvu Mangi Rindi wa Moshi, kisha kumtumia kudidimiza utawala wa Mangi Sina. Mangi Rindi ambaye alijulikana kwa jina la Mandara, alikuwa kiongozi wa Moshi mwaka 1860. Alikuwa miongoni mwa viongozi waliokuwa na ndoto ya kutawala eneo lote la Kilimanjaro.

Ili kufanikisha mikakati yake aliungana na viongozi wa kabila la Arusha eneo la mlima Meru na waswahili kutoka Pwani, kisha kusaini mkataba wa Wajerumani kwa lengo la kuiweka Kilimanjaro chini ya Utawala wa kijerumani katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Mwaka 1891 alifanikiwa kuhifadhi ngome ya kijeshi ya Wajerumani kwa ajili ya kusambaratisha utawala wa Mangi Sina wa Kibosho. Uhusiano wa Mangi Rindi na Wajerumani, uliwezesha Moshi kuwa makao makuu ya mkoa wa Kilimanjaro hadi mwaka 1919 wakati makao ya mji huo yalipohamishiwa eneo la kudumu ulipo mji wa Moshi hivi sasa.

Mangi Marealle wa Marangu alisimikwa na Mangi Sina mwaka 1880 wakati eneo la Marangu lilipokuwa sehemu ya himaya ya Kibosho.

Mangi Marialle wa kwanza alikuwa kijana mwerevu na mwenye shauku ya kuwa kiongozi bora kuliko waliomtangulia Kwa kuwa Mangi Marealle hakuwa mtu wa kutumia mitutu, aliamua kujifunza lugha ya kigeni ili kuweza kuwasiliana moja kwa moja na viongozi wa Kiarabu na wakoloni wa Kiingereza na kuwaalika kuwekeza katika eneo la Marangu.

Pia, alijaribu kujenga urafiki na uongozi wa utawala wa Kijerumani na inadaiwa inadaiwa kuwa 1890 Mangi Marealle alifanikiwa kushawishi uongozi wa jeshi la Kijerumani, kuamini kuwa kuwa watu wa kibosho na Moshi walikuwa na njama ya kuangusha kutawala wa Kijerumani, jambo ambalo lilisababisha machifu wa Kibosho na Moshi kunyongwa na utawala wa Kijerumani.

Himaya ya Watu wa Machame ilijengwa na Mangi Abdiel Shangali, ambaye aliingia madarakani mwaka 1923 na kuongoza mfululizo hadi mwaka 1946 alipopandishwa cheo na kuwa chifu wa jimbo la Hai, kwa kujumuisha eneo la Machame na kibosho.

Mangi Shangali alitawala kipindi cha amani, hivyo alifanikiwa kubadilisha mfumo wa uongozi kutoka utawala wa kichifu wa kuridhishana hadi utawala wa mfumo wa kisasa kwa kuchagua viongozi kwa njia ya demokrasia.

Hata hivyo, wachaga hawakuacha kuzozana kuhusu uhaba wa ardhi na hali hiyo iliendelea hadi Tanganyika ilipopata uhuru na kufunja mfumo wa utawala kitemi na kuunda serikali ya umoja wa Kitaifa. Baada ya Uhuru wachaga waliendelea kukodoleana macho kila kundi likitamani ardhi ya kundi jingine.

Hata hivyo Rais Nyerere alifanikiwa kumaliza tatizo hilo kwa kuwahimiza wachagga watawanyike na kushika ardhi katika maeneo mengine katika ardhi ya Tanzania badala ya kung'an'gania ardhi ndogo katika mteremko wa mlima Kilimanjaro.

Hali hiyo iliwafanya Wachaga kuamua kuwekeza katika elimu ili kuwawezesha watoto wao kujenga uwezo wa kujitegemea na kwenda kutafuta maisha sehemu nyingine. Hali hiyo imewawesha wachagga kutawanyika sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi kujitafutia maisha kwa kushiriki katika nyanja mbalimbali hasa katika uongozi wa mashirika, ualimu na biashara.

Watafiti wa masuala la kisiasa wanasema mfumo wa maisha ya Wachaga, umesababisha watu wa kabila hilo kuwa washabiki wa siasa zenye upinzani kutokana na tabia yao ya kujihami kisiasa.

Ingawa viongozi kadhaa wa juu wa vyama vya upinzani wanatoka mkoa wa Kilimanjaro, inaelezwa kuwa ni vigumu viongozi hao kuunganisha vyama vyao na kuunda chama kimoja chenye nguvu, kutokana na ukweli kuwa hata Machifu wa zama za kale, walishindwa kuungana na kuchagua mtawala mmoja.

NB:Kama ilivyo kwa Watanzania wengine, Wachaga wanapokuwa katika mikoa au nchi tofauti, husahau tofauti zao za nyumbani na kushirikiana kama ndugu wa mama mmoja. Hali hiyo imewezesha wachagga kuishi popote na kushirikiana na watu wa makabila mengine bila kusahau utamaduni wa kwenda kwao angalau mara moja kila mwaka.

Naamini umejifunza kitu kipya ama umeongeze ufahamu kuhusu wachaga

JIFUNZE KUWEKA AKIBA KWA FAIDA YA MAISHA YA MBELENI

Mtu kuweka akiba, ni muhimu sana kama vile ilivyo kwa taifa. Saikolojia ya matumizi ya fedha inaonyesha kuwa mtu hupenda kutumia sasa kuliko kusubiri baadaye ambapo ingeongeza faida na thamani zaidi.

Fedha ni kitu ambacho kipo tu kwa muda kama mtu aliyekuwa nayo sasa akishindwa kuidhibiti leo, kesho hatakuwa nayo. Suala mtambuka hapa ni je, kwa nini niweke akiba au niwekeze kwa jambo lingine?

Ningependa nizungumzie juu ya njia mbalimbali za kuweka akiba ambapo zikitumika zinaweza kukuletea faida kwa karne hii, japo kiuhalisia kwa Waafrika kuweka fedha ni tatizo sugu kwa walio wengi. Hali kama hii inatokana na uwezo mdogo wa kudhibiti fedha kwa mitindo ya kisasa na kibiashara pia. Elimu juu ya jambo hili haijafika au haijakaa vizuri katika upande wa ubongo iliyo wazi kwa mazingira ya hapa nchini.

Zipo njia ambazo ni nzuri zikitumika kwa kuweka akiba kwa faida zitaongeza maendeleo ya wengi. Njia hizo ni:

1», ni kununua fedha za kigeni. Mara nyingi fedha za kigeni mfano Dola za Marekani, Euro, Pound ya Uingereza na fedha kutoka Bara la Asia kama vile za Saudi Arabia, huwa zinapanda thamani ukilinganisha na za Tanzania.

Mfano, ulinunua Dola moja ya Marekani Novemba, mwaka jana kwa Sh1,300. Mwaka huu unaiuza kwa Sh2,100. Ukipiga hesabu umepata faida ya Sh800. Kama ulinunua Dola 10,000, leo hii ikiziuza una faida ya Sh1 milioni, na kadhalika.

Mtindo wa kununua dola kwanza unapunguza kubeba lundo la fedha nyingi, inakuzuia kuitumia bila sababu, hivyo kuendelea kuwa akiba, kukulinda na kukuwezesha uwe na faida pale mfumuko wa bei unapoongezeka na inaweza kukusaidia iwapo itakulazimu usafiri nje ya nchi. Ukisafiri nje ya nchi itakufanya usitumie fedha nyingi za kununua za kigeni kwa gharama kubwa.

2», ni simu benki. Huu ni mfumo ambao upo sana siku hizi eneo la Afrika Mashariki. Siku hizi kampuni za simu zimewezesha mtu kuweka akiba.

Huduma imeboreshwa zaidi kwa kuweza kuzihamishia kwenye akaunti za benki, kulipia huduma na bidhaa au kuzitoa katika nchi nyingine kulingana na aina ya fedha za eneo husika.

Hii inamuwezesha hata kama mtu akiwa mbali na benki na kuwa na uwezo wa kuokoa muda kwa kutumia pesa alizoweka kwenye simu yake kwa kuzitoa kwa wakala aliye karibu naye.

Vilevile, kwa kutumia simu waweza kuvuta fedha kutoka kwenye akaunti yako ya benki na kuziingiza kwenye simu yako na kuwa huru kuzitoa ili kuzitumia eneo lolote kwa kutumia mawakala.

Siku hizi pia kwa kutumia akiba kwenye simu unaweza kupata huduma nyingine kupitia simu hiyo kama vile kununua umeme, kulipia bili ya maji, matibabu, king’amuzi na hata tiketi za kuingia kwenye michezo ya soka au tamasha. Mtu aweza kudunduliza fedha kidogokidogo kwenye simu yake.

3» kuweka akiba kwa kutumia benki na taasisi nyingine za kifedha. Hii husaidia sana kuhamasisha huduma za kuweka akiba kwa malengo kama vile kumsomesha mtoto au amana.

Uwekaji wa fedha za namna hiyo pia huweza kusaidia kuwa na fedha za kukabili dharura na kuwa na mitaji mikubwa ya kibiashara na hatimaye kuleta maendeleo makubwa yaliyokusudiwa.

4», ni kumkopesha mtu na kurudisha kwa riba. Siku hizi aina hii ya ukopeshaji imeenea sana, hasa mijini na vyuoni. Hii imetokana na watu kuzidi kukua sana kiuelewa, wamebadili mwelekeo kutoka kumkopesha mtu pasipo riba hadi kuwa na faida.

Watu wameerevuka na kufahamu kuwa fedha ya mwezi au wiki hii ni tofauti na ya mwezi au wiki lijalo. Tatizo lililopo ni kwamba hakuna maandishi ya kukopeshana kwa walio wengi kwa sababu za kujali utu. Lakini ukweli ni kwamba wanadamu wengi wana tabia ya kubadilika. Kama huna maandishi ya kukopeshana itakuwa vigumu kupata fedha zako pale anapokuwa si mwaminifu.
5», ni kuwekea bima mali zako na biashara yako. Hii ni njia ambayo ni muhimu sana maana hakuna mtu anayeweza kuzuia majanga ambayo ni ya asili au ya kawaida, hivyo bima hasaidia sana siku ukipata ajali ya biashara kwa kuibiwa au kuungua.

6», ni kununua vitu kama nyumba, ardhi na vifaa vya gharama vyenye kudumu muda mrefu. Hivi waweza kuviuza baadaye kwa bei ya juu.

NB.
Maendeleo ya mtu mmojammoja ni mafanikio ya taifa.
Taifa lenye akiba ya kutosha kwa kawaida linakuwa imara na wananchi wenye akiba kwa njia mbalimbali kama nilivyoorodhesha, ni watu wenye maisha ya uhakika. Dharura zote wanaweza kuzikabili na hapa ndipo pia mitaji mikubwa ya biashara inatokea. Kuweka akiba ni jambo la msingi.

ASANTENI

Jumanne, 25 Oktoba 2016

MAMBO YA KUFANYA ILI FIKRA ZAKO ZITUMIKE KUFANIKISHA MAISHA YAKO


MWL: C. MWAKASEGE

AWAMU YA PILI

SOMO:5

MAMBO YA KUFANYA ILI FIKRA ZAKO ZITUMIKE KUFANIKISHA MAISHA YAKO

▶Lengo
Kuweka maarifa ya Kibiblia ndani yako yatakayokuwezesha kutumia FIKRA zako ili ufanikiwe ktk maisha yako

*Mith 23:7(a)*

*HATUA AMBAZO UNAHITAJI KUZIFUATA KAMA UNATAKA KUTUMIA FIKRA ZIKUSOGEZE KIMAISHA*

➡Tumeshaangalia hatua 2 tuko tumeanza seminar. Leo tuendelee na ya 3

3⃣Panga FIKRA zako kwa upya ili zisikupitishe tena mahali pabaya ulipokwisha pitia.

✅FIKRA zinapangika
✅Mfano kwa mama mjane baada ya kusaidiwa na Elisha akitaka hali ile ya mwanzo isijirudie tena lazima abadiri kufikiri kwake la sivyo ile hali atarudi tu

*2Falm 5:7*
Mama mjane alipanga FIKRA zake kwa upya..lazima ujifunze kupanga FIKRA zako kwa upya
Tuonaona mstari wa 7

➡...Nenda kauze mafuta...
Si FIKRA tu kutumika bali MUNGU alitaka Mama mjane ajuaje na akubali ndani yake kuwa MUNGU ndiye amfundishaye kupata faida.

*Isy 48:17*
✅MUNGU hakufunsidhi tu kuhubiri au kuimba bali pia hukufundisha na hupanga FIKRA zako ili zipate kujua MUNGU ndiye akupaye faida

✅FIKRA lazima zipate msaada wa kufundishwa jinsi ya kupata faida

✅Pata tofauti sana kati ya kufundishwa kupata faida na kufundishwa Biashara. Ni sawa na ilivyo tofauti kati ya kufundishwa kufaulu mtihani darasani na kufundishwa juu ya kufaulu mtihani wa kimaisha

✅Maana si kila mtu aliyeko darasani atafaulu maisha, na si kila afanyaye Biashara atapata faida..lazima ujifunze kuvuka hapa

*MAENEO MUHIMU YA KUTAKIWA KUBADILIKA*

*1).* Weka FIKRA zako zikubali MUNGU ndiye anayekufundisha kupata faida

▶Watu wengi wakikwama kiroho hukimbilia kanisani ila uchumi wao ukikwama huwaoni kanisani hukimbilia Benki, sasa sisemi Benki ni mbaya au usiende Benki ila wanasahau kuwa

▶ROHO MTAKATIFU ni mwalimu mzuri sana wa kukufundisha ujasiriamali wenye kupata faida

*2).* Lipa Deni
✅Elisha alimwambia Mama mjane ....kauze kisha lipa deni....

✅Alikuwa anatafuta kitu gani?
▶Alikuwa anapandikiza nidhamu za kutumia fedha ambazo MUNGU amempa kwa sababu zake alizokupa au ulizomwomba tena kwa mwongozo wake!

▶Mama mjane alikwenda kutaka msaada wa watoto wake kutokuchukuliwa watumwa(Alitaka kupata fedha za kuwakomboa watoto wake)

▶Hakuwa na FIKRA zilizojengeka kulipa deni maana Biblia haituonyeshi aliwahi kukopa. Kama huna FIKRA za kukopa huwezi ukawa na (nidhamu) FIKRA za kulipa deni.

*Mama mjane alikabidhiwa matumizi ya fedha ktk maeneo haya*
⚫Kulipa deni
⚫Gharama za kwake na zile za baadaye
⚫Gharama za watoto na za wakati ule wa baadaye
⚫Kuhakikisha ya kwamba hamalizi faida lazima abaki na mtaji.

✳Je unamwomba MUNGU pesa kwa ajili ya nini au kwa ajili gani?
▶Kumbuka pesa huyumbisha mawazo na kujikuta watumia nje ya lile kusudio

▶Ukikorofisha hapo MUNGU hukaa pembeni. FIKRA zinahitaji nidhamu kwenye matumizi ya pesa. Kama MUNGU anakupa kwa ajili ya kitu fulani hakikisha unaielekezea hyo pesa kwenye hicho kitu.

▶Tofauti na hapo utaona ROHO MTAKATIFU anakuhimiza TOBA

*Mith 13:22*
▶Watu wengi wana FIKRA za kujitazama wenyewe tu kwenye upande wa pesa wanajikuta kusahau kuwa wana familia na watoto!

▶Biblia inatuhimiza kuweka akiba mpaka za wajukuu!

▶Usitazame kukwama kwa mme/mke wako ama wazazi wako, usifike mahali hata pa kuwakasirikia badili FIKRA zako ili wewe uvuke hapo kisha mrushie kamba naye atoke hapo oooh hallelujah Hallelujah

*HOME WORK*
➡Orodhesha madeni yako

*Zab 37:21*
✳Umuhimu wa kuorodhesha madeni

▶Usipolipa mikopo MUNGU haji kukupigania katika haki zako.
▶Unapoteza haki katika haki
▶Mikopo isiyolipwa ugeuka deni
▶Deni ubeba vitu (rehani) ili akili zako ziamke. Na baada ya kutaka kuja kuvichukua ndipo akili zako zitaamka
▶Si kila ambaye anashindwa kulipa deni hana hela bali hana mpangilio mzuri wa matumizi na ulipaji

*Yer 22:21*
✅Si kwamba hapendi kusikia bali hataki kusikia maana yake hataki kutekeleza alichoambiwa

✅Gharama kubwa ya kutokufaulu mipango yako ni kupoteza utulivu wa MUNGU kukusemesha

✅Wengi wakisha kopa kwenye kulipa hulipa nusu na nusu wanaweka mfukoni wanasahau MUNGU ndiye aliwafundisha kupata faida na au walipewa kibali cha kupata mkopo

✅Usije ukasahau na kusema huu utajiri ni nguvu zangu wakati ni MUNGU ndiye aliyekupa nguvu za kupata utajiri

*UNAFIKIRI KWANINI MUNGU ALILETA SADAKA*
▶Si kwamba ana shida na pesa yako
▶Lengo la kwanza lilikuwa kutumia sadaka kukutengenezea FIKRA sahihi ndani yako
✳Tazama maana ya
⚫Malimbuko=MUNGU anataka umfikirie yeye kwanza
⚫Zaka ya kwanza=MUNGU anataka kupewa heshima ktk maisha yako

✅Watu wengi kwenye kipindi kigumu na chenye kibano wako tayari kutafuta hela kulipa Benki lakini si kwa MUNGU. Kwa MUNGU excuses zitakuwa nyingi sana na hata kusema "MUNGU we si unajua nilivyobanwa"

✅MUNGU hana maana wala hataki kukufirisi bali anataka kukutengenezea FIKRA zenye Nidhamu

✅Jifunze kumpa MUNGU 100% naye anakurudishia 100%

✅Muulize MUNGU kwanza kwenye kila kitu, ratiba zako, muda wako na mambo yako mkabidhi na mfikirie MUNGU kwanza

✅Usitamani kuiga maisha na FIKRA za mtu mwingine hakikisha MUNGU anakupa mbinu za kujenga FIKRA za kwako mwenyewe.

✅FIKRA zenye kujenga nidhamu ndani yako.zitakufanya utende haki wala hazitakupeleka kwenye kupokea rushwa

✅FIKRA hizi zitakuwekea unyenyekevu ndani yako, kujishusha na kujifunza kutoka kwa wengine

✅Usijaribu ku copy na ku paste kutoka kwa mtu mwingine BWANA atakupa mikakati sahihi ndani yako

*MAOMBI*

*..."Jesus Up"...*

*****SIKU YA TANO*****

SOMO:6

NAMNA YA KUFANYA ILI FIKRA ZAKO ZITUMIKE KUFANIKISHA MAISHA YAKO

▶Lengo
Kuweka maarifa ya Kiblia ndani yako yatakayokuwezesha kutumia FIKRA zako ili ufanikiwe ktk maisha yako.

*Mith 23:7(a)*

▶Tunaendelea na *HATUA....*

4⃣Omba MUNGU akusaidie uweze kupata kutoka kwenye vitabu maarifa yanayohitajika ili uhitajike

*Dan 12:4*
✅Tutazame hatua kwa hatua ktk mtirirko ufuatao:-

*1).* Ni vyepesi mtu kuhitajika akiwa na maarifa yanayohitajika ktk kipindi husika

*Dan 1:17-21*
➡Watu hawakuajiri sababu ya Cheti bali ujajiri maarifa uliyonayo

➡Wakikuajiri sababu ya Cheti na kukaa nawe muda wakagundua una Elimu lakini huna maarifa utashushwa cheo

➡Hatuambiwi kina Daniel walikuwa wangapi, ila walisomeshwa na kupimwa ktk mtihani. Kuanza kwako chuo walikuwa tayari na mtaji..swali la kujiuliza kile walichosomea kiliwasaidia kupata maarifa?

*Dan 1:3-4*
➡Walikuwa na Elimu pamoja na maarifa kwa kiwango fulani.

➡Ilibidi wakae darasani miaka 3 wapate maarifa juu ya maarifa. Haijalishi Elimu na maarifa waliyokuwa nayo awali.

*Mwz 41:37-40*
➡Yusufu alipewa nafasi ya Uwaziri Mkuu akiwa jera baada ya kugundua kuwa ana maarifa

➡Haijalishi uko wapi, jera? Umefunikwa? Umefungiwa au wapi lakini ROHO MTAKATIFU ni mwaminifu atakukutanisha tu na kusudi kama una maarifa yanayohitajika

➡Usiende shule au usisome kwa ajili ya kupata.Cheti bali soma ili upate maarifa. Maarifa yatakusaidia kutoka maishani ila si cheti

*2).* Kuna Vitabu vilivyobeba maarifa yanayotakiwa kwa muda husika

*Dan 12:4*
➡Muda ndiyo unaodai aina ya maarifa

➡MUNGU aliumba kwanza nyakati(muda) kisha mtu

*Mwz 1:1*
➡NENO mwanzo=aliumba muda kwanza kisha mbingu na nchi

➡Muda na maarifa zinaenda pamoja

➡Daniel aliambiwa yatie muhuri= Mtu yeyote akisoma asipate maarifa yaliyomo ndani yake kwa sasa mpaka kwa muda ulioamriwa. Hata yeye kwa kipindi kile asingeelewa hata kama angesoma

*Dan 1:4*
➡Mfalme aliagiza wafundishwe Elimu ya wakaldayo maana yake walikuwa tayari na kiwango fulani cha uelewa.

➡Ni sawa na kuchukua mtoto wa darasa la kwanza kumpeleka Chuo Kikuu haiwezekani maana kuna ngazi tofauti tofauti maana *Umri uenda na aina fulani ya kufikiri*

➡Ni hatari sana kusoma na kuwa na Elimu halafu huna lugha ya kutafsiri maarifa hayo(Wasoma kiswahili halafu interview kichina)

➡Kumbuka lugha inakunyima kazi

➡Njia yako uendana na lugha vilevile yaani kuchukua maarifa Ujerumani siri imefichwa kwenye kitabu hicho cha lugha ya kijerumani. Lazima usome mwaka mzima kijerumani kwanza kuweza kutoa maarifa yaliyoko humo.

*Ayb 35:16*, *34:35*
➡Kuna maneno hayana maarifa.
➡Si kila kitabu chenye maarifa chaweza kukusaidia isipokuwa kwa wakati sahihi na muda ulioamriwa!

*3).* Vitabu vilivyobeba maarifa uwa vingine vinafungwa visitoe maarifa hadi muda/wakati wa kuhitajika kutoa maarifa au muda umekaribia au umewadia

*Dan 12:4*
*Dan 9:1-3*
➡Kitabu chochote chenye sababu hii ya (3) lazima ukishakisoma utapata msukumo wa kuyaweka kwenye matendo yale yote uliyoyasoma

➡Nunua Vitabu Chini ya msaada wa ROHO MTAKATIFU, mwombe MUNGU akupe hekima kununua vitabu ambavyo.vina maarifa unayoyahitaji. Hii ni nidhamu unahitaji kujiwekea

➡Kumbuka kitabu chichote kilicho na maarifa ya wakati huo na sahihi kinakupelekea kupata msukumo ndani yako kuweka kwenye matendo hayo uliyosoma na kupata msukumo wa kuyaombea.

*4).* Ni muhimu kwa kitabu kufunguliwa na akili ya msomaji kufunguliwa kwa pamoja ili maarifa yaliyomo ndani ya kitabu yawe msaada ktk muda husika kwa ajili ya msomaji huyo

*Luk 24:44-49*
➡Kitabu kilikuwa kimefunguliwa lakini akili zao zilikuwa zimefungwa

➡Kitabu kilifunguliwa kwa ajili yao na YESU alijua akisema nao waweze kuoanisha kutoka kwenye vitabu vya torati na zaburi ndiyo maana akili zao zilifunguliwa na kufunuliwa wapate kuelewa walichokisema manabii waliotangulia kinatimia sasa

*5).* Mwombe MUNGU akukutanishe na Vitabu vilivyobeba maarifa unayoyahitaji na avifungue kama bado vimefungwa ili upate maarifa unayostahili kama hayo

*Uf 5:1-5*, *10:1-11*
➡Simba wa Yuda (YESU) alipata nafasi ya kukifungua kitabu.

➡Kitabu kinaweza kikawa kimefungwa ukaomba kifunguliwe

➡Pia kinaweza kikawa kimefunguliwa, sasa omba maarifa ukifunguliwa akili uweze kukielewa

➡Tazama Biblia ni kitabu bora na ni ileile inabeba maarifa ya kukusaidia bila kujali muda uliowekwa maana muda ukifika unafunguliwa tu

➡Jiulize ni kwanini watu wengi wanasoma shule lakini si wabunifu? Mfano waliosoma Administration waambie waanzishe ofisi binafsi uone..wanasubiri ku copy na ku paste ila leo MUNGU anakutafuta kukupa maarifa ukagunguliwe akili...oooh hallelujah!

*MAOMBI*
Orodhesha madeni yako maombi yataendelea siku ya 7(leo)

✅Maelfu ya watu walimpokea YESU pia

*..."Jesus Up"...*

*****SIKU YA SITA*****

SOMO:7

NAMNA YA KUFANYA ILI FIKRA ZAKO ZITUMIKE KUFANIKISHA MAISHA YAKO

▶Lengo
Kuweka ndani yako maarifa ya Kiblia yatakayokuwezesha kutumia fikra zako ili ufanikiwe ktk maisha yako

*Mith 23:7(a)*

*Summary*
✅Kubadili maisha yako badili kufikiri kwako
✅Maana ya fikra...rejea day 1
✅Hatua ambazo unahitaji kuzifuata kama unataka kutumia fikra zikusogeze kimaisha..rejea day 1-6
✅Jana tuliangalia mtiririko wa mambo kama 5 hivi, lile la 5 tuliangalia; uhusiano kati ya maneno na Vitabu maana kitabu kimebeba maneno, muda na maarifa *Dan 12:4*
✅Maarifa ndani vitabu uachiliawa kufuata na uhitajika wake kipindi husika
✅Wazo la vitabu lilianzia rohoni si mwilini

..Tuendele na mtiririko huo..

*6).* Zijue njia za kupata maarifa kutoka ndani ya maneno yaliyomo ndani ya kitabu

*Josh 1:8-9*
▶Maneno ya MUNGU alizungumza na Joshua baada ya Musa kufa

▶Alikuwa akimtia moyo kuendelea mbele na watu wake ili kusudi litimie.

▶Joshua alitazama kazi aliyopewa na kuangalia kufanikiwa pamoja na kustawi kwake pamoja na watu wake hakika kwake halikuwa jukumu jepesi ndiyo maana alipewa njia ya kunsaidia...mstari wa 8

▶Aliambiwa chukua kitabu maana humo ndiko kuna maarifa ya kushinda kwako.

▶Maana miaka 400 walikaa bila kuwa na utaratibu wa KIMUNGU, MUNGU baada ya kukumbuka Agano alilofanya na Ibrahim na Yacobo akawatoa utumwani, walipofika Sinai akatengeneza utaratibu ambao utafananafanana na yeye ili kukaa nao. Lilikuwa jambo jipya sana kwako

▶MUNGU akija na kuamua kukaa mazingira take ubadilika kabisa ndo maana akatengeneza kitabu na ndani yake kuna maarifa, kuna masuala ya ujenzi, kilimo, uchumi, mahusiano ya kila aina, kitabu kukusaidia kustawi sana na uweze kuishi pamoja naye

*JOSHUA ALIAMBIWA VITU 3 VYA MUHIMU ILI UWEZE KUTOA MAARIFA NDANI YA KITABU, NA NI KITABU CHOCHOTE KILE*

1⃣Kisiondoke kinywani mwako
✅Jifunze kufikiri kila ambacho unakiona na kukisoma ndani ya kitabu na kutaka kitokee kwako

✅Jifunze kusema kila unachokiamini ndani ya kitabu *Mark 11:23*

✅Yale uliyonayo utegemea sana kile unachosoma na kukisema

*Rum 10:8-10*
✅Ukitaka kupata kilichopo kwenye kitabu lazima ukiri. Ukikuta mtu anapinga kilichopo ndani ya kitabu jua hakitatokea kwake

*Zab 45:1*
✅Ulimi unaandika
✅Kuzungumza ni kuandika kwenye mioyo na vibao vya nyama kwako.

✅Ndiyo maana ni rahisi tukikutazama tukajua nani kaandika ndani yako

✅Unaposema unaandika kwenye nafsi yako
✅Haitoshi kusoma jifunze kusema maana uanzia kuandikwa ndani. Maana sauti ninayoisikia kuongea si sauti ninayoisikia kuongea

2⃣Yatafakari maneno take mchana na usiku
✅Ni zaidi ya kusoma, kukariri
✅Tamka kutoka moyoni. (Meditation)

✅Tafakari=Tafuna
✅Kukariri=Kumeza na hii so guarantee zitafanya kazi

✅Huwezi ukatoa maarifa ndani ya kitabu bila kutafakari= fikra na akili zako kuchanganya ili utakapotembea utakuwa neno linatembea. Maana NENO alifanyika mwili akaa kwetu

✅Kutafakari NENO kuna kupa nafasi ya kutafuna na kupata nafasi ya kuwa na maswali mengi sana utakuwa mtu wa kutembea na note book na kalamu Mara nyingi si Ku copy na kupaste bali utapata maarifa zaidi

3⃣Upate kuangalia na kutenda sawasawa na maneno yaliyoandikwa humo
✅Utendaji unahitaji nidhamu ya kiwango cha juu sana

✅MUNGU anapoachilia wazo la biashara ndani yako usiwe na haraka kushirikisha watu maana kufanya hivyo kesho utamkuta mwenzako katekeleza..unahitaji nidhamu ktk hili

✅Swala si wazo au utekelezaji bali anahitaji kukuweka utaratibu wenye nidhamu kwanza

*Muh 12:9*
Tuongezee jambo jingine
4⃣Tafuta waalimu ambao wanakufundisha upate maarifa si wale watakaokufundisha upate darasa=cheti

✅Hata ktk vyuo vya kuandaa walimu lazima waandaliwe kutoa maarifa ndani ya Vitabu na si tu wawafundishe wanafunzi kunaliza shule

✅Binafsi nitamsikiliza na kumfuatilia mwalimu yule kesho na kesho kutwa kila nikimsikiliza nitapata maarifa=lugha ya mjini ninamwelewa sana

✅Paul alipokuwa na kiu ya kumtumikia MUNGU alipata waalimu walikuwa wanatoa maarifa ya Dini si maarifa ya KRISTO

✅Jiulize kwanza waalimu gani wanakufundisha? Unapeleka watoto shule jiulize ina walimu wa namna gani

*7).* Uwe mwangalifu na Vitabu unavyosoma

✅Si kila Vitabu vina uwezo wa kutoa maarifa
✅Kuna vingine haviendani na njozi yako. Hivyo usipoteze muda mwingi kusoma visivyo vya kwako maana muda hautoshi na huna muda wote ukifikiri ni wa kusoma

*Muh 12:12*
✅Vutabu ukisoma vinakuchosha
✅Usijaribukushindana na watunzi wa Vitabu ktk kusoma maana utakufa na wataendelea kutunga tu

✅Pia kuwa mawangalifu sana na Vitabu vya hadithi maana hutoa maarifa ndani ya mtu na pia utoa maarifa kwa njia ya hadithi *1Tim 1:3-4*

*Matendo 19:19*
✅Vilichomwa Vitabu hivyo maana maarifa yake yalikuwa hayatakiwi

✅Kama Vitabu vimepitwa na wakati wasomaji wakisoma fikra zao urudishwa nyuma ila vipo vile Vya zamani ambavyo maarifa yake ni ya mbele

*8).* Jizoeze kwa maombi kunyunyizia DAMU YA YESU juu ya kitabu unachosoma

*Ebr 9:19-22*
✅Maana si kila kitu unachosema kitakuzalishia jambo ulitakalo

*Ayb 38:2*
✅Maneno yasiyokuwa na maarifa uachilia giza

✅Mfano angalia ukitaka kusoma Biblia sekunde chake umechoka, umelala, uelewi lakini tazama ukitaka kusoma msg kwenye Simu au gazeti, waweza soma msg zote na magroup yote bila kuchoka na kuwa active zaidi

✅Ukigundua hili unajua ni vita na DAWA YAKE NI DAMU YA YESU PEKEE

✅Kabla ya kusoma achilia DAMU ya YESU kuondoa Giza na kufunga fikra usielewe

✅Jifunze kuombea miguu ya waalimu
✅Jifunze kuombea eneo unalopatia elimu. Mussa aliambiwa vua viatu

✅Kuna uhusiano mkubwa kati ya miguu na sikio na kichwa pia

✅Hatua unazokanyaga na jinsi unavyofikiri kuna uhusiano mkubwa sana

✅Miguu lazima ifungwe utayari maana waweza pata maarifa halafu ukapata uzito kutekeleza.

✅Shetani akiweza kukubana kwenye miguu yako na masikio yako huwezi kufanikiwa hata kidogo.

✅Jiulize Mara ya mwisho kusoma Biblia tena unayo kwenye Simu yako ni lini? Ila Mara ya mwisho kusoma msgs ndani ya Simu ni lini?

*MAOMBI*
✳Masikio yako vs Simu yako

*..."Jesus Up"...*

*****SIKU YA SABA*****

SOMO 8

NAMNA YA KUFANYA ILI FIKRA ZAKO ZIFANIKISHE MAISHA YAKO*

Tumekuwa na semina nzuri sana na kama ni siku yako ya kwanza tafuta kanda.  Na somo hili hapa ndio nilikuwa naanza tu kwenda ndani kwa hiyo omba kwa Mungu ili atupe tena nafasi nyingine maana somo bado linaendelea.Pia ombea na kamati maana muda wetu wa kufanya semina hapa Dar es Salaam ni kipindi cha mvua hasa ile semina ya Kwanza kwa hiyo omba tupate muda mwingine au kiwanja kingine.

Tumesoma neno kutoka Mithali 23:7a   Maana aonavyo mtu nafsini mwake. Na tumeangalia tafsiri mbali mbali, moja inasema atafsirivyo, na nyingine imesema anavyotafakari . na pia ukisoma Zaidi ndipo utajua na tafsiri zingine nyingi. 

Na nilikuambia kuwa  *Fikra ni mkusanyiko au mtirirko wa mawazo yanayotengeneza msimamo wa kiutekelezaji ndani ya mtu* na Fikra zina tafsiri mbali mbali. Kwenye siasa/ Uchumi tunaweza sema ni *sera* na kwenye makabila tunaweza sema ni mila.

*Hatua ya Tano*.  *```Jizoeze kijiuliza maswali yanayofanya Fikra zako zifikiri kiubunifu```*

*1* *Jifunze kufikiri juu ya soko kwanza kabla kitu unachofikiri kuuza*

Tafuta soko kwanza hata kama, yaani demand ya kitu chako kwa sababu biblia inasema *anatanga mwisho tangu mwanzo*. Start with end in mind. Usianze kulima shamba lako kama hujui unalima kwa ajili ya nini yaani unalima kwa ajili ya chakula au kwa ajili ya biashara. Na kama hujajibu swali hili kuwa unalima kwa ajili ya nini ujue tayari umefeli.

*MFANO* Kuna wakati nilitaka kulima maparachichi kwenye shamba ambalo baba alituachia urithi. Na nilitafuta watu wanaotaka tulime kwa mkataba yaani tukivuna wao ndio wananunua  na alikuwepo mzungu mmoja ananunua hayo maparachichi. Nilitafuta mawasiano yake nikayapata na  nikaongea nae ila sikupata majibu sahihi kwa hiyo nikaamua kumfuata kule kule aliko.  Na Nilikuwa na maswali ambayo nataka kujua kwa sababu ukilima maparachichi baada ya miaka miwili unavuna na uzalishaji wa mti ulioupanda unaanza kupungua mwaka wa sita. Yaani baada ya miaka sita uzalishaji unashuka.  Na kuanza hicho kilimo ilikuwa inahitaji hela nyingi kidogo, ili kuwekeza. Na kwa kuwa kuuza kutaanza baada ya mwaka wa tatu kwa hiyo nikamuuliza baada ya mwaka wa tatu (yaani tokea ukipanda itakuwa imepita miaka 3 hadi unaanza kuvuna)  bei yake itakuwa sh ngapi? Akasema hajui sasa nikamauuliza tena je wewe utakuwa unauza wapi? Akasema Uingereza, sasa nikamauuliza kama wewe utakuwa unauza uingereza basi ni kuwa lazima umepiga hesabu za bei na ndio maana umekuza kuwekeza huku kununua maparachchi.

Na hakupenda sana maswali yangu maana hakutegemea kama kuna mtu atamuuliza maswali kama yale kwa sababu walikuwepo wengine wanalima tu kwa kuwa wamesikia mzungu ananunua. Na mimi nilimwambia kuwa *nahitaji kupiga mahesabu* kwa sababu hata kama nataka nikakope benki lazima wajue kuwa je huu mradi ninaoutaka kufanya je utakuwa na faida? Na je utaweza kuerejesha mkopo wao na je mimi mwenyewe ntapata faida?

Mradi wowote hata kama unaweka pesa za kwako jaribu kupiga mahesabu na jaribu kuwauliza na watu wa benki kama wanaweza toa mkopo kwenye aina hiyo ya mradi? Kwa sababu benki huwa wanaangalia kama huo mradi unaweza rudisha hizo hela zao unazotaka kukopa.  Na ukiona benki wanakaa basi ujue kuwa mahali hapo ni hatari kuwekeza kwa lugha ya kitalaamu tunaita *risk*  na hata kama unalipa vipi uwe makini nao sana au acha usiweke hela yako hapo maana inaweza ipotee.

Kwa hiyo nikaenda kuwauliza Wafanyakazi wake na wao pia waliweza kujibu kwa sehemu basi, nikaa chini nikapiga mahesabu na nikagundua baada ya mwaka ya 5 ndio naweza pata faida ya laki 7 (700,000) yaani hiyo ndiyo faida na wakati uwekezaji wake umenigharimu mamilioni ya pesa. Kwa hiyo nikamwambia yule mzungu kuwa siwezi kulima kwa sababu kama nalima kwa ajili ya biashara nahitaji faida na kama maparachichi ya kula ntanunua sokoni.  Kwa hiyo *Fikiri kwanza soko kwa sababu ile chupa ya mafuta ingekuwa haina thamani kama hamna soko*

*2* *Zizoeze fikra zako kufikiri kiubunifu*

Fikra za aina hiyo ndizo zinaoleta viwanda, kwa sababu viwanda vinakuja kwa njia ya ubunifu.  Na kasome uingereza , Ujerumani na Afrika ya Kusini.  Utajua hiki nianchokummbia,

*3*  *Tafuta kujua mahitaji ya muda*

Biblia siku  ilitoa kabisa mwongozo kuwa maarifa siku za mwisho yatakuwa mengi sana na yatenda kwa spidi sana. Kwa hiyo ukijua mahitaji muda husika iatkusaidia sana, Kwa mfano, Mwanvuli ni kwa ajili ya kipindi cha mvua na ukitumika kipindi cha kiangazi utatumika kwa kazi zingine kabisa.

Tulikuwa na mkutano mmoja huko marekani na moyor wa lile jiji alitangaza kuwa kutakuwa na barafu *Storm* na hali ya hewa ingebadilika sana na nikawa natazama kwenye television wakawa wanatabiri kuwa hata safari za ndege zataahirishwa na hata wanafunzi walitangaziwa kuwa hakuna kwenda shule kwa sababu ya barafu itakayoshuka.   Na sisi ilikuwa inatakiwa tuondoke siku hiyo. Basi nikaingia kwenye maombi kama masaa mawili hivi ili kusemesha mbingu za mahali pale ili kuzuia hiyo barafu na niweze kuondoka na ndege yetu pia iweze kuwepo yaani *flight isiwe cancelled* yaani iahirishwe. 

Walifanya kila maandalizi na magari yaliliyokuwa na chumvi tayari kwa ajili ya kuyeyusha barafu huko barabarani na pia hata magari ya kwenda airport  ilikuwa ni tabu sana kwa sababu walishatangaziwa kuwa watu wabaki nyumbani kwao . Basi tulifanikiwa kutoka na tukaenda airport na tuliikuta ndege yetu ipo na safari za ndege zingine ziliahirishwa.

Na tulikopokuwa tunatazama television tena na zile saa walizotabiri kutokea kwa hizo storm  hazikutokea na walishindwa kutoa sababu, na tuliwaambia watu wawili tu wa ule mji. Na baada ya sisi kuaondoka ilishuka storm kubwa sana.  Hawakujua kuwa ni sisi ndio tulibadilisha hali ya hewa ya mahali pale.

Na tulipoondoka rafiki yetu mmoja alituambia kuwa ile chumvi yote imeharibika kwa sababu chumvi iliandaliwa kwa masaa  na haikuandaliwa kwa ajili ya chakula. Na ndio maana iliharibika . ndio  maana nakuambia kuwa *zizoeze fikra zako kufikiria mahitaji ya muda*

*1* *Ukisikia malalamiko popote   usizizoeze fikra zako kulalamika, Bali fikra zako zijue kujibu juu ya
~~ *nani analalamika*
~~ *Kwanini analalamika*
~~ *Anamlalamikia nani*
~~ * Muda gani analalamika*
~~ *Malalamiko yake huwa yanajirudia kipindi gani*

>>Hata kama ni halali kiasi gani, wakati wenzio wanalalamika chukua fikra zako kufanya utafiti  na ujue ni akina nani wanalalamika, kwanini, lini na wanamlalamikia nani.
*MFANO*  Hesabu 13-14
Habari za wapelelezi, ambao walitumwa kwenda kuipeleleza nchi ya Kanani na walitumwa kwa sababu za kiuchumi kabisa kwa sababu hawakutumwa habari za kiroho kujua wale watu wanasali wapi au la.
*SABABU WALIZOTUMWA*
>>  _Hesabu 13:17-20  17 Musa akawapeleka ili waipeleleze nchi ya Kanaani, akawaambia, Pandeni sasa katika Negebu mkapande milimani,

18mkaitazame nchi ni ya namna gani; na watu wanaokaa ndani yake, kwamba ni hodari au dhaifu, kwamba ni wachache au wengi;

19na nchi wanayoikaa kwamba ni njema au mbaya; kwamba wanakaa katika matuo au katika ngome;

20nayo nchi ni ya namna gani, kwamba ni nchi ya unono au ya njaa, kwamba ina msitu au sivyo. Iweni na moyo mkuu, mkayalete matunda ya nchi. Basi wakati ule ulikuwa wakati wa kuiva zabibu za kwanza.

Angali pia na katika iingereza (NIV) hii mistari
*Numbers 13:17-20 17When Moses sent them to explore Canaan, he said, “Go up through the Negev and on intothe hill country. 18See what the land is like and whether the people who live there are strong orweak, few or many. 19What kind of land do theylive in? Is it good or bad? What kind of towns dothey live in? Are they unwalled or fortified? 20 How is the soil? Is it fertile or poor? Are theretrees in it or not? Do your best to bring back someof the fruit of the land.” (It was the season for thefirst ripe grapes.)* 

Hawa wapelelezi walitumwa kwa masuala ya kiuchumi kabisa  na walitumia siku 40 kufanya utafiti na aliwaambia waliete na matunda ya zabibu ili wasije na cooked data yaani wangeweza wasiende maana wangefanya utafiti wa kuitungia. Kazi ya utafiti ni kuwasaidia watu kuweza kufikiri. 

Angalia  Majibu ya Utafiti wao mstari 33 *Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi*.  Soma sura zote mbili ndiponutaelewa vizuri. 

Fikra zao zilishindwa kutafsiri kile kitu ambacho Mungu alitaka waone. Na Mungu alisema hawa watu nitachukuliana nao hadi lini?

*VITU VYA KUJIFUNZA KATIKA HABARI HII*
a). Mungu alikuwa anataka kuwaonesha tatizo ina maana alikuwa anawaandaa kifikra ili waweze kutafsiri na kujua namna ya kutatua tatizo maana kutatua tatizo ndio chakula chao.
*Mithali 3:5-6  Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako*

Fikra zako inabidi zikae mkao wa kutafuta suluhu ya tatizo, na akili zako zikifanya kazi na Mungu ujue kuwa lazima utafanikiwa.

b). Mungu aliijua Kanani vizuri sana, kwa sababu aliwaambia kuwa  ni nchi ya maziwa na asali. Na hawakujua kuwa maziwa na asali ni processed  products

*2* * Kulalamika ni ishara ya kuwa fikra zako hajioni jibu bali zinaona kikwazo*

*3* *Fikra ziliumbwa ziweze  kutafsiri changamoto ili ziwe fursa*

Ukisoma 2 Wakorintho 4:3-4 utona habari za kuwa ibilisi hupofusha fikra za watu . maana Mungu alipoumba changamoto au matatizo ni ili watu waweze kula.  Kwa sababu ukisoma biblia mwadamu aliumbwa na hamna mahali alipewa kitanda cha kulala. Maisha ya Mwanadamu 1/3 ni anatakiwa kulala. Sasa inatetegemea yeye mwenyewe atalala wapi kama kwenye majani, au kwenye ngozi au kama kitanda kizuri au ni banko. Ni wewe mwenyewe, kwenye biblia huwezi kuta kuna mahali Mungu alisema pawe kitanda.  Sasa ni jukumu lako kutengeneza kitanda. Sasa unapohitaji muujiza wa kitanda fikiri kwanza.

Katika biblia huwezi kuta kuna neno maendeleo, nilitafuta kwenye concordance (itifaki ya biblia) ni kitabu chenye kuonesha maneno yaliyomo kwenye biblia.  Sasa katika biblia neno maendeleo limefichwa kwenye neno *nuru* maana yake aliposema kuwe Nuru ina maana kuwe na maendeleo.

*4* *Ile kwamba mtu amekutangulia haina maana kuwa anafikiri vizuri kuliko wewe*  

Wana wa Israel walipokuwa jangwani, na wenzao waliotumwa kwenda kanani kupeleleza nchi ina maana ilitakiwa waweze  kufikiria mbele kuliko  wenzao.  Lakini Fikra zao zilikwama na wao waliishia jangwani. Na katikati ya Jangwani na Kanani kulikuwa na Fikra, japo imani walikuwa nayo ila fikra zao ziliwakwamisha na waliishia pale. Ila watoto wao ndio alienda kwenye nchi ya Kanani. Kwa hiyo angalia kinachokutoka katika kinywa chako.

Ukifikiri kama ni watu wanaokaa jangwani na wewe utabaki jangwani maana unaweza kwama hapa walipokwamia.  Kwa hiyo mtu anaweza akawa mkubwa lakini fikra zake bado ni ndogo.

*5* *Palipo na Malalamiko hapo ni fursa ya chakula fanya utafiti wa kulalamika kwako 
~~ *nani analalamika*
~~ *Kwanini analalamika*
~~ *Anamlalamikia nani*
~~ * Muda gani analalamika*
~~ *Malalamiko yake huwa yanajirudia kipindi gani*

Ukiona watu wanalalamika, basi wewe zifanye fikra zako ziweze kufikiri na fanya utafiti maana kuna chakula hapo.  Na hii ndiyo iliyotoa fursa kwa akina Kalebu na Joshua. Maana Mungu alipowaonesha matatizo wao walitafsiri kwa matatizo kama Fursa,

Kule kulalamika kwa wana wa Israel, kulisababisha wao kutokwenda Kanani ila watu wawili tu. Sasa piga hesabu watu waliotoka Misri walikuwa ni zaid ya million 2 lakini walioingia Kanani ni Wawili tu. Na hawa  ni watu walioweza kutafsiri na fikra zao zilifikiri tofauti na wengine.

Hata huko mbinguni naamini huwa wanacheka sana maana kuna wengine wanaona kuna majitu Mungu tunaomba kuyaondoa na wengine wanaona chakula.

*MFANO WA 2* *Hesabu 11:11-15* 
Hapa tunaona habari za Musa kuwa alianza kulalamika na alipokuwa anamlalamikia Mungu na katika kulalamika kwake kulitengeneza ajira ya watu 70.  Na ukiona kiongozi analalamika kuwa kazi zake zimemzidi basi anza kukaa mkao mzuri maana kutakuwa na kazi hapo.  Na wewe ukiungana na kulalamika kwake basi wakati anatangaza kazi zingine atakuacha kwa sababu wewe ni mlalamishi.

*MFANO WA 3* *Habakuki 1-2*
Sura ya kwanza tunaona Habakuki akilalamika kutokana na kutokuwepo haki. Na baada ya kulalamika Mungu alijibu kulalamika kwake.  Na alimjibu kuwa kwa njozi na njozi inamfanya aweze kufikiri.  Kwa sababu ukipewa njozi bila matatizo  inakuwa haina maana. *Vision must have problem to solve or must have value*
Na kama akili yako inaweza kusolve  matatizo ya watu basi ujue kuwa kuwa utakuwa demanded . na ndivyo ilivyotunavyouza kahawa ambayo bado iko katika hali ya kuwa ghafi. Na ukiweza kufikiri ina maana unaweza kubuni kiwanda cha kuweza kuprocess .
Fikra zako ili ziweze kufanya kazi Zaidi inatakiwa unapokuwa unaomba kwa Mungu unganisha na matatizo yaliyopo kwenye jamii yako na omba Mungu akuwezeshe kukusaidia kujibu hayo matatizo na ukienda na kanuni hii basi ujue utapata business idea,. Thamani ya Mwalimu ni uhitaji wa Kiroho wa wanafunzi. 

*Ombea Fikra zako mara kwa Mara ili Mungu aweze kuzifungua.  Na hapa ni mwanzo omba Mungu ataoe tena kibali cha somo hili ili tuweze kuendelea. Homework Tafuta mahali penye malalamiko maana pana chakula*
SEMINA ZIJAZO.


- 6 Novemba 2016 - Birmingham, Alabama USA
11 - 13 Novemba 2016 - Washington DC USA
Kumbuka kuziombea semina hizi,kusudi la Mungu lifanyike. Mbarikiwe!!
Kusoma Zaidi Mafundisho ya Mwl Mwakasege tembelea
*Facebook*
https://www.facebook.com/Christopher-Diana-MwakasegeMana-Ministry-132462780111984/
Youtube
https://www.youtube.com/channel/UC4p4lrpgpNd-9bHPgHJ4xWw
Ustream
http://www.ustream.tv/channel/mwakasegemanaministry
website
www.mwakasege.org

SEMINA IKO ITAKUWA LIVE YOUTUBE USTREM NA KWENYE www.mwakasege.org na www.kicheko.com
BARIKIWA NA YESU.
Felix…..

FAIDA ZA KIAFYA ZA KUTUMIA KITUNGUU SAUMU (GARLIC) FEATURED

Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.

Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umen'genyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu. 

Historia inaonesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika China mwaka 510 K.K na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Roma. Aidha wasafiri wa vyombo vya baharini na vijijini pamoja na wakulima barani Afrika walivitumia sana.

Mwaka 1858, mtafiti na mwanasayansi wa nyakati hizo, Louis Pasteur aligundua uwezo wa kitunguu swaumu katika kuua vimelea mbalimbali vinavyosababisha magonjwa, na hivyo vikaanza 

kutumika kama dawa ya kusafishia vidonda na kuzuia kidonda ndugu hasa zama za vita ya kwanza na pili ya dunia. Isitoshe, mpaka sasa zipo dawa kadhaa zilizotengenewa kwa kutumia jamii hii ya 

vitunguu swaumu ikiwemo dawa ya kusafisha mdomo (mouth wash) ingawa watumaiji wake wengi huilalamikia dawa hiyo kwa sababu ya harufu mbaya ya dawa hiyo inayowasababishia kunuka kwa mdomo.

Faida za vitunguu swaumu

Katika tafiti mbalimbali vitunguu swaumu vimeonekana kuwa na uwezo wa kutibu maambukizi ya bakteria, fangasi na virusi vya aina mbalimbali. Aidha husaidia kuzuia magonjwa ya moyo ikiwemo kuondoa lijamu katika mishipa ya damu na hivyo kusaidia katika kurekebisha shinikizo la damu. Faida nyingine za vitunguu swaumu ni pamoja na

Kutibu saratani ikiwemo saratani ya tumbo na utumbo mkubwa. Tafiti zinaonesha idadi ndogo ya wagonjwa wa saratani katika nchi ambazo wakazi wake wana utamaduni wa kutumia vitunguu swaumu kwa wingi.

Vitunguu swaumu husaidia kudhibiti kiwango cha sukari katika damu. Hata hivyo inashauriwa kwamba wagonjwa wa kisukari wanaotumia sindano za insulin wasitumie kitunguu swaumu kwa wingi mpaka watakaposhauriwa na daktari.

Huzuia kusanyiko la chembe sahani zinazosaidia kuganda kwa damu (platelet aggregation)

Husaidia ufyozwaji wa thiamin, hivyo kusaidia kuepusha mwili na ugonjwa wa beriberi

Ina kiasi kikubwa cha vitamini C ambayo husaidia kuzuia ugonjwa wa kiseyeye

Hutumika kutibu magonjwa nyemelezi kama toxoplasmosis, hasa kwa watu wenye upungufu wa kinga mwilini.

Ushahidi wa Kitafiti 

Katika utafiti uliofanyika nchini Czech ilionekana kuwa matumizi ya vitunguu swaumu yalisaidia sana katika kupunguza kusanyiko la lijamu (cholesterol) pamoja na mafuta yasiyofaa mwilini (low 

density lipoproteins) katika mishipa ya damu. Aidha, mwaka 2007 BBC iliripoti matumizi ya vitunguu swaumu katika kusaidia kumkinga mtumiaji dhidi ya aina fulani ya mafua 

iliyosababishwa na virusi. Mwaka 2010, ulifanyika utafiti mwingine ambao ulijumuisha wagonjwa 50 wenye shinikizo la damu sugu ambalo lilikuwa ni vigumu kudhibitiwa hata kwa matibabu 

yaliyozoeleka ya dawa na njia nyingine. Kama njia ya kuchunguza ufanisi wa vitunguu swaumu katika kutibu shinikizo la damu, baadhi ya wagonjwa hao walipewa vitunguu swaumu wakati 

wengine walipewa dawa isiyohusika na matibabu ya shinikizo la damu (au placebo). Ilionekana kuwa wale waliopewa vitunguu swaumu kama dawa ya shinikizo la damu walionesha maendeleo 

mazuri kwa vitunguu swaumu kuweza kushusha vizuri kiwango cha shinikizo la damu, hususani systolic pressure, tofauti na wale waliopewa placebo.

Nini siri ya kitunguu swaumu?

Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na mambo yafuatayo;

Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.

Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.

Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.

Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo inayotolewa baada ya kuvila.

Nini Madhara ya vitunguu swaumu?

Ukiacha faida zake, vitunguu swaumu pia vina hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na;

Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa au kunywa maji mengi.

Kwa baadhi ya watumiaji, vinaweza kuwaletea mzio au mcharuko mwili (allergies au inflammatory reactions)

Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha.

Huweza kusababisha hatari ya kuvuja damu, kwa sababu huzuia kazi ya seli sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda kwa damu kushindwa kufanya kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito, baada ya upasuaji au mara baada ya kujifungua.

Huingiliana katika utendaji kazi wake na dawa kadhaa kama vile warfarin, antiplatelets, saquinavir, dawa za shinikizo la damu kwa ujumla hasa calcium channel blockers, na antibiotiki za jamii ya quinolone kama vile ciproflaxacillin.

Aidha, vinaelezwa pia kuwa na madhara kwa wanyama jamii ya paka na mbwa.

FAIDA YA KITUNGUU SAUMU KINATIBU MARADHI MENGI BINADAMU ANAJISAHAU KUTUMIA KITUNGUU SAUMU. 

Kitunguu swaumu hakikosekani katika kila jiko duniani.Ni mmea maarufu sana kwa tiba.Kitunguu swaumu ni jamii ya yungiyungi.Kitunguu swaumu kilicho bora zaidi duniani ni kinachotoka misri kwasababu ya tabia ya ardhi yake na mto nail.Kitunguu swaumu kina harufu ya kipekee isiyowapendeza watu wengi ingawa kimebeba siri nyingi za tiba.Kwa ajili hiyo maana yake kilatini ni HARUFU ICHOMAYO.

Ili kuepukana na harufu ya kitunguu swaumu baada ya kukila,kula tofaa au tafuna majani mabichi ya naanaa,au kunywa maji yaliyotokosewa karafuu.Kitunguu swaumu kitapoteza nguvu ya tiba iwapo kitapikwa na kila kinapowekwa muda mrefu ndipo nguvu zake huongezeka (baada ya majani yake kukauka kabisa).

Kitunguu swaumu kimekusanya protin 49%,sulphur 25%,kiasi fulani cha chumvi,homoni zitoazo nguvu za kiume,viuaji sumu,vikojozavyo,vitoavyo safura,vinavyoteremsha hedhi,vimeng'enyo vyenye kuyeyusha mafuta na viini vyenye kuua minyoo.Kila utafiti unapoendelea ndipo faida na maajabu ya kitunguu swaumu yanapoongezeka.

BAADHI YA MARADHI YANAYOTIBIWA NA KITUNGUU SWAUMU;

1.Kiua sumu

2.Kisafisha tumbo

3.Kiyeyusha mafuta(cholestro)

4.Huzuia mvilio wa damu

5.Kusafisha njia ya mkojo

6.Kutibu amoeba

7.Kuzuia kuhara damu(Dysentery)

8.Tumbo kushindwa kumeng'enya(Indigestion)

9.Gesi

10.Msokoto wa tumbo

11.Typhoid

12.Kidonda kilichooza

13.Dondakoo

14.Mabaka

15.Baridi yabisi(Rheumatisim)

16.Mishipa

17.Uziwi

18.Virusi vya homa ya mafua(Influenza)

19.Mafua

20.Saratani(Cancer)

21.Kifaduro

22.Kifua kikuu cha mapafu

23.Kipindupindu

24.Kutoa minyoo

25.Upele

26.Kuvunjavunja mawe katika figo

27.Mba kichwani

28.Kuupa nguvu ubongo

29.Kuupa nguvu fizi

30.Kuzuia meno kung'ooka

31.Nguvu za kiume

32.Maumivu ya kichwa

33.Kizunguzungu/kisunzi

34.Kutuliza maumivu ya meno

35.Kujenga misuli na kutia nguvu

36.Mkakamo wa ateri(Arteriosclerosis)

37.Shinikizo la damu

38.Kinga ya tauni na ukimwi

39.Magonjwa ya macho

KITUNGUU SAUMU

kimekuwa kikitumika kutibu na kuboresha afya ya mwili na hivyo kumfanya mtumiaji awe mrembo na mwenye afya bora.

Matumizi ya kitunguu saumu kibichi yamekuwa yakisaidia vitu vingi sana mwilini.

Baadhi ya hayo ni pamoja na kupambana na virusi, bakteria, fangasi na pia sumu mbalimbali hasa zile zinazosababishwa na baadhi ya vyakula mwilini.

Kutokana na hilo, matumizi ya kitunguu saumu kama tiba na kipodozi, ni jambo linalopendekezwa na wataalamu wa urembo wa asili.

Katika matumizi yake kitunguu saumu hutumika kwa kula na wakati mwingine kupaka, ambapo hili hutegemea zaidi na mahitaji au matatizo ya mtumiaji husika.

Pamoja na njia hizo nilizotaja hapo juu, lakini wataalamu wanashauri ulaji wa kitunguu saumu kibichi kila siku, kwani husaidia kuboresha afya ya muhusika.

Ikiwa utashindwa kukitafuna chenyewe, unaweza kuchanganya kwenye chakula kingine ambacho unatumia alimradi tu ukipate kikiwa halisi.

Kwenye urembo, kitunguu saumu husaidia kuondoa matatizo yafuatayo;

Chunusi

Changanya kitunguu saumu kilichosagwa kijiko kimoja na kijiko kimoja cha juisi ya ndimu. Chukua pamba na paka sehemu zote zilizoathirika. Kaa na mchangyiko huo kwa muda wa dakika 15 hadi nusu saa.Ikiwa utaendelea kwa muda wa wiki moja. Tatizo la chunusi litakuwa limeondoka kabisa.

Kunyonyoka kwa nywele

Ni kwa muda mrefu sasa kitunguu saumu kimekuwa kikitumika kama tiba ya kunyonyoka kwa nywele. Unachotakiwa kufanya ni kutumia mafuta yake kwa kupakaa kwenye ngozi ya kichwa kila siku kabla ya kulala. 

Fanya hivyo mara kwa mara kwa muda usiopungua miezi mitatu na utaona matokeo yake. Ikiwa utakosa mafuta yake, si vibaya ikiwa utatumia kitunguu chenyewe kilichosagwa kwa kupaka kwenye ngozi ya kichwa kila siku usiku na kuosha asubuhi yake.

Fangasi vidoleni

Kupambana na fangasi kwenye vidole vya miguu na mikono, unashauriwa kutumia kitunguu saumu kilichosagwa kwa kupaka eneo lililoathirika. Hakikisha unakaa nacho usiku kucha ukiwa umevaa soksi ama glavu. Fanya hivyo kila siku hadi utakapoona muwasho na maumivu yameisha.

MBA

Paka kitunguu saumu kilichosagwa katika ngozi ya kichwa ama sehemu yeyote iliyoathirika. Hakikisha unatumia hadi pale ugonjwa utakapokuwa umetoweka kabisa.

MATUMIZI KATIKA NCHIMBALIMBALI:

kitunguu ni kiambatanisho muhimu kidishi kimaendeleo katika sehemu nyingi ulimwenguni.

Zamani Egpta iliheshimiwa kuwa ya hadhi ya kimungu.

MAANDALIZI YA KITUNGUU SAUMU KIMADAWA:

Kitunguu saumu na asali. Jaza chupa ya glasi na vitunguu saumu vilivyomenywa na

kukatwa katwa polepole mwaga katika asali ya kwamba inajaza nyufa katikati ya fundo ya

kitunguu. Weka glasi kwenye sehemu ya joto yenye c 20oc. Katika siku mbili hadi wiki nne,

asali itanyonya juisi ya kitunguu saumu na kitunguu hicho kitachechemea na kutoingiza

mwanga usichuje. Tumia katika muda wa miezi 3.

Kitunguu Saumu dawa ya kikohozi

Ponda kijiko cha chai cha kitunguu saumu katika kipimo hicho hicho cha sukari au asali.

Tumia mara moja k.mf. kwa kikohozi.

Kitunguu saumu mafuta. Weka g 200 za vitunguu vilivyokobolewa saga kitunguu saumu na

kuweka kwenye chombo cha glasi na ongeza mafuta ya kutosha (au vizuri mafuta ya chakula)

funga. Funga jagi kwa kubana vizuri, na weka ikae kwenye sehemu yenye joto kama C 20

kwa siku tatu. Tikisa mara chache kila siku. Halafu weka kwenye sehemu ya baridi, bila

kuchuja. Tumia katika muda wa mwezi mmoja.

Kitunguu saumu „tinkcha“. Loweka g 200 za vitunguu vilivyomenywa na kukatwakatwa

katika lita moja ya brandi au alikoholi 40-50%, kwa siku 14 kwenye C 20° katika chupa

yenye kufungwa vizuri bila kupitisha hewa. Tikisa chupa hiyo mara nyingi kwa siku. Chuja

vipande vya kitunguu saumu. Tinkcha inakaa muda wa mwaka.

MAPENDEKEZO YA MATUMIZI

Kula kitunguu saumu kibichi- hii ni bora.

Tumia katika kupika.

Kula vitunguu saumu vingi kuzuia magonjwa. Kitunguu saumu ni safi sana kwa mfano kuna

usemi kwamba, chakula chako kiwe ndiyo dawa yako, na dawa yako chakula chako. Hii ni

kweli tu, hata hivyo, kwa kitunguu saumu kibichi, kama ilivyo vitu vingi vyenye nguvu

vinaangamizwa katika kupikwa. Vitunguu saumu vibichi vinatia nguvu katika mfumo wa

kinga ya maradhi. Matumizi kawaida ya vitunguu saumu yameonyeshwa katika kupunguza

madhara ya magonjwa ya moyo, kiharusi, kansa, msukumo wa damu na homa ya mafua

Makali (flu). 

Tunashauri kwa nguvu ya kuwa wanaoteseka kwa UKIMWI (AIDS) waweke

kitunguu saumu katika chakula chao cha kila siku, kupunguza nguvu ya magonjwa mengine.

Kwa sababu inafanya mara mbili, kwa matumizi ya nje na kwa ndani kama dawa ya kuua

wadudu, vitunguu saumu ni masaada wa kutibu magonjwa yote ya kuambukiza; Toifodi,

minyoo, bilhazia, malaria, damu yenye maambukizo na sumu n.k. Zaidi yake vitunguu saumu

vinaimarisha kumbukumbu, hupunguza shindikizo la damu na Homa, na vinafanya kazi

kupinga ugumu wa kuta za ateri (hardening of arteries). Vitunguu saumu pia vinapinga virusi

na dhidi ya kinyume cha mambo ya fangasi.

1.Majipu au uvimbe na chunjua.

Saga vitunguu saumu vibichi na funga vilivyopondwa kwenye sehemu ya jipu, uvimbe au

Chunjua mara mbili kwa siku na gandamiza. Anza matibabu haya mapema iwezekanavyo.

2. Amiba.

Katakata vitunguu saumu sawasawa vipande vidogo na chukua kijiko kikubwa 1 pamoja na

Chai mara tatu kwa siku (usitafune, kusaidia kupinga kutoa harufu mdomoni). Endelea na

Matibabu haya kwa siku 5. I (H-M Hirt) aliponywa mwenyewe toka Amiba kuharisha

damu kwa Tiba hii.

3. Malaria.

Katakata vitunguu saumu sawasawa. Meza kijiko kimoja cha vitunguu hivi mara tatu kwa

Siku na kunywa lita 2 za limao glasi ya chai kwa siku. Endelea na tiba hii kwa siku 5.

Angalia pia ukurasa wa 8 kwa ajili ya malaria.

4. Kisukari, shindikizo la damu 

kinga ya ugumu wa kuta za arteri (hardening of the

arteries).

Kula vitunguu saumu kwa wingi, vitunguu saumu na vitunguu vinapunguza sukari katika

damu na kusawazisha damu ya cholesteroli, na shindikizo la damu. Badala yake chukua

matone 20 ya vitunguu tinkcha mara 3 kwa siku, basi hii ni pungufu ifuatayo:

5. Kikohozi, homa, sinusitis na kuvimba koo.

a) Kula klovu ya vitunguu saumu mara tatu kwa siku.

b) Chukua kijiko cha chai cha kitunguu saumu asali kila masaa machache.

c) Watoto wanaweza kutumia kijiko cha chai cha kitunguu saumu

mchanganyiko kila baada ya masaa machache.

d) Chukua kijiko cha chai cha kitunguu saumu mafuta mara 6 kwa siku.

6. Kandika.

Chukua kijiko cha chai cha kitunguu saumu au kitunguu saumu yenye asali, kila masaa

machache. Weka mdomoni kwa muda mrefu iwezekanavyo.

7. Fangasi inayoambukiza pamoja na ugonjwa wa ukungu kwenye vidole vya miguu.

Funga sehemu zilizoathirika kwa juisi ya vitunguu saumu vibichi vilivyopondwa au

mafuta.

8. Homa ya matumbo na maambukizo mengine.

Kama itatokea homa ya matumbo, bacillary, kuharisha damu, kifua kikuu, kipindupindu,

trypanosomiasis (ugonjwa wa kusinzia): Siku zote ongeza kitunguu saumu kwa tiba ya

kawaida.

9. Kinga ya mishipa ya damu.

Kitunguu saumu siku zote kinafanya damu kuwa laini na kukinga kutengeneza damu

kuganda ambayo inasababisha shida ya thrombosis. Hii ni muhimu kwa wagonjwa wanaolala kitandani kwa muda mrefu.

10. Kuota meno utotoni.

Futa ufizi kwa fundo la kitunguu Saumu.

Kitunguu thaum kina harufu ya pekee isiyowapendeza watu wengi, ingawa kimebeba siri nyingi za tiba. Kwa ajili hiyo maanayake kwa kilatini ni : harufu ichomayo, na kwa kiarabu lugha ya Quraan huitwa: fuum, nayo ndio sahihi zaidi; kwasababu thaum ni lafdhi ya kihieroglifu ya kifirauni (hieroglyphic).

Allah S.W amesema:

" Na (kumbukeni habari hii kadhalika) Mliposea: Ewe Mussa! hatuwezi kusubiri chakula cha namna moja tu, basi tuombee kwa Mola wako atutolee vile vinavyooteshwa na ardhi kama mboga zake, matango yake, fuum (kitunguu thaum) zake, adesi zake na vitunguu vyake." (2:61)

Iliandikwa katika piramidi (pyramid) huko Misri tangu miaka 4500 iliopita kuwa kitunguu thaum kilikuwa wakipewa wajenzi ya piramidi. Walikuwa wakila kitunguu thaum ili wapate nguvu na nishati.

Mwandishi wa kitabu juu ya tiba zinazotokana na kitunguu thaum alimnasihi mfasiri wake kuwa " Iwapo unataka nguvu, nishati na uwekevu basi kula tembe ya kitunguu thaum na glasi ya maji kila siku kabla ya kula chakula. Daud Al-Antaky ameeleza katika kitabu chake cha Tadhkira kuwa kitunguu thaum hupoza zaidi ya maradhi 40.

Wale wapiganaji wa miereka wa huko Roma walikuwa wakila kitunguu thaum kabla ya kupigana ili wapate nguvu na wepesi.

Imethibitishwa kisayansi kuwa kitunguu thaum husafisha damu kutokana na mafuta (cholestrol) ambayo husababisha magonjwa ya mishipa ya ateri na maradhi ya moyo, na pia husafisha damu kutokana na vijidudu na maikrobati kuliko (antibiotic) vengine. Pia imethibitishwa kwa kuzuia kuenea kwa sumu ya nyoka katika mwili wa mwanaadam na pia husafisha maida kutokana na vimelea (parasites).

Rais wa matabibu, Ibn Sina amesema kuhusu kitunguu thaum: "Kitunguu thaum hulainisha na kuondoa gesi, hutoa vidonda katika ngozi, huhifadhi maji. Vumbi lake likichanganywa na asli akipakwa mwenye ukoma litamfaa, kitunguu thaum humfaa mwenye maradhi magonjwa ya mishipa na nyonga (sciatia). Maji yake (yaliotolewa kwa kupikwa) hutuliza maumivu ya meno, vilevile hufaa kwa kikohozi.

Kitunguu thaum kimekusanya protein 49% mafuta muhimu ya sulphur 25% na kiasi flani cha chumvi, homoni (hormones) zitiazo nguvu za kiume na vinavyoteremsha hedhi.

BAADHI YA MARADHI YANAYOTIBIWA NA KITUNGUU SAUMU:

Kiua Sumu:

Saga tembe tano za kitunguu thaum, changanya na asali kikombe kimoja kilichochanganywa na habbasouda na kunywa papo hapo. Kunywa asubuhi na jioni. Paka mafuta ya kitunguu thaum pahala panapouma iwapo ni sumu ya nyoka au paka nje ya tumbo iwapo umekunywa sumu.

Kusafisha tumbo:

Kabla ya kula chakula, meza tembe za kitunguu thaum na baadae kunywa maji ya shimari yaliyochanganywa na asali kwa muda wa wiki moja.

Kiyeyusha mafuta (Cholestrol):

Unapokula chakula kila siku, weka katika kachumbari kiasi cha tembe 2 vilivyosagwa ule pamoja na kachumbari.

Kiongeza mkojo chenye kusafisha njia za mkojo:

Chemsha vizuri hairi, na baada ya kupoa tia tembe 3 za kitunguu thaum zilizosagwa. Kunywa kinywaji hicho kila siku kabla ya kula na kunywa juisi ya limau/ndimu.

Kuharisha damu (Dysentery):

Chukua tembe ya kitunguu thaum uikatekate na uile; fanya hivyo kwa muda wa wiki moja na bora zaidi ukinywa na mafuta ya zaituni kijiko kimoja.

Gesi na Indegestion:

Kunywa juisi ya pea iliyochanganywa na tembe 3 za kitunguu thaum kabla ya kulala kila siku.

Kutibu Typhoid:

Kata tembe 5 za kitunguu thaum, changanya ndani ya maziwa ya moto yaliyochanganywa na asali kunywa kabla ya kulala. Pia paka uti wa mgongo mafuta ya kitunguu thaum yaliyochanganywa na mafuta ya zeti, na asubuhi vuta moshi wa kitunguu thaum kwa muda wa dakika 5.

Kidonda kilichooza:

Ponda kitunguu thaum mpaka iwe laini kama marhamu halafu jifunge nacho kwa kutumia bendeji, japo kitawasha lakini kitazuia ugonjwa wa gangrene ambao unaweza ukapelekesha kukatwa kiungo. Vilevile unaweza kusafisha kidonda kwa kuchanganya kitunguu thaum kilichosagwa kikatiwa maji vuguvugu (warm water) na kikasafishwa kidonda.

Mishipa:

Kata tembe za kitunguu kitunguu saumu na umeza kwa maziwa ya moto (sio moto sana) yenye matone ya ambari kabla ya kulala kila siku, dawa hii huipa mishipa nguvu.

Homa ya mafua (Influenza):

Kunywa juisi ya machungwa na juisi ya limau zilizochanganywa na tembe 7 za kitunguu thaum kunywa juisi hiyo kabla ya kulala. Vuta moshi wa kitnguu thaum.

Mafua:

Meza tembe za kitunguu thaum baada ya chakula pamoja na juisi ya kitunguu thaum iliyochanganywa na juisi ya limau pamoja na kuvuta moshi wa kitunguu thaum.

Saratani (Cancer):

Katika kitunguu thaum kuna kiini kinachozuia saratani, kwa kila mgonjwa wa saratani anashauriwa ale kwa wingi kitunguu thaum na karoti (carrot).

Kifua kikuu (cha mapafu):

Kila asubuhi kabla ya kula chakula meza tembe 3 za kitunguu thaum, saga ule pamoja na mkate na jioni vuta moshi wake.

Kipindupindu (cholera):

Ili kujikinga na maradhi hayo wakati kikienea, kula kijiko kimoja cha kitunguu thaum kilichosagwa na kukorogewa katika asali baada ya kila chakula.

Kutoa minyoo:

Ponda tembe 3 za kitunguu thaum, tia ndnai ya maziwa na kunywa (bila kutia sukari) jioni kabla ya kulala na asubuhi kunywa mafuta ya mbono.

Upele:

Chukua tembe 5 za vitunguu thaum uvisage na uvikoroge katika shahamu na paka pale penye upele kuazia jioni mpaka asubuhi na ukoshe kwa maji ya moto tumia kwa muda wa wiki moja.

Mbaa kichwani:

Ponda uzuri vitunguu thaum 3 na uvikoroge katika siki ya tofaha (Apple vinegar) katika chupa ya bilauri (sio plastiki) na uache juani kwa muda wa wili moja. Baada ya hapo jipake kichwani pamoja na kusugua kwa muda wa wili 1 na baada ya wiki jipake mafuta ya zeituni.

Nguvu za kiume:

Saga kitunguu thaum kitie ndani ya mafuta ya zeti na weka katika moto mdogo mdogo mpaka iwe rangi ya manjano na tia katika chupa na wakati wa haja jipake katika dhakari na osha baada ya saa moja.

Kujenga misuli na kutia nguvu:

Kila siku kabla ya kula kunywa kikombe kikubwa cha maziwa ya ngamia yaliyotiwa tembe 2 za kitunguu thaum iliyosagwa. Kunywa kwa muda wa mwezi mmoja mfululizo.

Kinga ya taunni na ukimwi:

Ngao kubwa ya maradhi mabaya ni Kumcha Allah S.W mwanzo na mwisho wa siku. Chukua juisi ya kitunguu thaum uichanganye na asali na unywe utafanya hivo pamoja.

KITUNGUU SAUMU. 

tangu kale kimekuwa kikijulikana kama 'dawa ya kushangaza' na kutumiwa na watu wengi katika kutibu mafua na influenza. Miongoni mwa faida za kitunguu swaumu ni kuzuia kupatwa na magonjwa mbalimbali na maambukizo ya virusi. Hivyo kitunguu swaumu hujulikana kama antibiotiki ya asilia. Uchunguzi umeonyesha kwamba kula kitunguu swaumu kunapunguza kushadidi ugonjwa wa influenza na hata kuzuia kupatwa na ugonjwa huo. Vilevile kula kila mara kitunguu swaumu, huzuia kupatwa na magonjwa ya moyo, kwani kitunguu swaumu huzuia damu isigande kwenye mishipa ya damu. 

Halikadhalika kitunguu swaumu ambacho pia ni kiungo muhimu cha chakula kina potassium, na hivyo watu wenye ugonjwa wa shinikizo la damu wanashauriwa kula vyakula vilivyopikwa kwa kitunguu swaumu.

Si vibaya kujua kuwa katika uchunguzi uliochapishwa mwaka 2001, imeelezwa kwamba, kitunguu swaumu kina athari kubwa na nzuri pale kinapochanganywa na baadhi ya dawa nyinginezo katika kutibu Ukimwi au HIV. 

MADHARA YAKE:

Kitunguu saumu kinaweza kukera ngozi hasa baada ya kutumia kwa muda mrefu. Epuka

kuhusisha kwenye macho.